Yaliyojiri Semina ya Hali ya Uchumi wa Dunia: Mambo muhimu ya kuzingatia na maana yake kwa Afrika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,981
Habari wadau,

Leo nimebahatika kuhudhuria semina ya 'Hali ya Uchumi wa Dunia: Mambo muhimu ya kuzingatia na maana yake kwa Afrika' (The State of the Global Economy, Key Concerns and Implications for Africa).

Semina hii imeandaliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) inafanyika katika ukumbi Council Chamber hapa UDSM.

Mada hiyo inasilishwa na Dkt. Felipe Jaramillo, Mkurugenzi Mkuu wa Uchumi, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia.

Shughuli hii itaendeshwa pia na Prof Bonaventure Rutinwa ambaye ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo na Bi. Bella Bird ambaye ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Somalia.

Presentantion ya Dkt. Jaramillo itajadiliwa na wafuatao:-

  • Prof Samuel Wangwe
  • Prof Andrew Temu
  • Dr. Servacius Likwelile

Washirikia wameanza kuingia ukumbini na semina itaanza muda si mrefu. Nitahakikisha unapata yote yanayojiri hapa. JF pia wako live..

Updates
Anaanza kuongea Prof Bonaventure Rutinwa ambapo anawatambulisha waalikwa kutoka katika taasisi mbalimbali

- Kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nawakaribisha kwenye semina muhimu juu ya uchumi wa dunia. UDSM inaamini kuwa semina hii imekuja wakati muhimu kwa ajili ya vijana kujiandaa kwa ajira na ukuaji wa uchumi.

Bi. Bella Bird
- Anaelezea kwa ufupi juu ya kazi za Benki ya dunia Tanzania ambapo anasema ni kushirikiana na wadau katika shughuli za maendeleo ikiwemo kutekeleza miradi.

- Anamkaribisha muwasilishaji mada aongee na hadhira

Dkt. Felipe Jaramillo -
Muwasilishaji Mada

- Ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania. Nimepata fursa hii ya kuja kubadilishana uzoefu katika masuala ya uchumi kuhusu Afrika inavyoweza kukua kiuchumi na mambo gani ya msingi ya kuzingatia.

- Uchumi wa Tanzania unafanya vizuri duniani lakini changamoto ni kutokuwepo kwa miundombinu imara na mazingira mazuri kwa wawekezaji kuwekeza.

- Mwaka 2006 uchumi wa Afrika ulikuwa kwa kiwango kikubwa kuliko ule wa bara la Asia lakini miaka iliyofuata haukufanya vizuri. Uchumi wa Tanzania umeimarika na unakuwa kwa asilimia zaidi ya 5. Kwa ujumla uchumi wa Afrika unakuwa kwa kiwango kizuri.

Anasema Ukuaji wa uchumi kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara umekuwa hadi asilimia 3.2 mwaka 2018 na utafikia 3.5 ifikapo 2019 ambapo ni juu ya kidogo ya ukuaji wa idadi ya watu.

Kwa upande wa usafirishaji wa mafuta, ukuaji wa pato utakuwa mdogo lakini utaimalika nchini Ghana. Ukuaji katika nchi ambazo hazitegemei rasilimali asilia utakuwa wa kuridhisha, ukichagizwa na Senegal na Ivory Cost.

---Lakini jitihada zinahitajika kupunguza umaskini kwa sababu kiwango cha umaskini uliopitiliza kimeongezeka kutoka asilimia 15 mwaka 1990 hadi kufikia asilimia 49 mwaka 2015, licha ya idadi hiyo kwa dunia nzima kupungua kutoka watu bilioni 1.9 hadi milioni 702

- Uwekezaji wa dunia ulikuwa mzuri kwa mwaka 2017 na nchi nyingi zinazoendelea zilifanya vizuri kwenye uchumi lakini changamoto ni mazingira ya kufanyia biashara na ubovu wa miundombinu.

Licha ya sekta ya kilimo kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi bado wakulima hawajawezeshwa kuzalisha mazao na bidhaa zenye ubora zinaweza kushindanishwa kwenye soko la dunia ili kutengeneza kipato.

- Changamoto nyingine ni nchi za Afrika hazina balance nzuri kati ya mapato na matumizi ambapo rasilimali hazitumiwi vizuri kuondoa umaskini kwa wananchi

Nini Kifanyike

-
Matumizi ya teknolojia mpya na ya kisasa yatasaidia kuongeza uzalishaji

- Kuongeza ujuzi kwa wananchi ili waweze kuvumbua teknolojia na kuzalisha nguvu kazi itakayoongeza uzalishaji katika sekta mbalimbali

- Mbadiliko ya sera za kiuchumi ni muhimu ili kuendana na hali ya uchumi ya dunia na kuvutia wawekezaji mbalimbali ili kuwekeza katika miradi ya maendeleo

- Kuna haja ya kuboresha miundombinu hasa barabara ili kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza katika maeneo ya uzalishaji barani Afrika.

- Afrika inatakiwa kuimarisha taasisi zake za utendaji ili zijiendeshe kwa uwazi.

AFRICA.PNG

Prof Samuel Wangwe
-
Presentation ni nzuri imetoa mwanga kwa uchumi wa Afrika na Tanzania lakini kuna mambo muhimu lazima yaangaliwe ili kukuza uchumi wa Afrika.

- Tuongeze uzalishaji wa bidhaa ili kuongeza usambaji na kupata masomo ya bidhaa hizo.

- Ili uchumi ukue lazima kuwe na muunganiko mzuri wa uzalishaji ikiwemo kilimo na viwanda.

- Ni kuangalia sekta zipi tunazipa umihimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi mfano kilimo lazima kiangaliwe upya kwasababu hakijarasimishwa na kuwa rasmi ndio maana uzalishaji wake haukui na kuleta matokeo chanya kwenye uchumi wa nchi.

- Pia tuelewe utendaji wa uchumi dunia na unavyoathiri uchumi wa nchi ili tujiweke katika nafasi ya kukabiliana na mabadiliko yanoyotokea hasa kwenye soko la bidhaa.

Dr. Servacius Likwelile

Anasema kuna haja kuziwezesha sekta za fedha kuwa na utendaji mzuri. Pia kilimo kiangaliwe ili kiwe na mchango mzuri katika ukuaji wa viwanda.

Prof Andrew Temu
Umetuambia tuangalie mabadiliko ya sera lakini mimi naona mambo muhimu ya kuzingatia ni kwenye uzalishaji jumuishi ambao unahusisha sekta zote. Sera zetu lazima zilenge kutengeneza ajira na kuongeza wigo wa kupata kodi.

- Sekta ya fedha iangaliwe ili kuziongezea uwezo sekta nyingine za uzalishaji ikiwemo kilimo ili wakulima wapate teknolojia na fedha za kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa. Benki ya Maendeleo (TIB) ingalie zaidi sekta ya kilimo kwasababu ndio kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi.

- Wasomi wetu kutoka vyuoni wawekwe pamoja ili kuwa na mawazo chanya na kuwaongezea ujuzi wa kuzalisha katika sekta mbalimbali.

Washiriki wa semina wanapewa nafasi ya kuchangia mada iliyowasilishwa....

Tatizo sio ujuzi na maarifa au kuimarisha mfumo wa elimu, changamoto ni kuhusisha mabadiliko ya teknolojia na maendeleo kwasababu wananchi wengi ni maskini wanahitaji kutoka hapo walipo, tunawasadiaje hawa?

Vicent Mkwai

Anauliza ni mambo gani ya muhimu yanahiyajika ili nchi ifanikiwe kiviwanda na unawaandaje wananchi kutekeleza sera hiyo? Pia sekta binafsi imehusishwaje katika maendeleo?

Hatuna budi kuwa makini na takwimu zinazotolewa pale tunapolinganisha na nchi nyingine kwasababu wakati mwingine zinadanganya. Bado njia wanazotumia kwa uzalishaji hazikidhi mahitaji ya soko la kimataifa.

Azaveli Lweitama
Mmeongelea uvumbuzi na bidhaa mpya, nafikiri kuna haja ya kuhusisha uwekezaji huo na kuwaongezea ujuzi wanafunzi katika shule za msingi na sekondari kujifunza uwekezaji utakaofungua maeneo mbalimbali nchi kukua kiuchumi.

Hitimisho
Katika kuhitimisha semina hiyo juu ya ukuaji wa uchumi wa Afrika, Program Manager kutoka Benki ya Dunia, Yutaka Yoshino amesema Afrika na nchi nyingine ikiwemo Tanzania ipige hatua ya maendeleo ni muhimu kuboresha miundombinu, taasisi za serikali kufanya kazi kwa uwazi. Pia kutumia teknolojia ya kisasa katika uzalishaji na kuwaongezea ujuzi wananchi katika shughuli za uchumi.
 
Uchumi ukue huku na wananchi wakiwa hawana hofu ya kuuawa au wapinzani kusingiziwa kesi pamoja na kuteswa wasio hatia.
Vinginevyo ni kumpigia mbuzi gitaa.

My prayers: Get well soon , Hon.TA. Lisu.

R.I. P. Binti Akwilina A. B.
R.I.P Diwani CDM wa huko mkoani Morogoro.
Ndoto zenu zote zimezimwa ghafula kama vile mshumaa uzimwavyo.
 
Tatizo la wachumi wanaongea theory sana, bila ya kutazama mazingira yamebadilika. Wachumi wengi wamekariri macroeconomics and microeconomics which are static in nature depending on traditional theory. Lazima tuwe dynamic. Mfano, kwa sasa hata mashuleni inatakiwa wafundishwe clinical economics, ambapo unafanya economical diagnosis na kupata long run solution ya matatizo yetu.

Wachumi kama kina wangwe na kina temu wamepitwa na wakati, na sana sana watapiga blah blah tu!!!!
 
Kwani yule aliyesema, amegundua siri kwa nini hakuna hela, yeye hajaalikwa na wakati ana ugunduzi muhimu kwa nchi??
 
Tatizo la wachumi wanaongea theory sana, bila ya kutazama mazingira yamebadilika. Wachumi wengi wamekariri macroeconomics and microeconomics which are static in nature depending on traditional theory. Lazima tuwe dynamic. Mfano, kwa sasa hata mashuleni inatakiwa wafundishwe clinical economics, ambapo unafanya economical diagnosis na kupata long run solution ya matatizo yetu.

Wachumi kama kina wangwe na kina temu wamepitwa na wakati, na sana sana watapiga blah blah tu!!!!
Well said bro!
 
Duh!! Hii mpya yaani wachumi waliopitwa na wakati na wa ki leo wapoje mkuu?
 
Naufatilia vizuri sana mjadala kupitia JF. Mpaka sasa watanzania hawajaniangusha...kwenye mjadala huu. They are pouring in very sensible questions and comments.
 
Hayo mambo yapo na kila siku tunasema nini kifanyike lakini serikali imekuwa siyo sikivu. Ama ni nzito kutekeleza ya muhimu, ili walau hata tufike uchumi wa kati. Hiki kitu, kinaliponza taifa.
 
Duh!! Hii mpya yaani wachumi waliopitwa na wakati na wa ki leo wapoje mkuu
Mkuu kuna kitu kinaitwa clinical economics. Ili ujue tatizo LA nchi lilipo, lazima ufanye economical diagnosis, mfano, je umaskini tulionao unatokana na aina ya watu wetu? Au inatokana na hali ya hewa kubadilika? Au taasisi zetu haziko imara? Au human resource ya kuweza kuleta mabadiliko haijapewa kipaumbele? Au tuna weak financial banks and capital market kuweza Ku influence growth? Au tatizo ni wanasiasa tulionao na siasa wanazozifanya? Here you have to diagnose and come up with the final solution..!!! Siyo blah blah tu brother kama za hao maprofesa wako
 
Tunaipongeza Mahakama kwa Kutenda haki na kumfunga Mbunge Joseph Mbilinyi na Kutoa fundisho dhidi ya Watu wanaotumia Lugha za Kihuni.
 
Mkuu kuna kitu kinaitwa clinical economics. Ili ujue tatizo LA nchi lilipo, lazima ufanye economical diagnosis, mfano, je umaskini tulionao unatokana na aina ya watu wetu? Au inatokana na hali ya hewa kubadilika? Au taasisi zetu haziko imara? Au human resource ya kuweza kuleta mabadiliko haijapewa kipaumbele? Au tuna weak financial banks and capital market kuweza Ku influence growth? Au tatizo ni wanasiasa tulionao na siasa wanazozifanya? Here you have to diagnose and come up with the final solution..!!! Siyo blah blah tu brother kama za hao maprofesa wako
Hapo sasa nimekuelewa mkuu.

Lakini ulivyosema wachumi wa kizamani ndio nilikuwa na shaka mkuu.

Ila umefafanua points yako vizuri,nimekuelewa sana. Ila tutumie ct-scan au blood picture au ultrasound tukiwa tunafanya iyo diagnosis?

Hongera na pamoja
 
Habari wadau,

Leo nimebahatika kuhudhuria semina ya 'Hali ya Uchumi wa Dunia: Mambo muhimu ya kuzingatia na maana yake kwa Afrika' (The State of the Global Economy, Key Concerns and Implications for Africa).

Semina hii imeandaliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) inafanyika katika ukumbi Council Chamber hapa UDSM.

Mada hiyo inasilishwa na Dkt. Felipe Jaramillo, Mkurugenzi Mkuu wa Uchumi, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia.

Shughuli hii itaendeshwa pia na Prof Bonaventure Rutinwa ambaye ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo na Bi. Bella Bird ambaye ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Somalia.

Presentantion ya Dkt. Jaramillo itajadiliwa na wafuatao:-

  • Prof Samuel Wangwe
  • Prof Andrew Temu
  • Dr. Servacius Likwelile

Washirikia wameanza kuingia ukumbini na semina itaanza muda si mrefu. Nitahakikisha unapata yote yanayojiri hapa. JF pia wako live..

Updates
Anaanza kuongea Prof Bonaventure Rutinwa ambapo anawatambulisha waalikwa kutoka katika taasisi mbalimbali

- Kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nawakaribisha kwenye semina muhimu juu ya uchumi wa dunia. UDSM inaamini kuwa semina hii imekuja wakati muhimu kwa ajili ya vijana kujiandaa kwa ajira na ukuaji wa uchumi.

Bi. Bella Bird
- Anaelezea kwa ufupi juu ya kazi za Benki ya dunia Tanzania ambapo anasema ni kushirikiana na wadau katika shughuli za maendeleo ikiwemo kutekeleza miradi.

- Anamkaribisha muwasilishaji mada aongee na hadhira

Dkt. Felipe Jaramillo -
Muwasilishaji Mada

- Ni mara yangu ya kwanza kufika Tanzania. Nimepata fursa hii ya kuja kubadilishana uzoefu katika masuala ya uchumi kuhusu Afrika inavyoweza kukua kiuchumi na mambo gani ya msingi ya kuzingatia.

- Uchumi wa Tanzania unafanya vizuri duniani lakini changamoto ni kutokuwepo kwa miundombinu imara na mazingira mazuri kwa wawekezaji kuwekeza.

- Mwaka 2006 uchumi wa Afrika ulikuwa kwa kiwango kikubwa kuliko ule wa bara la Asia lakini miaka iliyofuata haukufanya vizuri. Uchumi wa Tanzania umeimarika na unakuwa kwa asilimia zaidi ya 5. Kwa ujumla uchumi wa Afrika unakuwa kwa kiwango kizuri.

Anasema Ukuaji wa uchumi kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara umekuwa hadi asilimia 3.2 mwaka 2018 na utafikia 3.5 ifikapo 2019 ambapo ni juu ya kidogo ya ukuaji wa idadi ya watu.

Kwa upande wa usafirishaji wa mafuta, ukuaji wa pato utakuwa mdogo lakini utaimalika nchini Ghana. Ukuaji katika nchi ambazo hazitegemei rasilimali asilia utakuwa wa kuridhisha, ukichagizwa na Senegal na Ivory Cost.

---Lakini jitihada zinahitajika kupunguza umaskini kwa sababu kiwango cha umaskini uliopitiliza kimeongezeka kutoka asilimia 15 mwaka 1990 hadi kufikia asilimia 49 mwaka 2015, licha ya idadi hiyo kwa dunia nzima kupungua kutoka watu bilioni 1.9 hadi milioni 702

- Uwekezaji wa dunia ulikuwa mzuri kwa mwaka 2017 na nchi nyingi zinazoendelea zilifanya vizuri kwenye uchumi lakini changamoto ni mazingira ya kufanyia biashara na ubovu wa miundombinu.

Licha ya sekta ya kilimo kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi bado wakulima hawajawezeshwa kuzalisha mazao na bidhaa zenye ubora zinaweza kushindanishwa kwenye soko la dunia ili kutengeneza kipato.

- Changamoto nyingine ni nchi za Afrika hazina balance nzuri kati ya mapato na matumizi ambapo rasilimali hazitumiwi vizuri kuondoa umaskini kwa wananchi

Nini Kifanyike

-
Matumizi ya teknolojia mpya na ya kisasa yatasaidia kuongeza uzalishaji

- Kuongeza ujuzi kwa wananchi ili waweze kuvumbua teknolojia na kuzalisha nguvu kazi itakayoongeza uzalishaji katika sekta mbalimbali

- Mbadiliko ya sera za kiuchumi ni muhimu ili kuendana na hali ya uchumi ya dunia na kuvutia wawekezaji mbalimbali ili kuwekeza katika miradi ya maendeleo

- Kuna haja ya kuboresha miundombinu hasa barabara ili kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza katika maeneo ya uzalishaji barani Afrika.

- Afrika inatakiwa kuimarisha taasisi zake za utendaji ili zijiendeshe kwa uwazi.

View attachment 701773

Prof Samuel Wangwe
-
Presentation ni nzuri imetoa mwanga kwa uchumi wa Afrika na Tanzania lakini kuna mambo muhimu lazima yaangaliwe ili kukuza uchumi wa Afrika.

- Tuongeze uzalishaji wa bidhaa ili kuongeza usambaji na kupata masomo ya bidhaa hizo.

- Ili uchumi ukue lazima kuwe na muunganiko mzuri wa uzalishaji ikiwemo kilimo na viwanda.

- Ni kuangalia sekta zipi tunazipa umihimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi mfano kilimo lazima kiangaliwe upya kwasababu hakijarasimishwa na kuwa rasmi ndio maana uzalishaji wake haukui na kuleta matokeo chanya kwenye uchumi wa nchi.

- Pia tuelewe utendaji wa uchumi dunia na unavyoathiri uchumi wa nchi ili tujiweke katika nafasi ya kukabiliana na mabadiliko yanoyotokea hasa kwenye soko la bidhaa.

Dr. Servacius Likwelile

Anasema kuna haja kuziwezesha sekta za fedha kuwa na utendaji mzuri. Pia kilimo kiangaliwe ili kiwe na mchango mzuri katika ukuaji wa viwanda.

Prof Andrew Temu
Umetuambia tuangalie mabadiliko ya sera lakini mimi naona mambo muhimu ya kuzingatia ni kwenye uzalishaji jumuishi ambao unahusisha sekta zote. Sera zetu lazima zilenge kutengeneza ajira na kuongeza wigo wa kupata kodi.

- Sekta ya fedha iangaliwe ili kuziongezea uwezo sekta nyingine za uzalishaji ikiwemo kilimo ili wakulima wapate teknolojia na fedha za kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa. Benki ya Maendeleo (TIB) ingalie zaidi sekta ya kilimo kwasababu ndio kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi.

- Wasomi wetu kutoka vyuoni wawekwe pamoja ili kuwa na mawazo chanya na kuwaongezea ujuzi wa kuzalisha katika sekta mbalimbali.

Washiriki wa semina wanapewa nafasi ya kuchangia mada iliyowasilishwa....

Tatizo sio ujuzi na maarifa au kuimarisha mfumo wa elimu, changamoto ni kuhusisha mabadiliko ya teknolojia na maendeleo kwasababu wananchi wengi ni maskini wanahitaji kutoka hapo walipo, tunawasadiaje hawa?

Vicent Mkwai

Anauliza ni mambo gani ya muhimu yanahiyajika ili nchi ifanikiwe kiviwanda na unawaandaje wananchi kutekeleza sera hiyo? Pia sekta binafsi imehusishwaje katika maendeleo?

Hatuna budi kuwa makini na takwimu zinazotolewa pale tunapolinganisha na nchi nyingine kwasababu wakati mwingine zinadanganya. Bado njia wanazotumia kwa uzalishaji hazikidhi mahitaji ya soko la kimataifa.

Azaveli Lweitama
Mmeongelea uvumbuzi na bidhaa mpya, nafikiri kuna haja ya kuhusisha uwekezaji huo na kuwaongezea ujuzi wanafunzi katika shule za msingi na sekondari kujifunza uwekezaji utakaofungua maeneo mbalimbali nchi kukua kiuchumi.

Hitimisho
Katika kuhitimisha semina hiyo juu ya ukuaji wa uchumi wa Afrika, Program Manager kutoka Benki ya Dunia, Yutaka Yoshino amesema Afrika na nchi nyingine ikiwemo Tanzania ipige hatua ya maendeleo ni muhimu kuboresha miundombinu, taasisi za serikali kufanya kazi kwa uwazi. Pia kutumia teknolojia ya kisasa katika uzalishaji na kuwaongezea ujuzi wananchi katika shughuli za uchumi.

Pelekeni jukwaa la uchumi
 
Nani anaandaa hizi mada?

Kwanin hawajadili mchango wa makampuni makubwa ya wazungu katika kufukarisha afrika kupitia mikataba ya ovyo?
 
Back
Top Bottom