Yaliyojiri kupatwa kwa Mwezi Usiku wa leo July 27-28,2018

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,914
23,079
Habari kutoka kwa wataalamu wa anga wanatushirikisha habari ya kupatwa kurefu kwa mwezi kwa karne hii ya ishirini na moja. Kupatwa huku kutatokea kati ya Ijumaa na Jumamosi wiki hii. Mabara yote yatashuhudia tukio hili isipokuwa bara Amerika ya kaskazini na Amerika ya kati. Watakao penda kufuatlia tukio hili watembelee channel ya 'timeanddate' siku hiyo inayopatikana youtube kwa jina hilo hilo i.e. timeanddate
RT.com

Sijui hii ndiyo ongeza baridi kwa kiasi hiki siku hizi hapa nchi? Wataalamu watatujuza kama hili linaambatana na baridi kali kwa nyakati hizi nchini Tanzania.

======

“Tukio la kupatwa kwa mwezi linatarajiwa kutokea leo ambapo nuru ya mwezi mkamilifu (full moon), itazuiwa na dunia hivyo mwezi kuonekana kuwa na rangi nyekundu katika kipindi cha saa kadhaa kuanzia saa 4:30 usiku hadi saa 6:14 usiku,”

Tukio hilo ambalo litachukua muda wa saa tatu mpaka kukamilika kwake ni la kwanza katika karne ya 21.


Habari zaidi...

Mnamo tarehe 27.07.2018 usiku, kunatarajiwa kuwepo kwa tukio kubwa duniani la Kupatwa kwa Mwezi, linalotarajiwa kuchukua muda wa saa moja na dakika 43. Kupatwa huko kutakuwa kwa Giza Totoro. Kupatwa kwa Mwezi huhusisha Dunia kuwa katikati ya Jua na Mwezi.

Chanzo cha kupata huko kuchukua muda mrefu, kunatokana na kwamba, Mwezi utakuwa katika eneo lake la mbali (farthest distance) la mzingo wake.

Wataalamu wanaeleza kuwa, kupatwa huko kwa muda mrefu ni matukio ya nadra ambapo tukio lingine litakalochukua muda mrefu, linatarajiwa kutokea miaka 107 ijayo, mwaka 2123, ambapo karibia wanadamu wote waliopo sasa, watakuwa hawapo tena duniani.

Kupata kwa Mwezi hakuna madhara ya kiafya, so watu wanaruhusiwa kuangalia tukio hilo bila kuhitaji miwani.
 
Last edited by a moderator:
tutembelee hiyo channel kufanya nini sa....wakati umesema kila bara litashuhudia...ama unaongea na na hao amerika ya kati na kaskaz
1.Mkuu wengine wanaweza wakawa wamebanwa ofisi..wasipate muda wa kutoka nje kushuhudia.
2. Channel hiyo ya youtube, itakuwa inatoa update namna kupatwa huko kwa mwezi kutakavyokuwa kunatokea maeneo mengine. Nadhani hii itakuwa ni nafasi muhimu kujua kinachondelea kwingine ulimwenguni.
 
labda mtoa anaongea na wana jf wenzake huko amerika akina nyani ngabu mana uzi wenyewe katoa usiku
tutembelee hiyo channel kufanya nini sa....wakati umesema kila bara litashuhudia...ama unaongea na na hao amerika ya kati na kaskaz
 
Wenzetu wa dhehebu jingine huwa wanadhani kupatwa kwa mwezi husababishwa na wakristo. Zamani ikitokea wakristo walikuwa wakisakwa na kulambwa mijeledi hasa maeneo ya Pwani
ha haha hahaa...ngoja wafia dini wenzako waje
 
Back
Top Bottom