Yaliyosemwa na mgombea ubunge CCM jimbo la Kinondoni Said Mtulia leo tar 3

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
871
1,000
*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI KWA TIKETI YA CCM, NDUGU MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KATA YA KIJITONYAMA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 3, 2018*

"Mtulia mie nilienda kuvunja kibubu changu nikaenda Mahakamani kuzuia bomoabomoa, Serikali ikanisikia na Watu hawakubomolewa" - Mtulia

"Nimeacha Ubunge ili nijiunge na chama cha ushindi, chama chenye dola, chama kinacholeta maendeleo" - Mtulia

"Chama nilichotoka wakisema nimewasaliti wapo sahihi maana tulikuwa 10 sasa wamebaki 9. Wewe Mwananchi nimekusaliti nini?" - Mtulia

"Sisi Wabunge ni kama Washenga ukitukana Wakwe utampata Mke? Wabunge wa upinzani wanaitukana Serikali, maendeleo watayapata wapi?" - Mtulia

"Hii ni ilani ya CCM ndio inayoendesha nchi. Kazi yangu mkinichagua ni kwenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi" - Mtulia

"Nikishinda mje ofisini kwangu Vijana na Wanawake mjiandikishe mkachukue mikopo yenu toka Manispaa" - Mtulia

"Kuna Mtu amekuja kugombea lakini hana familia wala kadi ya kupigia kura, mtampaje dhamana huyu Mtu?" - Mtulia

"Mtu ameshindwa kwa wapiga kura 3600, atawezaje kushinda kwa Watu zaidi ya laki 2" - Mtulia

"Kama wameshindwa kujenga chama jimbo la Kinondoni ukienda kukodi jeshi usitegemee utashinda. Mbunge wa Kinondoni ni Maulid Said Mtulia" - Mtulia

"Mkinichagua nitashirikiana na Serikali ya CCM kuhakikisha kila kata naleta magari mapya ya kuzolea uchafu" - Mtulia

"Kijitonyama mna matatizo ya kubambikiziwa bili za maji, mkinichagua hilo tatizo litakuwa historia" - Mtulia

"Mtanzania yeyote anayekufa kwenye hospitali ya Serikali, Marehemu asidaiwe pesa endapo uwezo wake ni duni" - Mtulia

"Utakitupaje mkono chama kinacholeta maendeleo, kinacho miliki dola?" - Mtulia

"Watu wa Kinondoni mnaona barabara za mwendo kasi, mnaona madaraja, mnaona hospitali nzuri. Yote ni matunda ya kazi za Chama Cha Mapinduzi" - Mtulia

"Nawaombeni sana mnichague Said Maulid Mtulia niwe daraja la kuwaletea maendeleo" - Mtulia

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,034
2,000
Nawaona wanakinondoni ndani ya Chanikiwiti....CCM MBELE KWA MBELE
 
  • Thanks
Reactions: UCD

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,034
2,000
Uchaguzi wa Kinondoni na Siha utakuwa kipimo cha IQ ya Wananchi wa maeneo hayo. Siamini yupo anayeweza kumchagua mtu aliyekataa kazi leo na baada ya muda mfupi akaomba tena kazi ile ile. Muda utaamua
Alikataa utumwa ndani ya UKAWA...!
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,756
2,000
Hicho ni kikao cha wana ccm wa kinondoni(angalia jezi) I hope wakitoka hapo wataenda kufanya kampeni!
Tangu Jeshi la Polisi waanze kwenda na vifaa vya kurekodia wazungumzaji kwenye Mikutano ya Chadema Matusi yameadimika kwenye Mikutano
Hongera Jeshi la Polisi kwa ubunifu
 
bs group

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
821
500
hapa utavuna ulichopanda mkuu, kinondoni inawatu wenye elimu zao...au labda ni mchezo wa comedi unaigza.. ungekuwa kijijin uko ungeeleweka..lakn kinondon hii umeliwa mjomba..
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,158
2,000
Uchaguzi wa Kinondoni na Siha utakuwa kipimo cha IQ ya Wananchi wa maeneo hayo. Siamini yupo anayeweza kumchagua mtu aliyekataa kazi leo na baada ya muda mfupi akaomba tena kazi ile ile. Muda utaamua
Hiki ulichoandika ndicho nami nachoamini pia,
Ukitaka kujua Wananchi wa Majimbo haya wana akili kias gani basi subiri matokeo baada ya hizi chaguzi
 
Lipijema

JF-Expert Member
Mar 8, 2015
572
1,000
Uchaguzi wa Kinondoni na Siha utakuwa kipimo cha IQ ya Wananchi wa maeneo hayo. Siamini yupo anayeweza kumchagua mtu aliyekataa kazi leo na baada ya muda mfupi akaomba tena kazi ile ile. Muda utaamua
 
Lipijema

JF-Expert Member
Mar 8, 2015
572
1,000
Uchaguzi wa Kinondoni na Siha utakuwa kipimo cha IQ ya Wananchi wa maeneo hayo. Siamini yupo anayeweza kumchagua mtu aliyekataa kazi leo na baada ya muda mfupi akaomba tena kazi ile ile. Muda utaamua
Ukweli ni kwamba jamii ya sasa siyo ile ya mwaka 1947 Wananchi wa kinondoni msifanye kosa, Salum mwl: anakubalika kwa saaana!
 
tofali

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
4,016
2,000
Uchaguzi wa Kinondoni na Siha utakuwa kipimo cha IQ ya Wananchi wa maeneo hayo. Siamini yupo anayeweza kumchagua mtu aliyekataa kazi leo na baada ya muda mfupi akaomba tena kazi ile ile. Muda utaamua
Haswaaaaa...tutajua wana kinondoni uwezo wao wa kufikiri...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom