Leo 31 Oktoba, 2014 kuanzia saa tatu kamili usiku CHADEMA itakuwa live ITV ikikuletea mapunduzi ya teknolojia kwenye siasa kwa kuzindua huduma 3 muhimu ambazo utakuwa na uwezo wa kuzipata na kuzitumia kupitia simu yako ya mkononi mahali popote ulipo. Huduma zitakazo zinduliwa leo.
1. E-Membership, hii itakuwa huduma ambayo mwanachama atakuwa na uwezo wa kujisajili mwenyewe kwenye mfumo maalumu wa kiteknolojia kwenye chama na kuweka taarifa zake kwa kutumia simu ya mkononi, ikiwa ni pamoja na kuweka picha na kupata taarifa kuhusiana na uwanachama wake.
2. Chadema media (chadema 3.0), hapa kupitia simu ya mkononi (aina yoyote) mwanachama, mpenzi au mfuasi atapata taarifa za motomoto kutoka kwenye vyanzo sahihi ndani ya chama kuhusu maswala mbalimbali yanayo husu chama. Atapata kujua ratiba ya matukio na mahali yanapofanyika, yapi yanatarajiwa na kwa wakati upi, kimsingi chadema media itakuwa moja ya vyanzo vikubwa vya taarifa/habari muhimu anazo paswa kuzipata mtanzania ili kuibua na kukuza ufahamu wake kwa maendeleo endelevu ya taifa letu.
3. Fundrising, hii itakuwa huduma ambayo kupitia simu ya mkononi, visa/master card na huduma nyingine za kibenk mwanachama, mfuasi au mpenzi wa chama atakuwa na uwezo wa kukichangia chama kiasi chochote cha fedha kwa namna anavyo ona ina mfaa akiwa ndani au nje ya nchi. Hupaswi kupanga kuikosa, ni kupitia kituo cha ITV kuanzia saa tatu usiku hadi saa tano kamili usiku matangazo ya moja kwa moja (Live) kutokea ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel.
Ungana na mamilioni ya watanzania watakao kuwa wanatazama ITV kwa muda huo, kuwa sehemu ya mabadiliko, wajulishe wengine nao wasipitwe maana siya kukosa.
Tumeanza na Mungu, tuko na Mungu na tutaendelea na Mungu.
Mpaka kieleweke.