Mnyamwezi wa Urambo
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 928
- 275
Sample size yangu ni kubwa mkuu huku ni kwetu napajua. Nimeshalala hoteli nyingi sana hapo Tabora lakini huduma ziko chini sana. Tatizo unataka kufananisha tukio hilo na hoteli zote. kwamba nikienda kulala hoteli nyingine muhudumu atanibamiza na mlango uvunjike kama ulivyovunjika wa Goodley Hotel. Sivyo! Ukilala hotel zingine utakumbana na kero ya aina nyingine.....siyo kwamba kero zinakuwa zan namna moja. naomba unielewe mkuu.
Kwa mfano unaingia hotelini unakuta toileti pepa hamna wakati ni hoteli kubwa kabisa napo utasemaje? Na kitu kama toileti pepa kuigundua haipo ni mpaka uende toileti na uwe na shida nayo. Ukiomba toileti pepa utaambia zimeisha na wewe unataka kujisaidi asubuhi uwahi. hiyo siyo kero?
Wewe ni muongo, mimi pia ni mzaliwa na nimekulia Tabora mjini. Usitegemee ulale guest za buku halafu upate matatizo uje ututukane humu. Karibu na stand kuna hoteli nyingi sana tu za maana kama GOLDEN EAGLE na FRANKMAN sijawahi kupata huduma mbaya toka kwao.
Huwezi kusema vibaya mkoa mzima kwasababu ya huyo mlevi na polisi njaa ambao wapo nchi nzima.