Yanayoendelea nchini: Nape atupa madongo

Hatutangazi dini hapa tunatangaza ukweli. Hata katika dini sharti utubu uonyeshe umetubu lakini Nape hajatubu. Biblia hiyo ya wewe mkristu lazima itakuambia utubu ili uuone ufalme wa mbingu. Nape hawezi maana hajazitubu dhambi zake na udhalimu aliouunga mkono huko nyuma. Damu za kina mwangosi na wengine zimo mikononi mwake pia. Huyu anachotafuta hapa ni sympathy ya watu kama ninyi mnaosahau nini kilitokea huko nyuma. Bashe ni ccm na ni mtu pekee ambaye ni mkweli wengine ni vibwengo tu
 
Siasa wanaiweza wanasiasa lakini pia hata wale wanaoamua kuingia kwenye siasa wakiwa na dhamira ya dhati wataiweza pia
Tena wapo watu timamu na wanaweza kuliko wale waliofanya siasa ni kazi ya kudumu.
 
Nape alipewa pembe lakini hakubaini kuwa ni za plastic akataka kupiga ukuta!.Yeye yuko nje syndicate hivyo yote atakayosema hayana msaada wwt kwa upande wake zaidi ya kuonekana kiburi tu.Kingine huyu ana radhi ya watu Mtama kwa kuiba ushindi wa S.Mathew na kisha kumfunga,arudi Nyangao akakonyoe korosho tu
 
Siasa wanaiweza wanasiasa lakini pia hata wale wanaoamua kuingia kwenye siasa wakiwa na dhamira ya dhati wataiweza pia
Siasa ni taaluma ngumu kuliko zote,kwani licha ya mikakati yake kupangwa gizani lakini ufanisi wake unatakiwa machoni pa watu.Namaanisha kuwa na mpangilio wa matamshi na vitendo utakaokuwezesha ku influence kundi kubwa la watu.
 
Kauli hii ya Nape wewe unaichukuliaje?
"Tulikuwa tunamwita mzee wa watu mgonjwa, lakini pengine sisi ndio tulikuwa na mgonjwa zaidi".
Au hii hapa.
" Siasa ni kuparurana, wakati wa uchaguzi tuliparurana na yamepita hayo hamna haja ya kuchukiana"
Ni wazi anaomba msamaha kisiasa, na hawezi kwenda zaidi ya hapo.
 
Siamini kama asilimia kubwa ya vijana wa kitanzania ni mapunguani kiasi hiki. Nadhani gene ya kuzungusha mikono ipo locus moja na pumbavu. Maana mtu anakoment tu bila hata ya kuisoma post kinagaubaga. Hiyo tweet ya Nape tarehe haziendani na jinsi title ya mwanzisha thread alivyo jitabanaisha.
Mijitu inainatiririka tu.
Nadhani kusoma vitabu inatakiwa iwe amri ili kuokoa kizazi hiki.
 
Ila kiukweli huyu mzee anakera sana,na anahitaji roho ngumu sana tena ya kizandiki kumkubali!!
Wengi wanampamba ni kwa ukabila tu lkn ni mtu ambaye hafai hata kuwa kiongozi wa kitongoji
 
Naona nape toka yule mhaya luge amuingingize choo cha kike now days haish kutapa tapa
 
Nape, Sumaye,Lowasa,............................ ni sehemu ya matatizo wanayo pitia kwa sasa.
 
Siri ya mtungi ajuaee kata .Nape ni Kata ya huu mtungi .haya madongo ni ya muhimu sana kuzingatiwa maana ndio ukweli wa siri za mtungini .eeehhe Mungu tusaidie majanga haya tuyapite tukiwa salama.Amina
 
Nape alishawahi sema Lowassa in maiti haiwezi kuingia ikulu. Leo Lowassa amekuwa shujaa wa Nape..???
Wanasiasa hawatatuletea maendeleo zaidi ya chuki tuu. Maendeleo huletwa na wewe mwenyewe
Haijalishi kwani alikuwa hajui alitendalo kama ni ovyu .ila sasa ametambua na anajirudi ndivyo tulivyo binadamu na kwa Mungu kwake ni mwingi wa kusamehe .kwahiyo hatuna budi nasi kumsamehee
 
Wewe kweli msahaulifu muulize mbona aliendelea nao mpaka baada ya uchaguzi? Hivi ninyi watu mnashindwa kujua kuwa ccm wote wanaonyimwa nafasi walizozitaka ndiyo wanakua wa kwanza kutetea wapinzani ama kujiunga na upinzani? Lowasa asingekua cdm kama angefanikiwa kupewa nafasi na ccm. Nape hasira ya kutemwa uwaziri anajifanya yupo na kina Lissu aliokua anawapinga. Sympathy tu huyu anatafuts
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…