Yaliyonikuta Tabora

Yaliyonikuta Tabora

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,662
Wakuu natumaini hamjambo,

Leo napenda niwaeleze jinsi baadhi ya mikoa yetu ilivyo nyuma kimaendelo na tulikuwa hatujui sababu ya mikoa hiyo kuwa nyuma kimaendeleo. Lakini kwa safari yangu ya Tabora mjini nimegundua ni kutokana na upeo mdogo wa wananchi wa mikoa hiyo iliyo nyuma kimaendelo.

Ni kwamba nilikuwa likizo ya mwaka haki ambayo kila mtumishi anapaswa kupewa. Nilipomaliza likizo yangu usiku wa kuamkia tarehe 15 Mwezi huu nililala kwenye hoteli moja mjini Tabora karibu na stendi kwa ajili ya kujidamkia mabasi yanayokuja Dar Es Salaam ambayo saa ya kuripoti ni saa kumi na moja na nusu alfajiri. Nilifuata taratibu zote za kihoteli na ilipofika saa kumi na moja na robo alfajiri nilikuwa tayari (mimi na mke wangu) kwa safari.

Kufika mapokezi hatukukuta muhudumu yeyote. Nilijaribu kuita kwa sauti kumwita mhudumu atufungulie mlango tuondoke lakini hakuna dalili ya kuitikiwa. Bahati nzuri kuna mteja mwingine naye alikuwa akisafiri alfajiri hiyo naye akaja tukaungana kumtafuta muhudumu bila mafanikio.

Ndipo kwa kutumia maarifa mengine nikajaribu kumwita mlinzi wa nje huko getini aje atusaidie kutufungulia ama kumtafuta muhudumu atufungulie. Lakini tulishindwa kwa sababu getini ni mbali sauti zetu hazikumfikia mlinzi. Ndipo nikapata wazo la kumpigia simu jamaa yangu mmoja aliyepo Tabora mjini aje amgongee mlinzi kisha amfahamishe kuna watu ndani wanahitaji kutoka hotelini lakini hawamwoni muhudumu.

Wazo langu lilifanikiwa maana jamaa akaja akamgongea mlinzi wa hoteli na kumfahamisha ya kuwa muhudumu haonekani na kuna watu wanahitaji kutoka hotelini. Ndipo mlinzi alipomtafuta muhudumu akampata (sijui alimpata wapi hilo sijui). Muhudumu akaja kutufungulia lakini akiwa katika hali ya ulevi.

Baada ya kutufungulia (yule mteja mwingine amekasirika kupita maelezo) ndipo nikamwambia muhudumu nikiwa nimesimama mlangoni kuwa wasilalamike kutopata wateja maana moja ya sababu yawezekana ikawa ni hii aliyotufanyia leo.

Muhudumu akanijibu ".......hata usipokuja tena kwani mteja ni wewe peke yako? Nipishe nifunge mlango......." Huku akinisukumiza na mlango nitoke mlango ukabamiza mabegi niliyokuwa nimeshika mkononi na matairi ya mabegi yakavunja vioo vya mlango huo.

Kilichofuatia akaamuru mlinzi afunge geti tusitoke mpaka hapo polisi watakapokuja. Nikafungiwa ndani ya geti la hoteli kuanzia saa 11 dk 29 alfajiri mpaka polisi walipokuja saa 1 dk 40 asubuhi. Wakaja wakanikamata kwa tuhuma ya kuingia hotelini kwa nia ya kuharibu mali!

Kwa hiyo basi likaniacha na safari ikawa imekufa!

Nikawekwa mahabusu mpaka saa 5 na nusu asubuhi yule jamaa yangu alipotafuta watu wa kuja kunitolea dhamana. Kesi ikaamuliwa nilipe mlango wa hoteli shilingi LAKI SABA ili nisipelekwea mahakamani. Nikawaomba badala ya kulipa pesa mimi nitafute fundi aje atathmini gharama kisha atengeneze nimlipe.

Suala ni kutengeneza mlango....Nilipata upinzani mkali sana polisi kwamba nawafundisha kazi. Nikawaambia sheria za nchi yetu siyo nzuri,mlalamikaji anaaminiwa sana kuliko mshitakiwa.

Wao walikuwa na uthibitisho gani kuwa mimi niliingia hotelini kwa nia ya kuharibu mali? Aliyevunja ni muhudumu siyo mimi!!

Hatimaye ikakubalika nitafute fundi. Nikampata fundi gharama ya kioo ikawa ni shilingi elfu ishirini na ufundi ni shilingi elfu kumi tu. Mlango ukawa umekamilika kutengenezwa saa 7 dk 36 mchana.

Hayo ndiyo yaliyonikuta Tabora. Mlango wenyewe ni huu nilio u atach na muhudumu mwenyewe ni huyo dogo mwenye shati jekundu. Ameniboa sana........!!!!!

MLANGO.jpg
 
Miafrika banah sijui ikoje!..huo ni umaskini au we ni le mbebez mwalimu.

Tatizo mnalala gest za maskini. Nenda lodge ya maana afu lala presidential suite uone kama utapata hayo majangazi!!
 
miafrika banah sijui ikoje!..huo ni umaskini au we ni le mbebez mwalimu!...tatizo mnalala gest za maskini. Nenda lodge ya maana afu lala presidential suite uone kama utapata hayo majangaz!!

Hapana mkuu......ni katika hali ya kuwa karibu na eneo la stendi.......Kwa taarifa tu kwa tabora hata hoteli iwe kubwa kiasi gani uelewa wa watu wa Tabora unafanana.
 
Sasa mkuu kwan hayo ndo yanayosababisha tabora isiendelee?

Ndiyo mkuu mojawapo ya sababu za backwardation ni hiyo. Mhudumu anakuwa ahjui wajibu wake na pia hana customer care unafikiri pana maendeleo hapo?
 
Duh pole sana kwa yaliyokukuta ila ingekuwa mimi nilivyombishi ningewaambia police wanipeleke mahakamani
Sasa la pili nyie mlikuwa mtu nne yaani wewe,mkeo,mteja mwezio na jamaa yako wa tabaro mlishidwa vipi kusimama kidete kupigania haki yenu?
Mlishidwa vipi kumtia dogo adabu hata makofi??

Kuna siku niliingia kwenye hiace abiria mwanamke akafungukua kioo cha hiace kumbe kilikuwa kama kimetegeshswa kikamwagika chini kodda na dreva wakakomaa huyo dada alipe abiria wote tuliungana kumtetea na hakukipa kitu na tukamwabia huyo dada ashuke kituo kilichofuata achukue hiace nyingine na kesi ikaishia hapo
 
Hiyo hotel inaitwaje?

Kwanza naomba mnipe madhara ya kuitaja ama kutoitaja isije mada hii ikafutwa. kama mkinihakikishia kuitaja nitakuwa sijafanya makosa sasa hivi naianika hadharani.
 
Duh pole sana kwa yaliyokukuta ila ingekuwa mimi nilivyombishi ningewaambia police wanipeleke mahakamani
Sasa la pili nyie mlikuwa mtu nne yaani wewe,mkeo,mteja mwezio na jamaa yako wa tabaro mlishidwa vipi kusimama kidete kupigania haki yenu?
Mlishidwa vipi kumtia dogo adabu hata makofi??

Kuna siku niliingia kwenye hiace abiria mwanamke akafungukua kioo cha hiace kumbe kilikuwa kama kimetegeshswa kikamwagika chini kodda na dreva wakakomaa huyo dada alipe abiria wote tuliungana kumtetea na hakukipa kitu na tukamwabia huyo dada ashuke kituo kilichofuata achukue hiace nyingine na kesi ikaishia hapo

Yule jamaa mteja mwingine alitangulia kutoka sasa mimi nilipobaki kumweleza aliyotufanyia ndipo yakatokea hayo. Tukabaki wawtatu mimi, mke wangu na jamaa aliyekuja kumgongea mlinzi. Tulishindwa kutok maana geti lilifungwa na jamaa yangu aliyekuja aliingiza gari ndani Tusingeweza kutoka........
Na Tabora unavyopajua saa 11 alfajiri uanzishe varangati si utaambiwa jambazi!!! Polisi walivyokuja kwa suala la kioo tu walitoa pingu wanifunge sembuse ufanye fujo? Mkuu Tabora mimi ni kwetu napajua sana. Uelewa ni ziro! Hata ukiwa mwalimu ukapangiwa Tabora ukiacha tabora boys, Milambo na Tabora girls Tabora ni matatizo....!!!!!!!
 
Sehemu yoyote walopita waarabu sijajua ni kwa nini,nilienda kufacilitate semina Mtwara wahudumu wa hotel hawajali wateja similar kesi Lindi napo ni hivo hivo lakini nilienda Mwanza,Mbeya,Kilimanjaro huduma safi sijui waliwapa dawa gani hawa waarabu.
 
Ndiyo mkuu mojawapo ya sababu za backwardation ni hiyo. Mhudumu anakuwa ahjui wajibu wake na pia hana customer care unafikiri pana maendeleo hapo?

Sasa hapo ni wewe umeona Tabora kwa nini iko nyuma na kwetu sie tulioko ughaibuni huwa tunaiona Tanzania kwanini iko nyuma "Poor customer care" kuanzia airport hadi sehemu zote.
MIAFRIKA NDIVYO ILIVYO- NN
 
Taja jina la hotel Ili iwe fundisho...........inawezekana mmiliki pia yupo humu.........

siku nyingine nenda Zanzibar kale upepo na wife.......kule watu wamezoea utalii.........

Mkuu Preta Tabora ni kwetu kwahiyo kwenda kule ni sehemu ya kumpeleka mke wangu akapajue. Tena nimekumbuka kitu mkuu. Walimchukua na mke wangu kwenda kumhoji kama kweli mimi ni mume halali. Nayo iliniboa. ina maana asingekuwa mke napo ningepata kesi nyingine.......Polisi bwana...!
 
Last edited by a moderator:
Hapana mkuu......ni katika hali ya kuwa karibu na eneo la stendi.......Kwa taarifa tu kwa tabora hata hoteli iwe kubwa kiasi gani uelewa wa watu wa Tabora unafanana.

Pole sana, yaliwahi nitokea hayo mwanza, nimemwambia meneja mie nina safari asubuh na mapema, so nikipata mtu wa kunidamsha na mhudumu wa kunifungulia mlango mapema itakuwa fresh, weeh nikapitiliza usingiz ka dak 20 kufika mapokezi hamna mhudumu nilihangaika kumpata mhudumu nusu saa baadae, nikachukua boda niwah basi manake nililaza mizigo kwenye basi, kufika stend basi limesepa ilinitoka naul ya kutoka mwanza to arusha kulipia Tax, customer care ya kibongo full majanga, yani ni shiiiiiida
 
Watu wa Tabora wana tabia za Kimwinyi sana! Ni vigumu sana kuishi na jamii tofauti
 
Taja hotel kwanza,inaitwaje?ili siku nyingine tukwambie ni ipi nzuri.
 

Sasa hapo ni wewe umeona Tabora kwa nini iko nyuma na kwetu sie tulioko ughaibuni huwa tunaiona Tanzania kwanini iko nyuma "Poor customer care" kuanzia airport hadi sehemu zote.
MIAFRIKA NDIVYO ILIVYO- NN

Mkuu Tabora imezidi. Polisi kila siku wanabambika watu kesi na upeo wao mdogo sana wa uelewa. Kosa dogo mfano huna kitambulisho mfukoni unafikishwa mahakamani. Nilipoingia mahabusu ya polisi kwa masaa hayo machache niliyokaa nilikuwa ni walala hoi tupu ndio wamo humo. Yaani inasikitisha sana.....Kuna wagonjwa na watu waliokondeana. harufu kali na wadudu kama vile papasi, kunguni, viroboto ni hatari! Walining'ata kweli.
Wanaosema mahabusu zimeboreshwa ni waongo kabisa!
 
Kwanza naomba mnipe madhara ya kuitaja ama kutoitaja isije mada hii ikafutwa. kama mkinihakikishia kuitaja nitakuwa sijafanya makosa sasa hivi naianika hadharani.
Hili jambo kaka ni muhimu utaje hiyo hotel yasije yakatukuta,pia tukatumia silaa tulizo nazo kihalali kumpekekanmtu kuzimu.Hilo jambo ni muhimu kabisa kutaja tujiepushe na hiyo hotel kama ukoma.
 
Back
Top Bottom