Uchaguzi 2020 Yaliyojiri: Mapokezi ya Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu na mkutano mkubwa Shinyanga

YOU MUST BE STUPID! You can not compare Lisu with magu in intellectuality, upstairs capability!
 


WanaJF

Karibuni kufuatilia mapokezi makubwa ya Mgombea Urais CHADEMA Tundu Lissu hapa mjini Shinyanga.

Lissu anatarajiwa kuhutubia mkutano Mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Joshoni ikiwa ni uzinduzi wa kampeni kwa Kanda ya Serengeti.

Mgombea huyo wa Urais anaambatana na Mgombea Mwenza Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe

Sisi wa Molemo Media tumesafiri usiku kucha kutokea Mwanza na tupo hapa Shinyanga kuihabarisha dunia.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu ameingia Kanda ya Serengeti (Mara, Shinyanga & Simiyu) ambapo leo atakuwepo Shinyanga Mjini akiambatana na Mgombea-mwenza, Salum Mwalim pamoja na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe

Picha zikionesha msafara wa Mgombea Urais wa JMT kwa Tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu tangu alipotua Uwanja wa Ndege wa Kahama leo asubuhi. Kisha kuanza safari ya kuelekea Shinyanga mjini ambapo alilazimika kusimama mara kadhaa sehemu mbalimbali kuwasalimia mamia ya wananchi waliosimama barabarani kuzuia msafara wakiomba awahutubie.

=========
Mnyika: Naomba mjiandae kwa sababu safari hii wamedhamiria kudhibiti mawakala wetu wasiingie vituoni, nyinyi wananchi kwa nguvu ya umma kabla ya kupiga kura awepo ndani ya kituo cha kupigia kura.

Wamejiandaa safari hii, ni hiari kumpa nakala ya matokeo ya uchaguzi wakala wa CHADEMA kwenye kituo cha kupigia kura, nawaambia mapema ili nyinyi wananchi muungane na sisi kwa pamoja katika ulinzi wa kura zetu kuhakikisha kila kituo cha kupigia kura tunapata nakala ya matokeo iliyoonesha Lissu ameshinda na inabandikwa kituoni..
Nimeshangazwa huyu Rais dikteta, Rais anayejiita mbabe, anayejiita jiwe eti leo anawawekea mabango Magufuli ni mtu mnyenyekevu kwelikweli, sasa basi.

Mbowe: Leo tunazungumza baada ya miaka mitano ya kufungwa midomo, mtakumbuka CHADEMA tulikuwa tunakuja Shinyanga mara kwa mara lakini leo tunaenda kucheza mchezo baada ya kukaa miaka mitano bila mazoezi, alafu alietufungia kwa miaka matano naye atakuja kesho, atabeba watu kutoka mikoa mbalimbali kwa matrekta, punda, malori

Hakuna kitu kibaya kama mtu kukunyima uhuru wako, miaka mitano tunashindwa kuzungumza. Unapiga marufu mikutano ya vyama vingine shindani, unaruhusu mikutano ya watu wako. Hii si haki na lazima tuoneshe hasira tarehe 28/10 siku ya kupiga kura.

Tumeona miaka matano ya udikteta katika nchi yetu kwamba kiongozi mkubwa ambae ni Rais anataka kuzungumza peke yake. Amefunga vyombo vyote vya habari vimsifie yeye. Vyo mbo sio vyake, sio vya ukoo wake, ni vyombo vya umma vinavyoendeshwa kwa kodi za watanzania.

Rais wetu anaendesha hii nchi kama ya ukoo wake, hii nchi inaendeshwa kwa katiba na inastahili kuheshimu katiba. Hata Raisi wetu tnaomba mumchague tarehe 28, tunategemea ataiongoza kwa misingi ya katiba na sheria.

Sehemu ya Hotuba ya Mgombea Urais Tundu Lissu

"Shinyanga inaongoza kwa idadi ya ng'ombe Tanzania lakini miaka nenda rudi wafugaji wananyanyaswa na tozo za ajabuajabu, imekuwa adha kuwa mfugaji, tutalimaliza hili tukipewa nafasi” - Mgombea Urais kwa Ticket ya CHADEMA, Tundu Lissu akiwa Shinyanga

“Serikali ya CHADEMA tutahakikisha tunatengeneza utaratibu utakaowawezesha wafugaji kwenda kufuga kwenye hifadhi wakati wa shida ya maji au ya majani, inawezekana, kama iliwezekana wakati hifadhi hazijaanzishwa itawezekana sasa, Nchi za wenzetu wanafanya" - LISSU

“Huu ni Mkoa wenye utajiri wa madini, Mimi nimekuwa maarufu Kimataifa kisa dhuluma waliyofanyiwa hapa Shinyanga mwaka 1996, Wachimbaji wakafukuzwa, niliwatetea nikakamatwa nikalala ndani na ndicho kilichofanya nipate kesi ya kwanza ya uchochezi wakati wa Serikali ya Mkapa" -LISSU

"Mkoa wa Shinyanga ndio Mkoa unaolima pamba kwa wingi kuliko Mkoa wowote Tanzania, niambieni wakulima nani ambaye hajakopwa pamba yake?, mnalima,mbegu, pembejeo zenu mkivuna mnakopwa hamlipwi, tutahakikisha mnatendewa haki na hamkwopi, toa pesa upewe pamba"- Mgombea Urais kwa ticket ya CHADEMA, Tundu Lissu akiwa Shinyanga

"Wafanyakazi wetu kibao wamefilisiwa na TRA, tutainyang'anya TRA mamlaka ya kufilisi, tuwe na mfumo wa kodi utakaojali haki ya mlipa kodi, tukifanya hivyo hela itakuwepo mtaani"-LISSU

"Serikali ya CHADEMA itakuwa Serikali ya haki,Askari Barabarani wamekuwa wakusanya kodi badala ya kuwa Walinzi wa Barabarani,kodi zote za aina hii tutaziondoa, tutafuta machozi ya Wachimbaji wadogo,Wafugaji na Wakulima, haki huinua Taifa"-LISSU

View attachment 1556422View attachment 1556423View attachment 1556431View attachment 1556721View attachment 1556722View attachment 1556723View attachment 1556724

Picha mbalimbali zikionesha Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu, kwa Kanda ya Serengeti (Shinyanga, Mara na Simiyu) uliofanyika leo Septemba 3, 2020, katika Uwanja wa Lubasha joshoni, Manispaa ya Shinyanga. Mbali ya Mgombea Urais Mhe. Tundu Lissu, wengine waliohutubia uzinduzi huo ni Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika.
View attachment 1556808View attachment 1556809View attachment 1556810View attachment 1556819View attachment 1556822View attachment 1556822View attachment 1556821View attachment 1556820View attachment 1556818View attachment 1556816View attachment 1556817View attachment 1556816View attachment 1556814View attachment 1556812View attachment 1556815View attachment 1556811

Hizi ndizo picha za Shinyanga sasa siyo zile alizoweka Henry. Ndiyo maana utopolo yanatuita sisi nyumbu! Tunajidhalilisha sana, mafuriko yapo lakini bado tunaweka picha za Lowassa hii haitusaidii bali inatudumaza! Kitu chengine nyie Molemo mnarudisha nyuma sana maendeleo, kulikoni hakuna live stream kwenye internet? Mnajua kabisa tumebaniwa kwa nini CHADEMA live isiwe hewani muda wote? Ina maana hatuna pesa za kampeni kiasi hicho? Kitengo cha habari CHADEMA kinatuangusha sana, mbona mlimani pale kuna vijana wazuri tu wa IT kwa nini msiwachukue wasaidie katika hili? Zile pesa walizokuwa wanakatwa wabunge wetu ndio wakati wa kuzitumia sasa! Safari hii tukishindwa kumtoa mkoloni mweusi mtu asinifuate tena!!
 
Back
Top Bottom