Yameishia wapi mayai ya kware na ufugaji wa kware?

Yameishia wapi mayai ya kware na ufugaji wa kware?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,143
Kulikuwa na wimbi kubwa la matangazo na mauzo ya mayai ya ndege mdogo aina ya kware. Mayai yake yalisifiwa sana na kushawishi watu wengi kuyatumia. Wapo hata walioanza na kuimarika katika ufugaji wa kware.

Mayai ya kware na ufugaji wa kware kwa ujumla vimeishia wapi?
 
Kulikuwa na wimbi kubwa la matangazo na mauzo wa mayai ya ndege mdogo aina ya kware. Mayai yake yalisifiiwa sana na kushawishi watu wengi kuyatumia. Wapo hata walioanza na kuimarika katika ufugaji wa kware.

Mayai ya kware na ufugaji wa kware kwa ujumla vimeishia wapi?
Mkuu jiulize hii habari ilianzia wapi?
Ilianzia namaingo business agency.
Sasa waliamia kwenye sungura na kilimo cha madodoki....
Namaingo Mungu anawaona yani watanzania wanadanganywa daily
 
Kulikuwa na wimbi kubwa la matangazo na mauzo ya mayai ya ndege mdogo aina ya kware. Mayai yake yalisifiiwa sana na kushawishi watu wengi kuyatumia. Wapo hata walioanza na kuimarika katika ufugaji wa kware.

Mayai ya kware na ufugaji wa kware kwa ujumla vimeishia wapi?
Kama alivyoishia Babu wa Loliondo.

Tanzania tunasumbuliwa na tatizo kubwa la "uelewa mpana wa mambo ya kawaida". Kwa hiyo watu wenye nia ya kujitajirisha hutumia "ujinga" wa walio wengi kujineemesha. Wanatengeneza matatizo ya kiafya akilini mwa watu, na kisha huja na "solutions" kwa ajili ya matatizo hayo baada ya kuona wananchi wametishwa na hayo "matatizo yao".

Ushauri wangu ni kuwa sisi tulio wazazi wa kizazi kipya, tuwasisitize watoto wetu kujifunza na kuitafuta elimu pana ya maisha yao. Tusiwakomalie tu kujifunza mkondo wao wa elimu husika maana watajikutwa wanadanganywa na watu wa upande ule mwingine.

Tusisitize holistic education ili kuwakinga na wanyonyaji wa kizazi kipya kama wauza mayai ya kware, kikombe cha babu na bibi na shangazi, na wauza dawa ambapo dawa moja inaweza kutibu hata magonjwa 150 yakiwemo ya kuambukiza, yasiyoambukiza, ya virusi, bakteria, protozoa, mzio, auto-immune, n.k. Yaani magonjwa yasiyohusiana kwa namna yanavyojengeka, namna yanavyodhihirika na kuathiri mwili wala namna yanavyotibika yote unaambiwa yanatibiwa na dawa moja tu.

Tukiokoe kizazi kijacho ndipo hata taifa litapata maendeleo.
 
Tena nakumbuka radio wapo ndio walioshupalia Sana Haya mayai ya kweli. Haya Dec ni hiihii radio na Kanisa lao. Daima wamekua watu wa kutafuta hela kwa udanganyifu Sana.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
hivi hao sungura wanaliwa waoi asee mbona mi siwaskii kbs kwenye,,nshawahi kuwakuta belcanto tuu
 
Kulikuwa na wimbi kubwa la matangazo na mauzo ya mayai ya ndege mdogo aina ya kware. Mayai yake yalisifiwa sana na kushawishi watu wengi kuyatumia. Wapo hata walioanza na kuimarika katika ufugaji wa kware.

Mayai ya kware na ufugaji wa kware kwa ujumla vimeishia wapi?
tunaenda na wakati sasa ivi tuna trend na forex trade na D9 kware tumeshapiga chini
 
Mkuu jiulize hii habari ilianzia wapi?
Ilianzia namaingo business agency.
Sasa waliamia kwenye sungura na kilimo cha madodoki....
Namaingo Mungu anawaona yani watanzania wanadanganywa daily
Vipi kikombe cha babu?

Sent from my Lenovo A2010-a using JamiiForums mobile app
 
Daah yani babu aliwapiga watu na ma phd yao kudadeki babu inabidi apewe degree ya heshima.
Na waliokimbilia kwa babu kunywa kikombe waulizwe walikua wanaumwa nini?

Sent from my Lenovo A2010-a using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom