Yaliyojiri Uwanja wa Kambarage: Mkutano wa Dr. Magufuli Jimbo la Shinyanga Mjini - 26 Septemba, 2015

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,906
10,389
Leo Septemba 26, Dkt Magufuli atafanya mikutano miwili. Wa kwanza utafanyika Solwa, na wa pili utafanyika Shinyanga Mjini.

Baada ya Solwa, Dkt. Magufuli anaelekea Shinyanga Mjini ambako atafanya mkutano. Star Tv watarusha mkutano huo moja kwa moja.

#HapaKaziTu
=========

Anaeongea kwa sasa ni aliyekuwa spika wa bunge, mheshimiwa Sitta na anawaongelea wagombea urais wa vyama viwili vikubwa, Magufuli na Lowassa.Anamshukuru mwenyezi Mungu kwa genge la mafisadi kumeguka na chama kilichokuwa kinapinga mafisadi ndio kimekuwa kimbilia lao na hayo ndio mabadiliko ndani ya CCM kwa kupambana na kundi lililojenga ndani ya CCM.

Anasema tabia ya watua kujikweza ni kutafuta sifa, aliamini matumizi makubwa ya pesa yataitisha kamati kuu ya CCM, akisahau mojawapo ya sifa ni uadilifu wa mgombea.

Naamini serikali ya Magufuli itakuwa na serikali isiyo na ufisadi, serikali inayowajali wanyonge.

Anaeongea kwa sasa ni mgombea Urais kupitia CCM, John Magufuli na anaongelea atakayofanya endapo watanzania watampa ridhaa ya kuwaongoza. Anasema mafisadi wanakimbia baada ya yeye kuteuliwa CCM kugombea kupitia CCM.

Anaongelea matatizo ya walimu na atakavyoyatatua, anaongelea pia wafanyakazi wanaofanya vibaya sehemu moja na kuhamishwa sehemu nyingine. Kwenye elimu anaongelea kuondoa karo ya shule na michango darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.


 
Last edited by a moderator:
Matukio katika Picha...

m1.jpeg
Wanakijiji wa Burige wamejitokeza barabarani alfajiri kuzungumza na Dkt. Magufuli, akielekea Shinyanga vijijini.
 
Baroda sana hapa kazi tu, kanda ya ziwa tunajiamini kwa sauti moja na kuwahakikishia watanzania tunawaletea rais wenu mnayemtaka, mchapa kazi na muadilifu ..sisi kama wenye kuandaa send-off, tutamuaga kwa tafrija na bashasha za bambamu, tutampa zawadi nyingi sana na kumfunda vyema ili aje kuwa rais muadilifu na mwenye manufaa kwa watanzania wooote na hata siku moja watanzania hawatajuta ..tunawashukuru sana watanzania wenzetu kwa kutupa heshima kuu na Magufuri atakuwa ni wa kwetu sote, pokeeni Magufuri.
 
Barida sana hapa kazi tu, kanda ya ziwa tunajiamini kwa sauti moja na kuwahakikishia watanzania tunawaletea rais wenu mnayemtaka, mchapa kazi na muadilifu ..sisi kama wenye kuandaa send-off, tutamuaga kwa tafrija na bashasha za bambamu, tutampa zawadi nyingi sana na kumfunda vyema ili aje kuwa rais muadilifu na mwenye manufaa kwa watanzania wooote na hata siku moja watanzania hawatajuta ..tunawashukuru sana watanzania wenzetu kwa kutupa heshima kuu na Magufuri atakuwa ni wa kwetu sote, pokeeni Magufuri. Hapa kazi tu.
 
Nilimkataa Lowassa akiwa ndani ya CCM, ninaendelea kumkataa akiwa nje ya CCM.

Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania.

I can't let our beautiful country go to the dogs

ww mwenyewe wazazi wako walishakukataa toka ukiwa tumboni mwao....hiyo dhambi unadhani itaisha itaendelea kukutafuna ukatae kila kitu hadi mungu wako...
bt mabadiliko ni pai dee swuare over four.
 
Sitta anasema mradi wa maji kutoka ziwa Victoria ulitekelezwa na Mkapa na si Lowasa pekee...pia Mwandosya alihusika.
 
Kwamba Lowasa anatabia za kujikweza na kuona kila jambo yy pekee ndio analijua na kulitekeleza- Sitta
 
Leo Septemba 26, Dkt Magufuli atafanya mikutano miwili. Wa kwanza utafanyika Solwa, na wa pili utafanyika Shinyanga Mjini.

Baada ya Solwa, Dkt. Magufuli anaelekea Shinyanga Mjini ambako atafanya mkutano. Star Tv watarusha mkutano huo moja kwa moja.

#HapaKaziTu
=========

Anaeongea kwa sasa ni aliyekuwa spika wa bunge, mheshimiwa Sitta na anawaongelea wagombea urais wa vyama viwili vikubwa, Magufuli na Lowassa.


#Hapa upumbavu tu
 
Last edited by a moderator:
Nyani hajioni nyuma...
Makufuli anaiponda serikali yake ya CCM kuwa..
1-Anasema serikali ya CCM imekithiri wizi wa
madawa ya hospitali
2-Anasema serikali ya CCM,Inatumia mgambo
kutesa wananchi
3-Anasema CCM imejaa ukiritimba hadi wanafunzi
wananyimwa mikopo..
4-Chini ya utawala wa ccm anasema kuna uporaji
mkubwa wa ardhi..
5-Utawala wa CCM anasema umejaa watendaji
wabovu..
kumbe serikali ya CCM haifai.
Kikwete anasema Makufuli yupo sahihi kuiponda
CCM kwa sababu anataka mabadiliko,M4C..lol
LAKINI
1-Na yeye alipora nyumba nane alipokua Wizara ya
ardhi.
2-Anawalaumu mgambo anasahau alivyokua
akiwawinda wavuvi masikini, mchana na
usiku,anasahau alipovunja sheli ya mtu Mwanza
kwa chuki binafsi akapigwa faini mahakamani..
3-Anailamu serikali yake ya CCM kwa kutowapa
wanafunzi mikopo kwa wakati ,anasahau Wizara
yake ya ujenzi ilipigwa faini ya bilioni mia tisa kwa
kutolipa wakandarasi..
5-Analaumu serikali yake ya CCM kua na watendaji
wabovu anasahau alinunua kivuko kibovu MV Dar
es Salaam cha mwaka 1978 kwa bilioni 6 hivi
karibuni,aliongeza nauli za vivuko lakini mara kwa
mara vivuko hivyo huzimika majini..
6-Anawataka wananchi wasikubali mabadiliko
lakini anajiita Makufuli for Change..
duh
@rif 2015
Cha kushangaza zaidi Wabunge wa Upinzani
walikua wakipigia kelele hayo mambo yote hapo
juu kwenye mijadala mbalimbali Bungeni lakini
Magufuli na CCM wenzake walikua ndio wa kwanza
kuwabeza Wabunge wa Upinzani walipokua
wakitetea Maslahi ya Wananchi kwa ujumla.
Sasa leo hii kwa kutuona watanzania ni
Wapumbavu na Malofa wanapanda Jukwaani na
kuomba Kura kwa kutumia Matatizo
waliyoyasababisha wao wenyewe kwa kutotimiza
wajibu wao ipasavyo na Rais nae bila aibu
anakubaliana kabisa na yanayotamkwa na
mgombea wa Chama chake ambaye ni Mjumbe
kwenye Baraza lake la Mawaziri hivi jamani hawa
watu wanatuonaje? Au ndio maana walituita Malofa
na Wapumbavu? Inatia hasira sana. Tumuombe
Mungu atupe uzima ili tuikomboe Nchi yetu kutoka
kwa hawa Wakoloni weusi ifikapo October 25.
 
ww mwenyewe wazazi wako walishakukataa toka ukiwa tumboni mwao....hiyo dhambi unadhani itaisha itaendelea kukutafuna ukatae kila kitu hadi mungu wako...
bt mabadiliko ni pai dee swuare over four.

toka hapa na wewe mabandiliko ngani hayo nahiyo ilani yenu yakumutoa babusea kifungoni?
 
Lowasa aliondoka serikalini miaka 8 iliyopita. Sumaye aliondika serikalini miaka 10 iliyopita. Sasa tujiulize maswali yafuatayo-
Hivi kweli kwa takribani miaka nane hakuna ufisadi uliotokea? Zaidi ya richmond? Mbona majukwaa ya kampeni za ccm hawayataji hayo?
CCM ime divert na kuwaduwaza watanzania na kusahau ESCROW, TOKOMEZA, Mabehewa ya train mabovu , rada etc, wanachozungumza ni Lowasa na richmond tuu. Ama kweli nimeamini watanzania ni NYUMBU
 
Back
Top Bottom