Yaliyojiri Uwanja wa Kambarage: Mkutano wa Dr. Magufuli Jimbo la Shinyanga Mjini - 26 Septemba, 2015

Magufuli hafai kuwa Rais.... Watanzania tufunguke macho..... CCM ni ile ile, hakuna kipya kutoka kwa CCM

Hatuwezi kumchagua fisadi Lowassa,huo urais ataishia kuusikia tu akiwa gereza la mafisadi.

Tunaenda na Magufuli, wewe endelea kula salama pesa za fisadi Lowassa maana mwishi tarehe 26/10 atakapogundua kuwa imekula kwake.
 
Mkoani Shinyanga watu wanasombwa kwa fuso,malori aina mbalimbali na matrekta kupelekwa uwanja wa Kambarage ili kutengeneza ‘mafuriko’ ambapo CCM inatarajiwa kufanya huko kampeni leo!!
 
Na leo pale Kahama ikiwa ulifuatilia vizuri wakati Sitta anahutubia, alipouliza ni wangapi watampigia kura Magufuli ... wanyoshe mikono ILIKUWA AIBU TUPU walivyokuwa wachache!
 
Nimetoka shy mida malori na matrekta toka nindo, salawe, tinde, old shinyinga, mwamnyepe, bubale, mhunze, usanda yana kazi moja ya kubeba raia
 
namsikitikia huyo mama wa watu tu. Angalia gauni limepasukia humo sasa kabaki uchiii anashikilia kwa mikono. Kisa lift ya trekta jamaniii tz kuna mambo yake. Nisombwe na trekta ati kwenda mkutano wa ccm! Ni aibu si ndiyo
 
Ndio kawaida yao ili mafuriko yawepo... wanasahau kuwa mwaka huu Kura zinebandikwa kila ktuo, maballot box hayahamishwi kituoni
 
Hinyo ndio CCM mafuriko bwana bila Lori Na trekta hakuna mafuriko mbona Sam Marla hatuambii watanzania?
 
MAGUFULI ANA PIGA PUSHUP ZA NINI MWAMBIENI ATUELEZE NI KWANINI HAJATAHIRIWA-by vincent nyerere.
 
AsoLkaw0BWoWV6nC_e9HTqriKM06Q18u3gj-5V0SEK9y.jpg
 
Leo Septemba 26, Dkt Magufuli atafanya mikutano miwili. Wa kwanza utafanyika Solwa, na wa pili utafanyika Shinyanga Mjini.

Baada ya Solwa, Dkt. Magufuli anaelekea Shinyanga Mjini ambako atafanya mkutano. Star Tv watarusha mkutano huo moja kwa moja.

#HapaKaziTu
=========

Anaeongea kwa sasa ni aliyekuwa spika wa bunge, mheshimiwa Sitta na anawaongelea wagombea urais wa vyama viwili vikubwa, Magufuli na Lowassa.Anamshukuru mwenyezi Mungu kwa genge la mafisadi kumeguka na chama kilichokuwa kinapinga mafisadi ndio kimekuwa kimbilia lao na hayo ndio mabadiliko ndani ya CCM kwa kupambana na kundi lililojenga ndani ya CCM.

Anasema tabia ya watua kujikweza ni kutafuta sifa, aliamini matumizi makubwa ya pesa yataitisha kamati kuu ya CCM, akisahau mojawapo ya sifa ni uadilifu wa mgombea.

Naamini serikali ya Magufuli itakuwa na serikali isiyo na ufisadi, serikali inayowajali wanyonge.

Anaeongea kwa sasa ni mgombea Urais kupitia CCM, John Magufuli na anaongelea atakayofanya endapo watanzania watampa ridhaa ya kuwaongoza. Anasema mafisadi wanakimbia baada ya yeye kuteuliwa CCM kugombea kupitia CCM.

Anaongelea matatizo ya walimu na atakavyoyatatua, anaongelea pia wafanyakazi wanaofanya vibaya sehemu moja na kuhamishwa sehemu nyingine. Kwenye elimu anaongelea kuondoa karo ya shule na michango darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.



AsoLkaw0BWoWV6nC_e9HTqriKM06Q18u3gj-5V0SEK9y.jpg
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom