Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Katika Mapokezi na Mkutano Mkubwa wa hadhara wa Tundu Lissu Mjini Bukoba

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
IMG-20200922-WA0003.jpg
Mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuingia kwa kishindo kikubwa mjini Bukoba.

Mji wa Bukoba ambao ni ngome Kuu ya Chadema unatarajiwa kuzizima Leo wakati shujaa huyo atakapokanyaga viunga vya mji huo.

Mgombea Ubunge wa Bukoba Mjini mwenye ushawishi mkubwa Chief Kalumuna amewaalika wananchi wote wa Bukoba kumlaki na kumsindikiza kwa maandamano makubwa mgombea huyo wa Urais atakapowasili Hadi katika viwanja vya Gymkhana.

Wachunguzi wa siasa za Bukoba wanasema huenda Leo mji wa Bukoba ukavunja Rekodi ya Mapokezi iliyowekwa na miji ya Tunduma, Mbeya na Mwanza.

Mpaka Sasa kila dalili zinaonyesha mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu ana Uhakika wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 60%

Kabla ya kuingia Bukoba Mjini Lissu atahutubia mikutano katika miji ya Karagwe na Misenyi

Yaliyojiri
Kama ilivyotarajiwa Lissu amewasili Bukoba Mjini majors ya saa 10 jioni na kulakiwa na umati mkubwa wa watu waliojipanga majiani huku msafara ikiongozwa na bodaboda zaidi ya Mia tano.

Akihutubia halaiki hiyo ya watu Lissu kwa maneno yake mwenyewe amesema kwa Sasa Bukoba ndiyo inayoshikilia Rekodi ya Mapokezi.

Pamoja na mambo mengine kwa Mara nyingine Lissu amelaani vikali sheria Kandamizi ya Mafao ya wastaafu inayozuia Fao la Kujitoa na kupunguza Mafao ya Wafanyakazi maskini wanapostaafu.

Lissu amesema ole wao Wafanyakazi wakiichagua CCM kwani Sheria hii iliyojaa hila na uovu ilaanza kutumiia mwakani.

Lissu ameahidi Wafanyakazi kufutilia mbali sheria hii isiyojali Haki za watu endapo wananchi wakimchagua kuwa Rais wao.

Sehemu ya Hotuba ya Tundu Lissu

"Bukoba Wakorawaituuuuu..."

Rekodi rekodi ya Bukoba Sasa, Nawashukuru sana watu wa Bukoba kwa yote...

Ngoja niwaambieni maana ya uchaguzi mkuu huu, imeandikwa kuwa "Wenye Haki Akiongoza Amani Utawala." na "Muovu Akitawala Watu Huugua." sasa uchaguzi mkuu huu tunanafasi yakuendelea kuruhusu Muovu atawale au wenye haki wafurahi.. Kipindi cha miaka mitano hii tumetawaliwa na viongozi wa ajabu Sana, Magufuli amekuwa muovu sana ndo maana akala rambirambi, tumetawaliwa na muovu ndo maana Wavuvi wanaugua, tumetawaliwa na muovu ndo maana wakulima wanaumwa. Watu wa Kagera mmefanyiwa uovu na Magufuli, raisi raisi ukiacha vtu vyake binafsi vitu vingine vyote Ni mali ya wananchi.. Tuna utaratibu wa majanga, kuna Sheria Ya Majanga chini ya Ofisi Ya Waziri mkuu, kwahyo Watanzania mnahaki yakupata msaada nasio kwa mapenzi yake. Nawapongeza watu Bukoba mnajielewa, alipokuja hapa juzi mkamzomea licha yakuleta watoto wa shule.. Kwa mara Ya kwanza TBC wakamzimia kwa sababu watu Walikuwa wanamzomea. Kagera mnanifurahia toka nimefika sababu mtu wa haki amewafikia.

Sasa watu wa Bukoba naombeni dhamana yakunichagua hyo tarehe 28 mkinichagua nitawatendea haki. Uwe Askari, Mwalimu, Mfanyabiashara, Mvuvi, Wakulima wote Serikali ya Chadema itawatendea haki. Sababu tumesema kwenye ilani Yetu. Uwe boda boda, uwe mama Ntilie wote nitawatendea haki.

Kingine nyie Askarii na wafanyakazi wote kuhusu Sheria kikokotoo Kipya kianze kutumika 2021 cha makato, kwamba utapata nusu ya mafao yako. Sasa Nyie Maaskari mkiambiwa mtupige ila mjue mkistaafu Nusu ya mafao yako yamekwenda na maji. Sasa tarehe 28 twendeni tukamtoe, alipoingia madarakani alisema anakataa ufisadi lakini Karagwe huko Magufuli amechukua Hector 25,000 kwa wananchi. Sasa kwakuwa tumekugundua nakwambia Magufuli rudisha ardhi ya watu.

Watu wa Kagera mnasumbuliwa na uraia wenu, mkoa mzima NIDA imekuwa shida. Watu wa Kagera mkisema kidogo tu mnahojiwa kuhusu uraia wenu. Mnakumbuka maaskofu walitoa waraka wa Pasaka, Magufuli akawatuma watu wa uhamiaji kumzonga Faza Sabaa wa pale Kasulu. Nawaombeni watu wa Bukoba muulizeni Askofu wenu kwanini Magufuli anawazonga zonga Maaskofu, Kanisa ina kauli gani kuhusu huyu mkandamizaji wa wananchi. Kakobe aliposema kidogo akatishwa akaambiwa athibitishe uraia wake kesho yake Askofu Kakobe akasema Magufuli ni mtu wa Mungu. Sasa Raisi anayewanyanyasa watu dini hafai kuwa raisi. Sio Maaskofu tu hata Masheikh wako magerezani kwa kesi za ugaidi na hawajafanya ugaidi wowote. Nauliza Watanzania mnampango gani nae, Chadema na wananchi tuungane tukatae kuongozwa na mtu mtu anayenyanyasa viongoz wakidini. Magufuli amesababisha wafanyabiashara wafilisike..

Wakati Magufuli anachukua uraisi Kahawa ilikuwa 2500, Sasahivi imeshuka mpaka 1200, wakati sukari ilikuwa 1200 Sasahivi 3000.

Sasa raisi wa Tanzania anapigiwa kura, kinyago tulichokichonga wenyewe hakitutishi lazima tukifanye kuni. Uchaguzi twendeni tukampumzishe, maana raisi anayetumia pesa za wananchi kujijengea uwanja wa ndege nyumbani kwake. Unaenda hospital unakosa dawa pesa zimeenda kujenga uwanja ndege. Watoto wanakaa chini shule kisa pesa zimejenga uwanja kwao. Nimesema mengi ananijibu ila hili la uwanja ametulia tuli.

Sasa tarehe 28 tukapige kura nakumuondoa madarakani na chama chake. Sasa nasikia hatutangazwa, Magufuli sasa hauna jeshi lakutuzuia tusitangazwe. Magufuli tutakushinda kuanzia Bukoba na Kagera na mpaka nchi nzima. Na akiaribu uchaguz huu atajikuta yuko the Hegue. Sasa tupige kura na tushinde kwa kishindo tukishinda kwa kishindo hawataiba kura, Chagua *Chief Kalumuna* kwaubunge wa Bukoba mjini, chagueni Madiwani wote wa Chadema na huo ndo mpango na yule diwani wa Cuf. Na Bukoba Kijijini ni *Bi Konchesta.'* na madiwani wake. Nchi nzima diwani Chadema na Madiwani Chadema, kwenye uraisi nihivi wasiempenda kaja, ama zangu ama jiwe..

Nawashukuru sana watu wa Bukoba, Mungu awabariki sana.








 
Huyo ndo Rais wa kweli atakayeleta maendeleo ya kweli, achana na Meko ambaye kwa sasa anafanya kazi ya kujitetea tu majukwaani.

Mara ooh, vitambulisho vya machinga sio lazima, mara ooh, serikali ya majimbo italeta umaskini, mara ooh, uwanja wa ndege wa Chato haujajengwa Rwanda.

Yaani kwa sasa hata ilani yao ameamua kuiweka kando. Atakufa kwa pressure huyu dikteta.
 
Nashangaa kwa nini hajadekiwa barabara kama ilivyokuwa kwa Lowassa!

Uzuri wa siasa za upinzani Tanzania, wagombea Urais huingia kwenye uchaguzi kwa mbwebwe na baada ya uchaguzi huanza kupotea polepole!

Tanzania kuna vituko!
 
Lissu anakamilisha ratiba huko kanda ya ziwa hana chake, mdomo wake umemponza. Anachukia meli,treni,daraja la busisi nk. kwa kifupi ngoja akatembee na uwepo wake unawaponza wagombea ubunge na udiwani kupitia chadema.
Kama namuona Lwakatare anavyochungulia kama panyabuku tunduni
Kila mmoja aliamini upinzani umekufa, mpaka watu na akili zao wakahamia NCCR Mageuzi baada ya kupata tetesi kuwa wana viti 20 vya bure na watakuwa KUB..... USALITI MTUPU, sasa kilichobaki ngoja waje wasalitiwe na wake zao maana nao hawastahili kutosalitiwa
 
Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu leo anatarajiwa kuingia kwa kishindo kikubwa mjini Bukoba.

Mji wa Bukoba ambao ni ngome Kuu ya CHADEMA unatarajiwa kuzizima leo wakati shujaa huyo atakapokanyaga viunga vya mji huo.

Mgombea Ubunge wa Bukoba Mjini mwenye ushawishi mkubwa, Chief Kalumuna amewaalika wananchi wote wa Bukoba kumlaki na kumsindikiza kwa maandamano makubwa mgombea huyo wa Urais atakapowasili Hadi katika viwanja vya Gymkhana.

Wachunguzi wa siasa za Bukoba wanasema huenda Leo mji wa Bukoba ukavunja Rekodi ya Mapokezi iliyowekwa na miji ya Tunduma, Mbeya na Mwanza.

Mpaka Sasa kila dalili zinaonyesha mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu ana Uhakika wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 60%

Kabla ya kuingia Bukoba Mjini Lissu atahutubia mikutano katika miji ya Karagwe na Misenyi
Asante sana Mkuu Molemo , kiukweli tungefaidi sana kama Watanzania tungepata fursa ya kushuhudia live kuputia TV, mikutano yote ya Tundu Lissu, kama tunavyo ishuhudia mikutano ya mgombea wetu Magufuli, ili Watanzania tuwapime tuamue tunamchagua nani!.

Nakumbuka hili niliwahi kushauri Chadema lakini hamsikii...
Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...
Nilisema
Wanabodi,
Sasa ili kuwafikia Watanzania wote na kuwaamsha waliolala, Chadema haiwezi kuwafikia Watanzania wote kwa kutegemea mikutano ya hadhara na mass media za wengine. Chadema lazima wawe na mass media yake ambayo ita propagate the message of changing the mindset ya Watanzania. Chadema wana all the resource kumiliki media yake lakini very unfortunately they are myopic, hawana vision ya kuona mbali kuangalia nje ya box and see a bigger picture. Hawajui kupanga priorities zao. Bei ya gari moja tuu la M4C linatosha kununua transmitter ya Digital ya redio na TV. Chadema bila media yake, ni kutwanga maji kwenye kinu, CCM ina media yake na TV yake TBCCM, radio zake na magazeti yake, Chadema bila media yake, ikulu wataendelea kuisikia tuu kwenye bomba, 2015 ni CCM tena! .

Wasalaam.

Paskali

NB. Paskali, sasa ni mwanachama, mfuasi na mshabiki wa chama fulani cha siasa, in fact ni kada!. Lakini ni kada Mzalendo mwenye kutanguliza mbele utaifa na maslahi ya taifa ndio maana licha ya kuwa kada wa chama kingine bado anawashauri vyama vingine the right thing to do.
P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom