Wadau, amani iwe kwenu.
Nina kila sababu kumshukuru Mungu Rabuka, kwa kusikiliza kilio chetu. Hakika mimi pamoja na wadau wengine humu tulianzisha mapambano ambayo kwa hakika yalikuwa magumu sana kwetu. Uzalendo wetu ndio ulituunganisha humu. Tulishikamana na tulitiana moyo ijapokuwa tulijua kuwa tuna kazi kubwa mbele yetu. Wapo waliotubeza humu kuwa tunapoteza muda bure kupambana na mtu mwenye pesa na mamlaka. Wapo waliosema kuwa tunatumika na baadhi ya wagombea. Wapo pia waliosema kuwa hakuna anayetusikiliza humu. Wapo pia waliobeza yale tuliyokuwa tunaandika huku wakituambia kuwa sisi ni wazushi. Hakika tulikumbana na misukisuko mikubwa sana. Wengi tumepigwa ban mpaka za mwezi lakini baada ya kifungo tuliendelea na mapambano hadi kimeeleweka.
Wadau, unapomuua nyani hutakiwi kumuangalia usoni. Ndivyo nilivyofanya pamoja na wadau wengine kama akina Simiyu Yetu, TataMadiba, Emma, kanone, Weston Songoro, Chabruma nk. Hatukumuangalia usoni Lowasa pale tulipobainisha mipango yake ovu. Tuliweka bayana pale alipogawa fedha kwa viongozi wa dini ili aungwe mkono. Tulieleza waziwazi jitihada za Apson Mwang'onda kuhakikisha kuwa fisadi Lowasa anaenda Ikulu. Mipango yake ovu hiyo ilibainishwa huku tukipata kwa urahisi taarifa ovu za Team Lowasa.
Wengi wetu humu hatukuwa na uhakika kama Lowasa atakatwa. Hii ni kwa sababu jamaa ana fedha nyingi na alijaribu kuhonga kila mtu aliyoeona kuwa ana maslahi kwake. Ila ameshindwa kutuhonga humu kutokana na utaratibu mzuri wa JF wa kulinda watoa habari. Lowasa hakuwa na namna ya kutufikia members humu. Alikuwa na mamlaka tu ya kuagiza mods watupige ban. Ila hiyo haikutukatisha tamaa. Pale tulipoanguka tulisimama tena na kuendelea na safari na sasa tumefika kileleni kwa furaha kubwa sana. Fisadi kakatwa. Jeuri ya fedha haijamsaidia. Mataikun waliomzunguka hawajamsaidia. Watu vichwa maji waliomzumguka hawajamsaidia.
Baada ya kuhakikisha kuwa CCM hakihodhiwi na mafisadi, sasa ni muhimu wana CCM tukashikamana kwani Umoja ni Ushindi. Kwa kitambo kidogo tuliwaweka pembeni mahasimu wetu, UKAWA. Tunarejea kwa kishindo. UKAWA kaeni chonjo. Mapigo yale yaliyowasambaratisha akina Slaa yanakuja tena kwa kasi ya hali ya juu. Naamini kuwa watu tuliofarakana kimawazo kama Ritz, MUSSA ALLAN, Minyoo, Funza, Ocampo four, Pasco nk tutakuwa pamoja tena katika mapambano dhidi ya adui yetu mkuu.
Mwisho niwaombe radhi wale niliowakwaza kwa namna moja ama nyingine. Mkumbuke kuwa si makusudi yangu kuwakwaza bali ni katika jitihada za kupambana na mafisadi. Baada ya ushindi huu, Naamini kuwa tutaendelea kuwa pamoja ili kuhakikisha kuwa CCM inashinda kwa kishindo ifikapo Oktoba.