Kuna baadhi ya mambo yakikupata ni dhahiri hata ukiwa huna hekima ya maamzi lazima utaipata. Lakini pia yapo matukio ya ki-ndoa yako dhahiri, yakikupata na kuomba ushauri baadhi ya watu watakushangaa, yamkini hata unapoanza kuomba ushauri hata wewe unaona aibu. Huu ni muda wa kuamua kusamehe au kuachana na ke wako.
Matukio ya namna hii huwa hayafutiki kichwani, hata kama utasamehe...bado hutajenga imani asilani, hutakaa ufurahie maisha ya upendo wa dhati kwa kiasi cha kutosha. utatilia wasiwasi safari zake, ukisafiri utakwenda ukae na wasiwasi kama hatafanya tena nk nk
Naamini unalo jambo la kufanya...
Nikupe ushauri mmoja tu ambao ukimudu kufanya utampa adhabu kubwa na ataishi maisha ya kujitafakari sana pengine ni adhabu mbaya sana kwake kama ni mtu mwenye akili na nia ya dhati ya kuishi na wewe, kama hana nia utajua...
UKIAMUA KUSAMEHE FANYA HIVI...
1. Kama huja muuliza nini kilichotokea huko hata akapigwa basi usimuulize, tulia kimya
2. Akikusimulia nini kilitokea msikilize hadi mwisho, usimjibu chochote, harafu nyanyuka ukatembee, ukirudi onyesha furaha tu. Fanya hivi ukijua moyoni umeshamsamehe ila usimtamkie
3. Ishi nae kwa furaha, hata ndugu na marafiki wakikuuliza juu ya tukio, waambie bado unatafakari
4. Usigombane nae kwa masuala mengine tofauti na hilo harafu tukio hilo nalo ukali-top up kama justification ya wewe ni huna makosa then yeye ana makosa mengi mojawapo ni tukio hilo baya ( usifanye kosa hilo)
5. Kama unamfahamu mwanamme aliyekamatwa naye, usimuulize lolote, hata kama akikufuata kujisafisha mzuie, then usimtukane...just be calm
Kama haya utayafanya bila kukosea, haya yatatokea
1. Mke ataamua kuvunja mji au kwa kutoroka au atatafuta sababu itakayompa uhalali wa kuvunja ndoa
2. Asipovunja ndoa, hatarudia tena kufanya hiyo tabia
3. Atakuheshimu tena kwa kukuogopa
4. Atawaza mambo mengi sana, juu ya nini hasa maamzi yako, nini hasa unachopanga kumfanyia yeye au mwanamme aliyekamatwa naye(Hapa ataishi bila amani, ataishi kwa kukuogopa, lakini atakuheshimu na hatorudia makosa)
5. Ataanza kukulazimisha mwende pamoja iwapo atakuwa na vijisafari vya kutoka kama ishara ya kuacha tabia hiyo au kukujenga imani
Saikolojia ya mwanamke hupenda kuona reaction ya mme wake anapokuwa na uhakika kuwa amekosa, amefanya jambo baya nk. Wapo wanawake wengine hutarajia kufokewa au kupigwa anapokosea na hayo akiyaona yamefanywa na mme wake hujiridhisha kwamba kesi imeisha.
Kwa ushauri niliokupa, hakuna reaction yoyote itakayomfanya aridhike kuwa kesi imeisha. Anategemea aone
umemfoka, umempiga, umemfukuza nk, lakini haya ukiyafanya (yaani hapo pekundu) na akaridhika kwamba kesi imeisha tabia yake atairudia kwa staili ambayo hutakuja ugundue kuwa anachepuka
Kama umeshamfokea, ushauri huu ni non applicable tena. Huu ni ushauri wa kumsamehe, usivunje ndoa yako maana yawezekana tabia yake analipa kisasi kwako kwa kuchepuka, you never know....
Mimi kwa jina naitwa John ni mwanaume mwenye umri wa miaka 35. Ninaishi na mke wangu wa ndoa ,na tumejaliwa tumepata watoto wawili,
Siku ya Christmas baada ya chakula cha mchana aliniaga akaniambia anaenda hospital kumuona rafiki yake amelazwa nikamruhusu nikamwambia aende lakini awahi kurudi.
baada ya kupita lisaa moja alirudishwa akiwa hoi na watu wakimzomea nilipotaka kujua amepatwa na nini.!!!nikaambiwa kafumaniwa na mume wa mtu !!!na waliomchakaza hivyo ni wanawake wenzake.
niliishiwa nguvu nikaamua nimpeleke hospital kusema ukweli nimekaa nimeshindwa kupata ufumbuzi naombeni ushauli wenu huyu mwanamke niendelee kuishi nae au nimpe talaka?