Yametimia, ndege ya ATCL, Dash8-Q400 angani

Yametimia, ndege ya ATCL, Dash8-Q400 angani

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,916
Ndege ya ATCL angani ikipasua anga na mawingu kwa ajili ya Test Flight. Sasa ni tayari kwa safari ya kuja nyumbani.

Alama ya Twiga wetu inaenda kuruka na kutambaa katika milima na mabonde ya Tanzania. Tunarudi tena katika anga la Tanzania. Nia ya dhati iliyotumika kulifufua shirika hili, itumike pia kutuweka watanzania kama wamoja, kwa chuki na uhasama wa "kuminywa demokrasia", turudishwe na tuwe wamoja.

Tunaenda hatua kwa hatua,kwa ile kanuni yetu ya "JF be the first to know", welcome back home.

The Wings of the Kilimanjaro

image.jpeg
 
Maneno yako hapo juu yamenikumbusha wimbo huu

Kuwasha mwenge,kuwasha mwenge
Nakuuweka Kilimanjaro,

Umulike hata nje ya mipaka yetu
Ulete tumaini ,

Pale ambapo hapana matumaini
Upendo mahali ambapo pana chuki
Na heshima ambapo pamejaa dharau ......
 
Mimi hofu yangu ni muda wa safari kuwa mrefu hivyo kushindwa kushindana na Fastest katika same root na hivyo kukosa faida na kushindwa kukua kibiashara. Sio mikoa yote ina idadi kubwa ya wananchi wanaweza kumudu kupanda ndege. Jamaa waumize kichwa na kufanya restructuring ya shirika sasa
 
Haikunji matairi au?
Rubani na ndege yenyewe haina muda wa kukunja matairi, ni mwendokasi kwa kwenda mbele- Tumechelewa kweli kweli. Inawahi kuja kuwatumikia wadanganyika na kama alivyosema waziri itatua viwanja vyote nchini. Ndege wakijifanya wendawazimu, mapangaboi yanapata mboga.

Maujanja ya kaka Kagame hayo!
 
Mimi hofu yangu ni muda wa safari kuwa mrefu hivyo kushindwa kushindana na Fastest katika same root na hivyo kukosa faida na kushindwa kukua kibiashara. Sio mikoa yote ina idadi kubwa ya wananchi wanaweza kumudu kupanda ndege. Jamaa waumize kichwa na kufanya restructuring ya shirika sasa
Mbona ishaandikwa humu mara nyingi tu kuwa safari ya jet ya saa moja na robo hii inatumia saa moja na nusu hivi. Tofauti ya speed sio kubwa sana.
 
Back
Top Bottom