Yaliyojiri kesi ya Mbowe 24/01/2022: Shahidi wa 11, H4347 Goodluck amaliza ushahidi wake. Shahidi wa 12 kuendelea tarehe 26/01/2022

CCM ni watu wabaya saana ndugu; kumtesa mbowe hivi kisa KATIBA MPYA.
CCM ya Serikali na Rais/serikali ya CCM ni hatari kwa ustawi wa Tanzania ya Tanganyika na Zanzibar.
Mikanganyiko na michongo yote ni mali ya CCM,kwa kesi hii wamelikoroga mazima.Sifahamu kwa nini wanaendelea kuwatesa Mh.Mbowe na wenzake,wakitumia gharama kubwa sana.
Sasa hivi wanatumika kuanza kupotosha kuwa eti viongozi wa CDM wanalipwa mamilioni ya fedha kuhudhuria kesi ya Mwenyekiti!
Salama yetu ni Katiba mpya tu.
 
Shahidi wa leo aligeuka akawa shahidi wa utetezi. Yani yeye Ni mpelelezi na anadai kwamba hajawahi kupata taarifa za mpango wa kutenda ugaidi. Hivyo basi inawezekana kosa la ugaidi limtengenezwa baadae baada ya watuhumiwa kukmatwa.
Na aliponitisha zaidi ni pale alipoulizwa kama katika task force yao Kingai ana taarifa tofauti na wengine, akathibitisha kuwa wote wako na taarifa zote pamoja. Kesi hii ni ngumu upande wa Jamhuri. Unakamata madawa ya kulevya halafu hayawi sehemu ya kidhibiti mahakamani, haiko katika certificate of seizure, wala haipelekwi maabara kuleta majibu kama ni madawa kweli au la. Jana nimetambua haya:
a) Kesi ya ugaidi iliwahusu washitakiwa wote isipokuwa Mbowe. Mbowe aliingizwa baadae sana baada ya kuona aliwasiliana nao wakati wa upelelezi dhidi ya makomandoo. Ref: wale makomandoo wengine walioshitakiwa na kuachiwa huru. Huenda upepelezi wa makomandoo ulihusiana na ugaidi kusini mwa nchi.
b) A5340 ilipandikizwa pamoja na risasi tatu na madawa. Mbili kati ya risasi zilizopandikizwa hazikuwa 9mm kwa hiyo zisingeletwa mahakamani (Ref: risasi mbili kutumika katika majaribio ya kupima silaha na kufanya risasi moja tu kuletwa). Mchanganyiko wa Luger CZ100 na A5340 ni wa ajabu kidogo kwa askari ambao katika jeshi la polisi wanaweza kuchukuliwa ni wasomi.
c) Kukosekana kwa ushahidi wa upangaji wa ugaidi kupitia voice au text messages au planted/underscover operative ni udhaifu mkubwa sana katika kesi hii. Confession ya mtuhumiwa lazima iwe backed up na ushahidii coz ushahidi unapaswa kuonesha kosa hata pale panapokuwa hakuna hiyo confession!!

Labda Urio ana ushahidi mzuri zaidi, ngoja tusubiri!!
 
Sijawahi ona mada ya kesi ya kipuuzi kama hii.mods ficheni upumbavu wenu kwa kufutilia mbali huu upuuzi unajaza server tu.
 
Hii nchi bhana!

Kwa mkanyiko huu , Acheni mahakama ione kama kuna hatia au hakuna Hatia.
 
Tunashukuru kwa kazi hii ya kutuhabarisha kwa ufasaha.imekaa kama umeleta vyote kwa ufasaha.Ila najifunza sana mambo ya kubambikia watu kitu ni kazi kubwa sana.Na mahakama ni sehemu muhimu sana.maana vitu vinawekwa wazinkabisa.ukiwasikia polisi wanapotoa taarifa kwenyr vyombo vya habari unaweza wachukia watuhumiwa right away,kumbe mambo mengi yanakuwa yamepotoshwa.

Ila lile neno linalosema "patana na mdai wako kabla hajakufikisha kwa kadhi......" sababu kwa kadhi shughuli ni kubwa sana.nadhani kuna mashaidi wengine wanajuta kuingia katika kesi hii.maana kuna elements za kujidhalilisha
Na ndio maana mashahidi wanasua Sua kufika mahakamani Ni pamoto kzimbn
 
Na aliponitisha zaidi ni pale alipoulizwa kama katika task force yao Kingai ana taarifa tofauti na wengine, akathibitisha kuwa wote wako na taarifa zote pamoja. Kesi hii ni ngumu upande wa Jamhuri. Unakamata madawa ya kulevya halafu hayawi sehemu ya kidhibiti mahakamani, haiko katika certificate of seizure, wala haipelekwi maabara kuleta majibu kama ni madawa kweli au la. Jana nimetambua haya:
a) Kesi ya ugaidi iliwahusu washitakiwa wote isipokuwa Mbowe. Mbowe aliingizwa baadae sana baada ya kuona aliwasiliana nao wakti wa upelelezi dhidi ya makomandoo. Ref: wale makomandoo wengine walioshitakiwa na kuachiwa huru.
b) A5340 ilipandikizwa pamoja na risasi tatu na madawa. Mbili kati ya risasi zilizopandikizwa hazikuwa 9mm kwa hiyo zisingelewa mahakamani (Ref: risasi mbili kutomika katika majaribio ya kupima silaha na kufanya risasi moja tu kuletwa). Mchanganyiko wa Luger CZ100 na A5340 ni wa ajabu kidogo kwa askari ambao katika jeshi la polisi wanaweza kuchukuliwa ni wasomi.
c) Kukosekana kwa ushahidi wa upangaji wa ugaidi kupitia voice au text messages au planted/underscover operative ni udhaifu mkubwa sana katika kesi hii. Confession ya mtuhumiwa lazima iwe backed up na ushahidii coz ushahidi unapaswa kuonesha kosa hata pale panapokuwa hakuna hiyo confession!!

Labda Urio ana ushahidi mzuri zaidi, ngoja tusubiri!!
Kwa Jaji huyu wa mchongo atafukia kwamba shahidi hajasema hivyo
Fuatilia kunasehemu shahidi alisema tulikamata madawa ya kulevya Jaji akasema walikamata yanayo hisiwa madawa ya kulevya Kibatali akamjibu Jaji isiwe shida ibaki hivyo hivyo

Fuatilieni huyu Jaji ni mburura sana
 
Kalala na mkewe nyumbani usiku wa kuamkia leo- wala sina shida na hilo- ila kuchakachua UPDATES ambazo ni kihererere chake kuzileta humu- public Sphere -HAIKUBALIKI
Una ushahidi kuthibitisha Hilo au unabwata tu.
 
Back
Top Bottom