Yanayojiri barabara ya Dar-Mtwara

Ee bana eeh!!!!
Nitasafiri kwa teksi kweli toka Mtwara hadi Mwanza kwa hali hii?
Ngoja nimpigie simu mzee Pombe Magufuli!

Hakuna wazir mwongo km magufur amekalia kukariri km za barabara toka mwaka 2010 napita hii barabara hakuna mabadiliko, utamsikia nimempa miez sita mkandaras amalize inakwisha cha mana hakuna. huyu kwangu ni mpiga kelele 2 hafai. wanawalaza njiani wa2 kila wakati.
 
Ni eneo baya sana Mimi nilikuwa Mtwara kama wiki mbili zilizopita lakini hali eneo la km 60 ni korofi sana. Mabasi mazuri kama HAMANJU yanapoteza ubora wake kutokana na barabara hasa eneo hilo.

Huyu mwenye HAMANJU ana roho ngumu basi nzuri km lile kulitoa sadaka mana litachoka mapema kwa yale mahandaki.
 
Kwani Mbunge wa huko ni Mheshimiwa nani?

We nawe sema wabunge! wako kina gasia mkuchika, membe, chikawe, majaliwa, njwayo, murji bungala almarufu *****. tena utashangaa wengi ni mawazir lakin ni bure kabisa.
 
Barabara hii inafadhiliwa na pesa za kodi zetu na si hela ya Bush.
Mkandarasi hapa ni Al Kharafi Contractors.
Kampuni hii ilipewa onyo nafikiri mwaka juzi na Mzee Pombe Magufuli, na walipewa miezi 5 kumaliza kazi hiyo.
Leo muda unayoyoma tu.

Hujiulizi kwa nini Mkandarasi hachukuliwi hatua?
 
Hapa kama sijakosea ni Muhoro, ili eneo nilisha wahi kukwama kwa muda wa masaa zaidi ya 4 mwaka 2007 na mwaka jana nilitoka huko bado hali ni ile ile.

inaonekana wewe ni mgeni ktk njia hiyo manzese na muhoro ni sehemu mbili tofauti maeneo ya muhoro kwa sasa ni lami. Kama unaelekea somanga kutoka muhoro ndipo barabara inakuwa chafu sana hasa maeneo ya malendego mpaka manzese
 
Umuhimu ni kujenga bomba la gesi fasta toka Mtwara hadi D'salaam na siyo barabara!
 
Tatizo ni moja.........hawa watu wa eneo husika hawahitaji hiyo barabara.....

1) inawezekana hawafanyi biashara kwa kutumia barabara hiyo
2) Hawasafiri kwa means ya barabara
3) kwanza lami inasababisha magari yanakimbia yanagonga wanavijiji na hasa watoto.....What the heck!!!

:sleepy::sleepy::sleepy::sleepy:
 
ila watu wa kusini kiasi fulani wana hitilafu vichwani.
gesi
mafuta
korosho
ni vitu ambavyo ni most wanted duniani. lakini ukiyaona makazi yao na hali ya maisha wanayoishi huwezi kuamini ndio wanaoikumbatia ccm kama TABORA

Kabla ya kupost kitu,muwe mnatafakari kwanza...

Sasa hao watu wa kusini,ulitaka washikamane wachukue majembe wakachimbe gesi na kuuza nje?
Ulitaka wachukue sululu na mapipa wakachote mafuta wauzie mikoa mingine?
Ulitaka wachukue korosho zao wakodi meli wakauze nje ya nchi?

Wachangiaji wengine bana!
 
kwa habari za chini ya kapeti ni kmamba ujenzi umesimama coz kampuni haina pesa na wanadai tsh. 11 bilioni kwa kazi waliofanya. Kwa hiyo usishangae mkandarasi hachukuliwi hatua licha ya deadline ilowahi kutolewa na magufuli j.g serikali ndio inachelewesha barabara hiyo. Halafu jamani mi naomba mnieleweshe. Kwa nini serikali inapenda kutekeleza miradi mingi kwa wakati mmoja wakati inajua wazi kuwa bajeti hairuhusu? Mfano utaona barabara nyingi inchini zinajengwa kwa kipitndi kimoja. Kwa nini zisijengwe kwa awamu? Kadhalika miradi mingine?.
 
Hiki kipande cha Nyamwage~ Somanga ni KM 60 na Magufuli alashakisemea mjengoni na hata ukipita sasa WAKANDARASI wapo pale wanawajibika ikiwa pamoja na kuwasaidia wanasao; kimsingi kama km 30 zishafanyiwa kazi zimebaki 30 na sehemu mbovu zaidi ni kama KM 10 tu; kutokana na mvua zilonyesha mfululizo ndizo zinazochelewesha jitihada hizi; lkn mimi binafsi nina Imani sana na Magufuli ktk hili atalisimamia vyema kama ilivyo sehemu zingine.
Panapo hitaji sifa za haki wapewe sifa, Kusini ilikua tatzo jamani du"
 
Raia wanashangaa shangaa shangaa tu
Jamaa wa maroli wanacheka
Eti wao wamezoea kulala njiani hivyo hawana presha taratibu kama kumsukuma mlevi

Unaongea hayo sasa kwa mshangao mkubwa...

Unapajua Daraja la Mkapa? Unajua watu walikuwa wanachukua mpaka siku 7 Dar-Mtwara?
Unajua watu walikuwa wanatumia meli Dar-Mtwara kipindi hicho?

Kwa watu wa kusini hicho ni kipande kidogo sana cha matatizo wakilinganisha na walikotoka..
Na si kwamba haitengenezwi,inatengenezwa,sema tatizo ni jiografia ya eneo husika,na matatizo mengine nisiyoyajua..

Vipi ulipata kusikia kilio cha "Kibiti - Lindi" enzi zile bungeni?
Ulipata kusikia Mbunge aliyeingia Bungeni akiwa amejaa tope,na Spika kipindi hicho akamlaumu kwa kitendo hicho? Alijibu kuwa kila siku anapopiga kelele barabara ya kusini itengenezwe,mawaziri hawaelewi taabu ya watu wa kusini... Sasa ameamua awaoneshe "live" labda wataelewa..
 
ila watu wa kusini kiasi fulani wana hitilafu vichwani.
gesi
mafuta
korosho
ni vitu ambavyo ni most wanted duniani. lakini ukiyaona makazi yao na hali ya maisha wanayoishi huwezi kuamini ndio wanaoikumbatia ccm kama TABORA



Ni kweli kabisaa. Tatizo la kule ni kwamba wameweka uislam mbele mno na shule hawataki bali madrasa. Mmaraba anaona bora ampeleke mtoto shule akasome koran tukufu, shule ambayo ndiyo msingi wa huyo mtoto wanaona si bora. Na ndiyo maana wanaliwa huku wakiwa macho. Anyways naweza kuwa bias kwani hata sie waTZ wengine tunaliwa na viongozi na hatufanyi chochote kazi yetu ni kusema tu na kulalamika humu JF na vijiweni huku viongozi wanatucheka. So all in all, we are equal na watu wa kusini (hatuna power).
 
Back
Top Bottom