Yamenishinda ya kufuga nywele ziwe ndefu maana zinauma kwenye kuchana

Agrarian

Member
Jan 8, 2018
18
16
Nimejitahidi kukaa na nywele kwa miezi sita, lengo ni kuzi-maintain ili nywele ziwe ndefu ndo iwe kama style yangu mpya.

Kufikia sasa nimedhamiria kwenda salon kuzinyoa tu maana nimeshindwa kwenda nazo sawa. Changamoto kubwa imekuwa ni zinauma wakati wa Kuchana.

Nipeni ushauri kwa wanaume wenzangu ambao mmeweza kufuga nywele ndefu,mnawezaje kwenda nazo sawa?

afro-hairstyles-for-black-men-60902.jpg
 
Mimi ni hizi shughuli tu ila huwa nina mpango wa kufuga kwa mtindo wa kiDrogba.

Nywele zinataka usafi wa hali ya juu zikishakuwa refu kuanzia kujikausha na mafuta unaayotumia. (Kipilipili sio kizuri kwa kufuga).

Kama wewe ni mwanamme wa Dar naelewa nia yako. Drogba anachoma nywele ili ziwe laini na kufanya kuwa ndefu ili azifunge kama wazungu. Watu wa Ivory Coast na nchi nyingi za Afrika Magharibi wana haya matatizo ya kujifananisha na wazungu na ndiyo maana wanajichubua sana. I hope hujafikia kuwa na haya matatizo ya kiakili.
 
Nafikiri zangu zikiwa nyingi zinafungika kwa zilivyo zikikataa ni poa pia.
 
Mimi ni hizi shughuli tu ila huwa nina mpango wa kufuga kwa mtindo wa kiDrogba.

Nywele zinataka usafi wa hali ya juu zikishakuwa refu kuanzia kujikausha na mafuta unaayotumia. (Kipilipili sio kizuri kwa kufuga).
Nimegundua ni rahisi kuchana zikiwa bado mbichi, shida ni huwezi kupaka mafuta nywele mbichi
 
Kwa mwanaume kufuga nywele ni uchafu kwani hatuna muda mwingi wa kuzifanya ziwe na muonekano wenye ushawishi Kwa wengine nyoa tu
 
Mimi ni hizi shughuli tu ila huwa nina mpango wa kufuga kwa mtindo wa kiDrogba.

Nywele zinataka usafi wa hali ya juu zikishakuwa refu kuanzia kujikausha na mafuta unaayotumia. (Kipilipili sio kizuri kwa kufuga).
Utaolewa wewe Masai wa kigoma
 
Na mkorogo unatumia pia?
Mkuu haya mambo yapo subjective...

najua unakonipeleka saana.

Ila Mfano nikikuambia natumia mkorogo au la hayakuhusu,hayatakuongezea chochote, mwenyewe hayataniongezea chochote pia.

Nikifuga nywele au nisifuge kwako mtakula au kama hamli hamtakula. its simple like that.
 
Mkuu unatoa nywele unabakia na kipara.? Au unakua na unga unga.? Binafsi nilishashindwa hata kupunguza. Nywele raha bhana. Zangu hazina matunzo hata mafuta yoyote ila zina muonekano mzuri. Hii inategemea na nywele zako.
 
Katika maisha yangu sijawahi kunyoa dongo(kipara). Nataka nibakize kidogo za kitana tu
 
Tengeneza dread kama utapenda,japo hizi zinaonekanaga kama uhuni hiv hasa makazini,ukishindwa nyoa tu hamna namna
Asante mkuu, bahati nzuri sehem niliyopo hamna hizi judgment za namna hii, unaweza kufanya yote ili mradi haimbugudhi mwingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom