Yameishia wapi mayai ya kware na ufugaji wa kware?

Yameishia wapi mayai ya kware na ufugaji wa kware?

Kulikuwa na wimbi kubwa la matangazo na mauzo ya mayai ya ndege mdogo aina ya kware. Mayai yake yalisifiwa sana na kushawishi watu wengi kuyatumia. Wapo hata walioanza na kuimarika katika ufugaji wa kware.

Mayai ya kware na ufugaji wa kware kwa ujumla vimeishia wapi?
Yalipata kiki kama kikombe cha Babu wa loliondo
 
Tatizo lililopo ni kuwa mamruki wa vitu. Huwa tukisikia kama dili fulani linalipa basi wote tunataka kufanya hilo dili bila kujua kwamba wengine inabidi tubaki wahitaji wa hizo bidhaa. Inafika sehem kila mtu ana mayai ya kwale, unamuuzia nani sasa??

= mamluki
 
Kulikuwa na wimbi kubwa la matangazo na mauzo ya mayai ya ndege mdogo aina ya kware. Mayai yake yalisifiwa sana na kushawishi watu wengi kuyatumia. Wapo hata walioanza na kuimarika katika ufugaji wa kware.

Mayai ya kware na ufugaji wa kware kwa ujumla vimeishia wapi?
kware anapigwa menu kali ya kuku broila. Halafu eti tiba! kweli kuna watu hamnazo!
 
Mkuu jiulize hii habari ilianzia wapi?
Ilianzia namaingo business agency.
Sasa waliamia kwenye sungura na kilimo cha madodoki....
Namaingo Mungu anawaona yani watanzania wanadanganywa daily
Projects za hawa jamaa ni pasua kichwa.
 
Kama alivyoishia Babu wa Loliondo.

Tanzania tunasumbuliwa na tatizo kubwa la "uelewa mpana wa mambo ya kawaida". Kwa hiyo watu wenye nia ya kujitajirisha hutumia "ujinga" wa walio wengi kujineemesha. Wanatengeneza matatizo ya kiafya akilini mwa watu, na kisha huja na "solutions" kwa ajili ya matatizo hayo baada ya kuona wananchi wametishwa na hayo "matatizo yao".

Ushauri wangu ni kuwa sisi tulio wazazi wa kizazi kipya, tuwasisitize watoto wetu kujifunza na kuitafuta elimu pana ya maisha yao. Tusiwakomalie tu kujifunza mkondo wao wa elimu husika maana watajikutwa wanadanganywa na watu wa upande ule mwingine. Tusisitize holistic education ili kuwakinga na wanyonyaji wa kizazi kipya kama wauza mayai ya kware, kikombe cha babu na bibi na shangazi, na wauza dawa ambapo dawa moja inaweza kutibu hata magonjwa 150 yakiwemo ya kuambukiza, yasiyoambukiza, ya virusi, bakteria, protozoa, mzio, auto-immune, n.k. Yaani magonjwa yasiyohusiana kwa namna yanavyojengeka, namna yanavyodhihirika na kuathiri mwili wala namna yanavyotibika yote unaambiwa yanatibiwa na dawa moja tu.

Tukiokoe kizazi kijacho ndipo hata taifa litapata maendeleo.
Post bora kabisa

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
1.KIKOMBE CHA BABU,
2.DECI,
3.MAYAI YA KWARE,
4.BAADHI YA TIBA ZA ASILI NA MIMEA,
5.BAADHI YA IMANI ZILIZO NA UTATA,
6.RUPIA ZA MJERUMANI
Pamoja na Abracadabra zingine zote kwa kweli ni vitu vinavyozuka kwa mbwembwe nyingi na kwa bahati mbaya wale wanaovianzisha hutumia technics za hali ya juu kwa kugusa yale maeneo sensitive yanawagusa watu wengi kama vile masuala ya kiafya, kiuchumi na kiimani. Usipokuwa makini utaingia mkenge, haijalishi elimu yako, cheo wala nafasi yako uliyo nayo katika jamii.

Huwa vinachukua muda fulani tu na mara nyingi siyo mrefu sana and then watu wakishagutuka basi vinafifia na kuwa historia. Bora sungura nimeona pamoja na kwamba kuna kaharufuharufu ka mizengwe mithili ya hiyo hapo juu kwa baadhi ya wadau lakini kwa kiasi kikubwa miradi ya ufugaji wa sungura ina uhalisia, hata wapo watu wengi wanaofuga na faida huiona ila siyo kwa kiwango kinachotiwa chumvi na baadhi ya wadau.

Tujifunze siyo kila kitu ni cha kukurupukia, akili ya mwenzio changanya kwanza na yakwako.
 
umenikumbusha lina kwenye interview ya powerjams ya sam enzi izo
 
Kama alivyoishia Babu wa Loliondo.

Tanzania tunasumbuliwa na tatizo kubwa la "uelewa mpana wa mambo ya kawaida". Kwa hiyo watu wenye nia ya kujitajirisha hutumia "ujinga" wa walio wengi kujineemesha. Wanatengeneza matatizo ya kiafya akilini mwa watu, na kisha huja na "solutions" kwa ajili ya matatizo hayo baada ya kuona wananchi wametishwa na hayo "matatizo yao".

Ushauri wangu ni kuwa sisi tulio wazazi wa kizazi kipya, tuwasisitize watoto wetu kujifunza na kuitafuta elimu pana ya maisha yao. Tusiwakomalie tu kujifunza mkondo wao wa elimu husika maana watajikutwa wanadanganywa na watu wa upande ule mwingine. Tusisitize holistic education ili kuwakinga na wanyonyaji wa kizazi kipya kama wauza mayai ya kware, kikombe cha babu na bibi na shangazi, na wauza dawa ambapo dawa moja inaweza kutibu hata magonjwa 150 yakiwemo ya kuambukiza, yasiyoambukiza, ya virusi, bakteria, protozoa, mzio, auto-immune, n.k. Yaani magonjwa yasiyohusiana kwa namna yanavyojengeka, namna yanavyodhihirika na kuathiri mwili wala namna yanavyotibika yote unaambiwa yanatibiwa na dawa moja tu.

Tukiokoe kizazi kijacho ndipo hata taifa litapata maendeleo.

Tunaendeshwa na masalia ya tamaduni zetu.... Kila tunachofanya kimekaa kiganga ganga....!! Can you imagine hadi maprofeseri, phd holders, ministers, prezdars walikwenda kwa babu..
 
Wameamia kwenye VUMBI LA MKONGO.

"PAMBANA NA HALI YAKO"
 
Back
Top Bottom