Yaliyojiri kwenye uzinduzi wa TAKUKURU wa kampeni ya kupambana na rushwa barabarani (UTATU)

Hilo tamasha usishangae wakisema ni mafanikio katika kupambana na rushwa. Sidhani kama kunahitajika tamasha katika kupambana na rushwa iliyo wazi, zaidi ya kuamua kupambana nayo kwa dhati.
Nimeona kama ni tafrija flani hivi imefanyika hapo.
 
Walipeni hawa askari pesa ya kueleweka; mtu anasimama barabarani kutwa nzima jua lake, mvua yake; kanikamata afu eti akatae msimbazi.... weee!!
 
Wewe inaelekea ni dereva mvunja sheria sugu. Siku zote lengo la faini ni ku-discourage mkosaji kutenda makosa. Ikiwa watashusha kiwango ina maana madereva watakuwa hawaogopi kutenda makosa. Kwanza jambo la kwanza la kukubali ni kuwa uendashaji wa magari barabarani wa Tanzania ni mbovu sana. Madereva hawajali kufuata sheria. Polisi wanatumia hii loophole ya uendeshaji mbaya kuchuma fedha. Tukirudi kwenye sheria za barabarani, ni kweli, kuna sheria nyingine zinakera. Jambo ambalo wanatakiwa kulifanya sambamba na huu uzinduzi ni kusikiliza maoni ya madereva na polisi ili kubadili sheria baadhi ya sheria. Watilie mkazo kwenye speed na vitu vinavyosababisha ajali mara kwa mara.
Hivi kupiga vita rushwa kulihitaji kufanya tafrija?Kuleta msanii a-perform?Sijui mpk Shekhe wa Mkoa kupiga sala.

Hakuna dhamira hapo ya kupambana na rushwa,kilichofanyika hapo ni sherehe kama zilivyo nyingine tu.
 
Wanaweza kudai ni kampeni ya awareness... kuwafanya watu wahamasike na kujua kuna kitu kipya kimeingia mjini. Kwangu mimi kitakachofanyika baada ya huu usinduzi ndicho kita-determine kama wamefeli au wameshinda. Madereva wote wajaribu kutoa ushirikiano tuone.
 
Kampeni za awareness ziko nchi hii miaka na miaka tangu inaitwa PCB mpk ikaja kuitwa PCCB.

Kwamba takukuru hawajui mali za matrafiki walizonazo?Na hawajui jamaa wamezipatje?

Ni kweli. Tatizo letu kubwa ni kuwa baada ya kuzindua mambo yanakuwa yameisha. Ni tatizo lililo kwenye kila sekta, kila mkoa na kila kichwa cha mtanzania. Kusahau mambo mapema. Wataalam wanasema wanyama kama manyani ndiyo walitakiwa wawe na tabia hii lakini nashangaa kwenye ni imekuwa ni binadamu badala!
 
Faini; kama nilivyotangulia kusema ni wachache wata-opt kulipa 30,000 badala ya 5,000 kumalizana na trafiki. Kuondoa tatizo hili, faini zipunguzwe - ziwe 5,000 kwa mfano hapo hutokaa usikie rushwa barabarani. TEHAMA inaweza kusaidia pia kwenye hili kwamba kwa mfano, ukionekana wewe ni sugu wa faini say ndani ya wiki moja umepigwa elfu tano tano mara 5 then automatically kwenye akaunti yako unaingiziwa bili ya 150,000 (mfano). Kwa utaratibu huu rushwa za barabarani kwisha badala ya kutumia nguvu nyiingi unnecessarily.
Yani wanahisi Trafiki ndio anayelazimisha kupewa rushwa wakati ni Dereva ndio anayelazimisha kuikimbia 30,000, Trafiki anachofanya ni kutengeneza mazingira tu!. Leo hii waweke faini 5,000 waone kama kuna trafiki ataota kitambi!.

Au kama vipi watengeneze mazingira wawafunge camera matrafiki wote!. Kila trafiki awe na Log yake kila akiingia kazini, Camera inakuwa ON na hatakiwi kuiziba plus camera iwe inarecord sauti pia!. Wenzetu wameweza mbona!.

Me siwezi mchoma trafiki atakayeniomba 5,000 ili asiniandikie 30,000, huo UTATU umekufa kabla hata ya kuanza kazi!..
 
... Mkuu wewe umenielewa na umefafanua vizuri sana nilichomaanisha. Thanks.
 
Kwa vile mkuu alishasema ni za kubrashia viatu basi bila shaka huo uzinduzi ni sawa na kupoteza muda tu
 
Wewe inaelekea ni dereva mvunja sheria sugu. Siku zote lengo la faini ni ku-discourage mkosaji kutenda makosa. Ikiwa watashusha kiwango ina maana madereva watakuwa hawaogopi kutenda makosa. Kwanza jambo la kwanza la kukubali ni kuwa uendashaji wa magari barabarani wa Tanzania ni mbovu sana. Madereva hawajali kufuata sheria. Polisi wanatumia hii loophole ya uendeshaji mbaya kuchuma fedha. Tukirudi kwenye sheria za barabarani, ni kweli, kuna sheria nyingine zinakera. Jambo ambalo wanatakiwa kulifanya sambamba na huu uzinduzi ni kusikiliza maoni ya madereva na polisi ili kubadili sheria baadhi ya sheria. Watilie mkazo kwenye speed na vitu vinavyosababisha ajali mara kwa mara.

Tena nafikiri faini ingekuwa mara 3 ya hiyo ili hata ukikosa unajilaumu na hutarudia tena kosa
Suala la kutoza faini kidogo maana yake unaendeleza makosa barabarani
 
Ni wananchi wangapi wataiamini hiyo TAKUKURU App na kuwa tayari kuipakua huku App yenyewe ikawataka watumiaji wa simu waridhie TAKUKURU wapate access kwenye simu zao na ku-manage contacts zilizomo, phone calls, picha, sms n.k.? Labda wasiojipenda maana karibia kila mkazi wa Tanzania ni mlaji na mpokeaji wa rushwa ila tu kiwango ndicho wanatofautiana.
 
Back
Top Bottom