Yaliyojiri kikao cha Rais Magufuli na Mawaziri, Makatibu Wakuu, MaRCs, MaRAS na TRA

Sio Tbc tu ata AZAM TWO Nao wako Live
TBC iko live ikionyesha Kikao Maalum kati ya Rais Magufuli na Uongozi wa TRA katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).



TRA: Uchumi unakua kwa asilimia 7% mwaka 2018 na itakua 7.3 mwaka 2019.

Chanzo kikuu cha uchangiaji wa ukuaji wa uchumi ni kama ifuatavyo:
  • Uzalishaji viwandani - 12.1%
  • Ujenzi - 11%
  • Malazi na huduma za chakula - 10%
  • Biashara - 9.5%
Mfumko wa bei Tanzania umeshuka kutoka asilimia 12.1% mwaka 2008 hadi asilimia 3.5% mwaka 2018.

Kulingana na TRA, bidhaa zinazopimwa kwenye mfumko wa bei kwa kila tarehe 8 ya kila mwezi, ni bidhaa 278, ambapo kati ya hizo, 181 ni bidhaa za vyakula.

Gavana wa Benki Kuu, ameelezea juu ya hatua ya Serikali kudhibiti uendeshaji wa Bureau-de-Change ili kubakia na zile zinazojiendesha kihalali. Alisema Dar es Salaam haihitaji kuwa na Bureau-de-Change 100 kwani kuna Benki nyingi.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga amesema kuna benki 55 zilizopo jijini Dar es Salaam, ambazo zina tawi moja moja tu, jambo ambalo halikubaliki. Ameeleza kuwa, BoT imeanza mchakato ya kudhibiti hilo, na kuhakikisha riba kwa wakopaji zinashuka.

Rais John Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu aandike barua ya kumpongeza Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Msafiri Mbibo baada ya kukataa kupokea rushwa kiasi cha Dola 2,000.

Fikiria nchi ya Tanzania yenye idadi ya watu takribani milioni 55, walipa kodi ni milioni 2.2 ambapo uwiano wa kodi kwa GDP ni asiliamia 12.8. - Rais Magufuli.

Katika makadirio ya kodi ya nyumba, wapo wanaokadiriwa hadi Sh. Milioni 2 au Sh. Milioni 3. Nyinyi wakuu wa Mikoa ni mashahidi, mtu amejenga nyumba kwa gharama halafu mnatoza kodi hizo, halafu hata bomba la maji hamjaleta. Rais Magufuli.

Kwenye suala la ukusanyaji mapato hatufanyi vizuri, japokuwa uchumi wa nchi unakwenda vizuri, mfumuko wa bei pia umepungua. Ikiwa Msumbiji wako milioni 27 na walipa kodi ni milioni 3.3, sisi tuko milioni 55 lakini walipa kodi ni milioni 2.2. - Rais Magufuli.

TRA tumeshindwa hata kurasimisha Sekta ambayo si rasmi ambayo ni asilimia 70, tunakusanya kwenye Sekta rasmi ambayo ni asilimia 30 pekee, tunashindwa kukusanya mapato kwenye Sekta isiyo rasmi, niseme ukweli hatufanyi vizuri kabisa. - Rais Magufuli.

"Tumeshindwa kurasimisha sekta isiyo rasmi ambayo inafikia asilimia 70, na sasa tunakusanya kodi kwenye sekta rasmi tu ambayo ni kati ya asilimia 30 hadi 40. Kati ya Watanzania milioni 55, ni Watanzania milioni 2 tu wanaolipa kodi."

"Uchumi unakuwa vizuri, mfumuko wa bei uko vizuri, lakini kwenye ukusanyaji wa mapato 'we are very poor'."

"Licha ya kuwa tumeongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni 800 hadi shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi, bado hatutakiwi kujipongeza."

Rais Magufuli ameiagiza TRA na Wizara ya Fedha kutoza kodi ya nyumba ya TZS 10,000 kwa nyumba za kawaida, TZS 20,000 kwa nyumba za ghorofa zilizopo wilayani na vijijini na 50,000 kwa nyumba kubwa. Na utozaji huo uzingatie hati ya kiwanja na sio idadi ya nyumba kwenye kiwanja.

"Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kiwango kikubwa cha kodi, hasa kodi ya majengo. Na hili linasababisha watu wengi kutolipa kodi na serikali kukosa mapato. Wekeni kodi za wastani ambazo wananchi watakuwa tayari kulipa"

"Kumekuwepo na tatizo la ukwepaji kodi ambapo baadhi ya makampuni yamekuwa yakitangaza kupata hasara ili kukwepa kulipa kodi. Kama kampuni inapata hasara kila mwaka, si ifungwe! Sisi hatutaki wawekezaji wanaopata hasara, hao kazi imewashinda."

"Kumekuwepo na tatizo la kubambikizia watu kodi kupitia mfumo wa kukadiria kodi. Mtu ana biashara ndogo, anakadiriwa kodi kubwa, mwisho wa siku mtu anafunga biashara yake, sasa hapo TRA mmepata faida au hasara? Wengine hufunga biashara na kwenda kufungua upya."

"Mazingira ya kufanyia biashara nchini bado ni tatizo. Usafirishaji, utitiri wa taasisi za usimamizi, ucheleweshaji bandarini, tatizo la umeme, kutumia muda mrefu kupata vibali vya biashara. Pia tumekuwa hatufanyi vizuri katika kuvutia wawekezaji."- Rais Dkt Magufuli

"Taratibu za kodi zikiwa rahisi na viwango vya kodi vikiwa chini, watu wengi watakuwa tayari kulipa kodi na hivyo serikali itapata mapato stahiki."- Rais Dkt Magufuli

"Najua wapo Watanzania wanaona fahari kukwepa kodi. Naiomba TRA mtoe elimu, muwape adhabu wakwepa kodi, lakini msiwaonee. Iwe ni aibu kwa Matanzania kukwepa kodi. Lakini haya hayakwenda sambamba na upunguzwaji wa viwango vya kodi."- Rais

"Watu wamekuwa wakikwepa kodi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tarafa wote mpo. Wakati mwingine naonaga kidogo kwenye TV mmekamata watu, ila najua ile mnafanyajaga kujitangaza kuwa mpo, baada ya muda hali inarudi ile ile."-

"Kuna mfanyabiashara kule Mwanza yeye halipagi kodi na anapitisha magari hata kumi kwa siku moja. Kuna wafanyabiashara wengine wawili wao wanaletaga makontena hadi 700 Kariakoo kwa mwaka. Wakileta wao ndio wanawauzia wengine. Nashangaa TRA, RC Dar hamuwajui."- Rais Dkt Magufuli

"Gavana wa BoT ameeleza hapa, alipovamia maduka ya kubadilishia fedha Arusha, alikuta maduka 37 hayana leseni, huku mengine yakifanya biashara bila hata TRA wenyewe kujua na serikali haipati hata shilingi 10."

"Tatizo lako Kichere (Kamishna Mkuu wa TRA), mtu anakosea hapa, unamtoa unampeleka pale. Hatutaki kubembelezana, ifike mahali mtu akipewa kazi ya kukusanya kodi ya nchi, akikosea, aondolewe. Menaja wa TRA Kilimanjaro yule anastahili 'promotion' awe mtu mkubwa."- Rais Magufuli

"Kuna Wafanyabiashara wanatetewa na wanasiasa, eti ni mchangiaji mzuri wa chama, mimi kama Mwenyekiti wa CCM Taifa nasema kamata, suala la kukusanya kodi halina chama, uwe CCM, CHADEMA, CUF ni lazima ulipe kodi, tufike mahali tujenge nchi yetu kwa kodi."- Rais Dkt Magufuli

Rais Magufuli: Nimeamua kufanya tofauti, nimetengeneza vitambulisho mimi mwenyewe ‬

‪> Kwa vile nimevitoa mimi sioni mtu wa kwenda kumsumbua mfanyabiashara yeyote atakayekivaa‬

‪> Nampa kila Mkuu wa Mkoa leo vitambulisho 25,000; jumla viko 670,000‬

‪#JFLeo
Rais Magufuli: Mfanyabiashara mdogo mwenye mtaji chini ya milioni 4 akiwa na kitambulisho hiki sitaki TRA, Halmashauri wala Mgambo kuwasumbua‬

‪> Nawapa tu onyo msije mkachukua bidhaa za wafanyabiashara wakubwa mkawa mnawauzia ili wakwepe kodi‬

‪#JFLeo

Rais Magufuli: Nimeamua kufanya tofauti, nimetengeneza vitambulisho mimi mwenyewe ‬

‪> Kwa vile nimevitoa mimi sioni mtu wa kwenda kumsumbua mfanyabiashara yeyote atakayekivaa‬

‪> Nampa kila Mkuu wa Mkoa leo vitambulisho 25,000; jumla viko 670,000‬

‪#JFLeo

Rais Magufuli: Kitambulisho kimoja ni shilingi 20,000 hivyo kwa vitambulisho 25000 itakuwa jumla ya shilingi 500,000,000 na ipelekwe TRA ili wasije sema ni mradi wangu wakati mimi ni facilitator tu‬

‪> Waambieni wasaidizi wenu wasiviuzae kwa bei zaidi ya hii iliyopangwa‬

‪#JFLeo

''TRA hakikisheni mnatoa adhabu kwa wakwepa kodi, ilimradi msiwaonee, hilo litafanikiwa tu endapo mtashusha viwango vya kodi".Rais Magufuli.

"Taifa linalokusanya kodi ndio taifa huru, huwezi kuwa huru usipojitegemea, kila siku utakuwa unaenda kupiga magoti".Rais Magufuli.
 
Mh.kaacha kusoma..

mamalishe,machinga...wapewe vitambulisho.

'Presidaa kachapisha vitambulisho vya ujasiriamali,kwa wajasiriamali tena bure...'

'Watachangia tsh 20,000/= jumla ya vitambulisho 670,000
20,000 x 670,000= 13,400,000,000

Kwa kifupi:
Itakusanywa Billion 13.4 za kitanzania
 
Mheshimiwa Rais, je Umetua Tanzania Jana au leo? Mbona kujifanya Mwema kipindi hiki kuelekea Mwaka Mpya? Unaonaje Sasa ukakiri makosa uliyoyafanya? Maana naona unarudi kwa mgongo wa kulaumu na wewe ilihali haya yamekuwa yakipigiwa kelele na WATETEZI HALISI wa Watanzania! KUWALAUMU TRA ni kujiosha Muheshimiwa, kulalamika kupungua kwa walipa Kodi ama kutokuongezeka kwa idadi ya walipakodi Ni matokeo ya misingi MIBOVU uliyoanza nayo. Hakuna Kati ya unavyovilalamikia ambavyo hukuviasisi. Leo Biashara zimekufa nyingi, Leo baadhi ya Investors wanapoteza muda Rumande kwa Amri za DCs wako bila kujua hao ndio wanaotunisha chungu chako, wengine wamefunga na kuhamisha Biashara, umeteua watu kwa mihemuko katika Sekta za kimkakati badala ya kuteua watu wa kimkakati katika Sekta za Kimkakati mf. Unamweka Kigwangala katika Wizara ya Maliasili na Utalii huku kazi yake kuonesha utupu wa Akili Yake mtandaoni, just to remind you, Tanzania is a Big Family compared to your own family.

Spinning Doctors wako bado hawana weledi katika haya unayotuambia Sasa, huku Ni kuvaa ngozi ya Kondoo ilihali wewe sii mmoja wao. Wema wako kwa Watanzania uonesha kwa kuliunganisha Taifa, kubali kuambiwa hata Kama unayoambiwa yanakuumiza, accept n recognize michango hata Kama Ni ya maadui zako, LIUNGANISHE TAIFA BABA, acha UBAGUZI, acha KUWADHARAU NA KUWATWEZA WENGINE, zingatia ushauri wa KAKOBE na Viongozi wengine wa Dini!

Nimeona nami niseme, Kama nimekosea, tuvumiliane, tuelekezane, TUIJENGE TANZANIA!
Umenena yaliyo moyoni.

Baba wa Taifa alitafsiri Maendeleo kuwa ni WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Moja ya hayo yasipokuwa kuwa sawa, hakika maendeleo hayatapatikana. Kwa jinsi hiyo jipime wewe unaangukia wapi kabla ya kutoa lawama kwa watu wengine.

Kuna haja ya mimi, wewe na yeye tuliopewa madaraka (cheo ni dhamana) tutimize wajibu wetu ili mwisho wa siku tujue nani anakwamisha juhudi za kuendeleza Taifa hili.
 
NIDA wajitathinini, Magufuli vitambulisho vya machinga katengeneza ndani ya miezi kadha.... halafu Nida zaidi ya miaka kumi vitambulisho vya Taifa wanaandikishaga tu.

Hiyo kazi wamwachie Magufuli mwenyewe sasa.!
Dah mkuu hadi nimechoka kabisa. Yaan una uelewa finyu sana tena sana... ss hao NIDA wanatengeneza kitambulisho kupitia taarifa zako sahihi za makazi, majina nk.. lkn hivi ni kama vitambulisho vya visitors katika organization yoyote ile havina alama yoyote kukutambua kwa jina just an identification ya uwepo wako tu...
 
Uchumi ungekua mzuri tusingeshindwa kufanya sherehe kuazimisha miaka 57 ya Uhuru. Hiyo miradi ya maendeleo haitaisha ikiwa taifa lipo hai.
 
''Bureau de change 37 na zote zinatumia leseni 1...na tra hawana data..''
Sasa mbona meneja wa TRA wa mkoa wenye hizo hizo bureaux de change kapongezwa na rais kwa kukataa hongo ya $2,000? Ina maana muda wote huo meneja huyo alikuwa hajagundua kwamba hao wafanya biashara wanatumia leseni moja?
 
HAKIKA TUKO VIZURI

"Mfumko wa bei Tanzania umeshuka kutoka asilimia 12.1% mwaka 2008 hadi asilimia 3.5% mwaka 2018."

Hilo hapo ni kweli kabisa,

Mfano:
Sukar ilkua 5,000 mwaka 2008,

Hivi sasa mwaka 2018 iko 2,300

##UzalendoKwanza##
MEMBE FOR PRESDENTIAL 2020
 
MEMBE FOR PRESDENTIAL 2020
FB_IMG_1544435557210.jpg
 
Back
Top Bottom