ujue kuna vitu vingine huwa havihitaji ufaham au elim ya chuo kikuu kutambua kama unaibiwa au umeshaibiwa inamaaana nyie wote mluiokwenda fiesta mmeamini kuwa umeme ulikatika?
au ni style 2 iliyotumika kuwaibia? hembu tusaidiane juu ya haya maswali machache yaliyokichwani mwangu then ndio tulaum na kulaumiana na kupeana pole.
1. mda wa kuisha show ya fiesta ulikuwa saa ngapi
(ikiwa umeme ulikatika saa 10 usiku/alfajiri?)
2.je ni wasanii wangapi ambao hawakupanda?
hembu ninukuu kidogo ' Wasanii Wengi akiwemo Diamond,Chege,Temba,Madee,Afan de Sele na Wengine Kibao hawajafanya show Wakati walikuepo kwa Ratiba'.
3.kwa wastani kila msanii alikuwa anatumia dk ngapi kupiga show.
tukiweza kupata majibu sahihi na yauhakika ya hayo majibu matatu basi tutajua mbivu na mbichi ni zipi juu ya huu utapeli.
mm binafsi sikubali kuwa umeme ulikatika kwa bahati mbaya na nawashutum na kuwatupia lawama moja kwa moja waandaaji wa tamasha hili sababu wanaijua vizuri nchi yetu hasa dar juu ya suala la umeme iwaje ishu mhim kama hii hawakuandaa jenereta ya dharula? kama sio kufanya makusudi? je kama raia wangeamua kufanya fujo na kufanya uharibufu mkubwa na yangetokea maafa na hata watu kupoteza maisha ingekuwaje ?>ikiwa na pamoja raia kupoteza na kuhalibiwa mali zao?
hivi kweli kama umeme ulikatika saa 10 mbona inaonyesha kama idadi ya wasanii waliobakia kufanya show kama walikuwa wengi sana kulingana na idadi ya masaa yaliyo bakia?
na ukizingatia show ndio ilikuwa inaelekea ukingoni ambako ndio kunawasanii ambao huwa wanafanya show za nguvu na ambao huwa wanakubalika sana hivyo huwa wanatumia mda zaidi kuliko wale fungulia mbwa wa mwanzo?
bila kusahau wasanii wageni kutoka nje ya nchi nao kumbukeni hawakupanda so kweli mda huo wa saa 1 ungetosha kweli?
au hawa waandaaji waliamua kukwepa aibu hii kwa ishu ya kukata umeme? bna kama umeme usinge katika ingekuwaje maana mm naona kama mda ni mdogo sana?
ni mtazamo na mawazo yangu jamani msijenge chuki