Yaliyojiri Fiesta

Yaliyojiri Fiesta

wekeni na picha na cc wa mbali tujifaidie jamani mweh
 
sound mbovu! performance ya baadhi ya wasanii mbovu hwajajua kutumia jukwaa la vile hata sielewi! na umeme ndo umehribu kinoma noma yaan kiujumla ni mbaya!
 
Mlishndwa kuwadunda? Mtaibiwa khla siku na hao wafu fm. Mngeondoka hata na viatu vya madam mchovu au simu ya bibi twelve.
 
SERENGETI FIESTA MWAKA HUU 2013 NI NOUMA SANA,UMEME WAKATIKA GHAFLA,WASANII KIBAO HAWAJAFANYA SHOW WAKIWEMO NA WALE KUTOKA NJE YA TANZANIA.WATU WATIMUA BAADA YA KUONA LONGOLONGO NYINGI.

Usiku wa kuamkia leo pale leaders Club jijini Dar es Salaam Palikuwa hapatoshi kulikuwa na nyomi ya kufa mtu wakipata Raha za Fiesta ila Gafla Majira ya saa 10 usiku Umeme Ukazima gafla Wakati Ommy Dimpoz akiwa jukwaani na J.Martins kutoka Nigeria na kusababisha show hiyo iishie hapo.

Wengi Wamelalamika kwa Sababu Wasanii Wengi akiwemo Diamond,Chege,Temba,Madee,Afande Sele na Wengine Kibao hawajafanya show Wakati walikuepo kwa Ratiba.

Kama Vile haitoshi hata Msanii kutoka Sweden Mahombi hajafanikiwa kufanya show.Watu wamesubiri mpaka saa 11 alfajiri hatimaye wakakata tamaa na kuanza kuondoka huku lawama nyingi zikienda kwa Waandaaji kwa kutojipanga Vizuri.

Watu kiukweli walijaa sana na wamepata adhabu ya kusimama zaidi ya Masaa 10 kwa sababu kulikuwa hakuna Viti wala mahali pa kukaa hivyo ukiingia ndani ni kusimama mpaka show inaisha.

Kitu kingine kibaya ni kujaa kwa Wahuni wengi nje ya ukumbi nawatu wameporwa vitu vyao hadharani tena kwa nguvu.

Maoni yangu kwa Waandaaji ni kujipanga ili kuepushana na Aibu waloipata Mwakahuu!!

Al-shabab hawakuwepo?
 
Back
Top Bottom