Yaliyojiri Jijini Mwanza: Freeman Mbowe akutana na vijana vyuo vikuu!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Kila kitu kiko sawa, ulinzi ni wa kutisha mpaka kwenye paa za nyumba. imenikumbusha ziara ya Obama! Vijana wana ari sijawahi kuona!

Update: Ukumbi umeshajaa na viongozi mbali mbali wamewasili tayari, na taarifa kamili ni kuwa kamanda atawasili ndani ya dakika kumi.

Update: Kamanda Mawazo anaingia anaingia anashangiliwa sana! anasalimiana na viongozi mbali mbali.

Kuna kijana anamwaga sumu anasema ni heri wajinga wasio hasara kuliko wasomi wasio na faida!

Uodates: Ameingia kamanda Kigaila akiongozana na katibu wa kanda Kabangila!

Updates: Kamanda Mbowe ndo anaingia sasa akiwa amelindwa kuliko siku zote kwa kweli Chadema wamejipanga.

Updates: Dr Kambangilia anatoa ufafanuzi kuwa mwenyekiti amekuja kuzindua kanda maalum ya vyuo vikuu. Anasema Ccm wamejifungia Mwanza hotel wakijaribu ku-copy mkakati wa chama!

Updates: Wenje anatoa taarifa kuwa jmanne kitaumana bungeni kwani kwani wanataka kujua haki iliyovunjwa ya meye wa Ilemela. Anasema yeye Zitto, Mdee na Mnyika ni product ya Mbowe

Updates: Mbowe anaanza hotuba yake akisema wakati wa TANU hakukuwa na computer za kupotosha umma kwenye mitandao.

Anatoa alivyoocha kazi na kukutana na Bob Makani na hakukumbuka jinsi walivyokuwa wote benki kuu.

Anasema alishinikiza Dr Slaa awe katibu mkuu wa chama na akashinikiza kufanya mabadiriko makubwa kabla ya kukubali kuwa mwenyekiti.

Anasema alimulipia nauli Kabuoru nauli toka Marekani na alipokuja alilipwa mshahara na yeye na Ndesemburo

Anatoa siri kwamba siri ya Chadema kutosimamisha wagombea urais, ni kwa sababu Makani na Mtei waligombania kugombea urais mwaka 1995 chama kikaamua kuwatosa!

Anasema wanaosema anataka uongozi ni mpuuzi na mmbea, kazi ya kuongoza chama hiki ni ngumu kwani kifungo ni chako, risasi ni zako na kufirisika!

Anasema ameshambuliwa Arusha kwa bomu la kivita, bunduki za kivita na bastora. Anayesema hatavumiliwa mtu yoyote anayetaka kutoboa mtungi uliyotengenezwa kwa miaka 25 mfululizo.

Anasema Chadema wana msiba Ccm wanalia kuliko Chadema wenyewe. Anasema Chadema iko imara na anayefikiria vinginevyo apime ataona!

Anasema atasimamia nidhamu kwa gharama yoyote. Anasema Mbowe hana kundi wala hana njaa! Hatuwezi kugombania vyeo wakati huu kwani wakipewa nchi watatoana meno.

Ametangaza kwamba chama kitafanya kazi kubwa ya kujenga chama kwa akina mama mwaka 2014. Amemaliza hotuba na anazindua kanda maalum ya vyuo vikuu.

 
!
!
duh!endelea kutujuza maana mpaka muda huu sijajua nisimame upande huu, nina uhakika nahitaji mabadiliko makubwa ila yatakuja kutokea upande upi ndio shida
 
tahadhari:: wale walio kinyume na mawazo yake waangalie sana wanaweza wasiuone mwaka mpya
 
Hivi Moshi,Arusha hakuna vyuo? mbona kwenye kumbukumbu zangu sijawahi kusikia Mbowe au Slaa akishirikisha vyuo vya huu ukanda katika siasa na maandamano?
 
Hivi Moshi,Arusha hakuna vyuo? mbona kwenye kumbukumbu zangu sijawahi kusikia Mbowe au Slaa akishirikisha vyuo vya huu ukanda katika siasa na maandamano?
Mkuu, huko hahitaji kufanya juhudi kuungwa mkono. Ndo nyumbani kwa CHADEMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…