Yamenikuta: Mchepuko umetibua ndoa

Yamenikuta: Mchepuko umetibua ndoa

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,665
Nilikuwa nakatiza maeneo ya Chang'ombe nikamwona mrembo anatembea juani alionekana amechoka, nikampa lifti kumsogeza mjini baada ya kumuuliza aendako,tulibadilishana anuani na tukawa tunawasiliana.

Binti mwenyewe ni mrembo na ameumbika kike haswaa. Sasa siku tuliyoonana tena nikajiona sana kumuachia hivyo nikaimba beti chache na hatimaye nikatusua mtoto. ikumbukwe hapo nimeoa.

Baada ya mchezo ule nilijuta kiasi ila nikanogewa tukawa tunabanjua amri ya sita kila mara bila kutambulika. Lakini hakuna marefu yasiyo na ncha, hatimaye nikagundulika na wife kwamba nakimbia mwenge nje ya chumba.

Moto uliowashwa daah sitausahau. Nahisi binti alikuwa ameniwekea kitu nijione nafanya jambo sahihi na baada ya kugundulika na wife ndo nikagundua upuuzi nilioufanya na almanusura ndoa ivunjike.

Ila nimemsihi sana wife anisamehe na sitarudia tena. Mke tunaendelea kuishi wote ila bado haniamini kwa hayo yaliyotokea.

Kiufupi ni kwamba nilitopea baada ya kuona nyumbani nakumbana na full stress na nakosa faraja, amani na upendo hivyo nikajiona nipo right kabisa kufanya dhambi ambayo leo naijutia.

Sharti alilonipa ni kwamba yeye ameandaa vijana wake hivyo nimlete yule binti ili abakwe mbele yake na kadhalika. Kitu hiko nimemwambia ni kinyume na utu na ni kuvunja sheria, ugomvi umeanza upyaaa.

Anasema kuwa namkwepesha huyo binti kwa kuwa nampenda. Naomba ushauri nifanyeje hapo maana ingawa najutia kosa langu lakini sipendi kutenda kosa la unyama kiasi hiki.

MREJESHO
Baada ya kuweka kesi yangu hapa nilipata mawazo mengi yanayojenga na hatimaye niliongezeka ujasiri. Ingawa mkosaji ni mimi lakini sikuona maana yeyote ya kutekeleza matakwa ya wifey as collateral ya umaluuni wangu.

Namshukuru sana Mwana JF mmoja aliyenijenga kifikra, dada huyu sitamsahau maishani kwani aliamua kubeba jukumu yeye mwenyewe na akawa ananishauri bila kuchoka na hata nilishare naye vitu vingi vya msingi ambavyo hata yeye alishangaa kuwepo na hayo mambo. Unajua mostly inaonekana WANAUME tuna makosa sana kutoka nje ila kuna slightly errors ambazo wake zetu wanafanya ambazo zinakupeleka moja kwa moja nje ya mipaka ya viapo vya ndoa.

Hivi sasa ninavyoongea mke wangu amepoa na ameacha vitisho vyake na hakuna tena kuvurugana ingawa hali inatulia kwa muda na kulipuka tena lakini kadiri siku zinavyokwenda ndivyo anazidi kuwa mpole. Ameelewa hatari ya kufanya kosa kama ngazi ya kurekebisha kosa la awali.

Nawashukuru sana JF mmenisaidia kisaikolojia na kuokoa ndoa yangu isisambaratike...


 
Tena fanya haraka mpeleke huyo bint kabla ya yote aliwe mbele yako na hasira yake iishe okoa ndoa mchepuko hauna maana ss fanya haraka
 
nabii mweusi

Binti akienda kushtaki polisi itakuwaje? Hapo ndo hofu yangu ilipo
 
Last edited by a moderator:
Leo ahsubuhi ninampeleka kazini. anatoa machozi nikimuuliza hataki kusema, baadaye amenipigia anasema kuwa ninamkwepesha yule binti hivyo bado ana uhakika naendelea naye.

Kiufupi ni kwamba anayo namba yake na wameshawasiliana sana na ameshapafahamu kwao. Najiuliza kwa nini anihusishe mimi ktk mpango wa kijinai?
 
Huo sio ubinadamu, kwani alikulazimisha kuwa nae? Halafu sisi wanawake huwa hatujiongezi tu, badala ya kudeal na tatizo ulilonalo ndani unakwenda kuparamia aliyetobgozwa.

Wewe mume ungekuwa na msimamo huyo dada angekulazimisha? Mkeo a napaswa akae nawewe akueleze madhara ya kutoka nje ya ndoa na akuulize sababu ya wewe kuamua hivyo.

Maana kama ni tabia yako utampeleka huyo binti wa watu atabakwa then utatafuta mwingine mwisho wa siku mtabakisha wangapi? Mwogopeni Mungu hiyo sio suluhu. Mnatakiwa muelezane kilichopungua badala ya kuadhibu wapita njia.
 
Nakushauri usifanye hivyo kwani huyu bnt hakukutongonga ni ww mwenyewe na matamanio yako cha msingi mwelee mkeo kuwa ulifanya vile kwa sababu hizo ambazo umetueleza so hakunahaja ya kumuhukumu binti wa watu wakat yeyekatongozwa kama ulivyomtongoza yeye hata kama kakukuta na kosa kuwa mkali sio akuendeshe na kwa ninavyokuona unaendeshwa kama gar bovu.
 
Nominomi

Nimejaribu kumsihi sana mke wangu kwamba pamoja na yote mimi ndiye mkosaji lakini yeye anashikilia msimamo kwamba kwa nini binti yule akubali kulala na mimi huku akijua kuwa nimeoa?

Nimejaribu kumwomba tukaombewe kanisani hasa mimi ili nisirejee upuuzi ule anasema huko hakuna jipya na msimamo wake ni ule ule. Ila ukweli nimemuudhi pamoja na kwamba ana hasira lakini utu wema ni silaha dhidi ya dhambi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom