MREJESHO
Baada ya kuweka kesi yangu hapa nilipata mawazo mengi yanayojenga na hatimaye niliongezeka ujasiri. Ingawa mkosaji ni mimi lakini sikuona maana yeyote ya kutekeleza matakwa ya wifey as collateral ya umaluuni wangu.
Namshukuru sana Mwana JF mmoja aliyenijenga kifikra, dada huyu sitamsahau maishani kwani aliamua kubeba jukumu yeye mwenyewe na akawa ananishauri bila kuchoka na hata nilishare naye vitu vingi vya msingi ambavyo hata yeye alishangaa kuwepo na hayo mambo. Unajua mostly inaonekana WANAUME tuna makosa sana kutoka nje ila kuna slightly errors ambazo wake zetu wanafanya ambazo zinakupeleka moja kwa moja nje ya mipaka ya viapo vya ndoa.
Hivi sasa ninavyoongea mke wangu amepoa na ameacha vitisho vyake na hakuna tena kuvurugana ingawa hali inatulia kwa muda na kulipuka tena lakini kadiri siku zinavyokwenda ndivyo anazidi kuwa mpole. Ameelewa hatari ya kufanya kosa kama ngazi ya kurekebisha kosa la awali.
Nawashukuru sana JF mmenisaidia kisaikolojia na kuokoa ndoa yangu isisambaratike...