Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,550
- 220,291
Tunafuatilia kwa karibu sana mkuu , Naona Molemo Media iko kazini , safi sana kamandaView attachment 1576775
Mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuingia kwa kishindo kikubwa mjini Bukoba.
Mji wa Bukoba ambao ni ngome Kuu ya Chadema unatarajiwa kuzizima Leo wakati shujaa huyo atakapokanyaga viunga vya mji huo.
Mgombea Ubunge wa Bukoba Mjini mwenye ushawishi mkubwa Chief Kalumuna amewaalika wananchi wote wa Bukoba kumlaki na kumsindikiza kwa maandamano makubwa mgombea huyo wa Urais atakapowasili Hadi katika viwanja vya Gymkhana.
Wachunguzi wa siasa za Bukoba wanasema huenda Leo mji wa Bukoba ukavunja Rekodi ya Mapokezi iliyowekwa na miji ya Tunduma, Mbeya na Mwanza.
Mpaka Sasa kila dalili zinaonyesha mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu ana Uhakika wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 60%
Kabla ya kuingia Bukoba Mjini Lissu atahutubia mikutano katika miji ya Karagwe na Misenyi