Yaliyojiri Fiesta

Yaliyojiri Fiesta

mjuba101

Senior Member
Joined
Oct 24, 2013
Posts
159
Reaction score
65
SERENGETI FIESTA MWAKA HUU 2013 NI NOUMA SANA,UMEME WAKATIKA GHAFLA,WASANII KIBAO HAWAJAFANYA SHOW WAKIWEMO NA WALE KUTOKA NJE YA TANZANIA.WATU WATIMUA BAADA YA KUONA LONGOLONGO NYINGI.

Usiku wa kuamkia leo pale leaders Club jijini Dar es Salaam Palikuwa hapatoshi kulikuwa na nyomi ya kufa mtu wakipata Raha za Fiesta ila Gafla Majira ya saa 10 usiku Umeme Ukazima gafla Wakati Ommy Dimpoz akiwa jukwaani na J.Martins kutoka Nigeria na kusababisha show hiyo iishie hapo.

Wengi Wamelalamika kwa Sababu Wasanii Wengi akiwemo Diamond,Chege,Temba,Madee,Afande Sele na Wengine Kibao hawajafanya show Wakati walikuepo kwa Ratiba.

Kama Vile haitoshi hata Msanii kutoka Sweden Mahombi hajafanikiwa kufanya show.Watu wamesubiri mpaka saa 11 alfajiri hatimaye wakakata tamaa na kuanza kuondoka huku lawama nyingi zikienda kwa Waandaaji kwa kutojipanga Vizuri.

Watu kiukweli walijaa sana na wamepata adhabu ya kusimama zaidi ya Masaa 10 kwa sababu kulikuwa hakuna Viti wala mahali pa kukaa hivyo ukiingia ndani ni kusimama mpaka show inaisha.

Kitu kingine kibaya ni kujaa kwa Wahuni wengi nje ya ukumbi nawatu wameporwa vitu vyao hadharani tena kwa nguvu.

Maoni yangu kwa Waandaaji ni kujipanga ili kuepushana na Aibu waloipata Mwakahuu!!
 
Kuna watu watakuwa wamefurah sana akiwemo jay dee
 
.....hawakutambikia/takasa vile viwanja kabla ya kuanza showwwwww......kila mmoja kwa imani yake alitakiwa akae kama dak 1 akiswali kulingana na imani yake....

MUNGU YUPOOOOOOOOO...binadamu anapanga MUNGU anapangua.......wengi walikuwa wanafanya/wameshafanya maovu pale uwanjani ndipo muumba wa vyote akapangua
 
hawa jamaa ujanja ujanja hauish kwakweli.. hv event kubwa kama ila wameshindwa kuwa na tahadhari kama hizo za umeme na mengneyo, siajabu hata first aid haikwepo na kitakachofuta watasema ooh tunaandaa show wataperfoam wasanii ambao hawakuperfoam then kiingilio 5000, ndio mambo ya fursa hayo, hawa jamaa wanadhani wao ndio akil zao zakua wengine tuko vilevile.
 
Yaani huwezi amini jinsi nilivyoboreka mpaka nikahisi naibiwa LIVE.Kwa kweli jana nguvu za shetani zilitawala mahali pale!
 
Sasa mnalalamika nini kwani kuna mtu aliwashurutisha kwenda kushiriki kutajirisha hilo genge la wahuni walioandaa fiesta. Kusimama masaa 10 si bora ungekuja hapa mliman city kuangalia move
 
Kwani Fiesta ni jana? Ama ni jumamosi ijayo?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
SERENGETI FIESTA


kufa mtu wakipata Raha za Fiesta ila Gafla
Majira ya saa 10 usiku
Umeme Ukazima gafla
Wakati Ommy Dimpoz
akiwa jukwaani na
J.Martins kutoka Nigeria na
kusababisha show
hiyo iishie hapo.

Wengi Wamelalamika
kwa Sababu Wasanii
Wengi akiwemo
Diamond,Chege,
Temba,Madee,Afande
Sele na Wengine Kibao hawajafanya show
Wakati walikuepo
kwa Ratiba.

Kama Vile
haitoshi hata Msanii
kutoka Sweden
Mahombi hajafanikiwa kufanya
show.Watu
wamesubiri mpaka
saa 11 alfajiri
hatimaye wakakata
tamaa na kuanza kuondoka huku
lawama nyingi
zikienda kwa
Waandaaji kwa
kutojipanga Vizuri.

Mmepata rahaaaa weeeee mpaka saa kumi alfajiri umeme kukatika mnaona ni doa. waswahili bwana kosa dogo linafuta mazuri yote!
 
Mzee Machache anawaleta P Square November hii. Tungoje tuone nae itakuaje!
 
teh teh teh teh teh teh teh safi sana ww ukiona kuna show ipo chini ya hawa clauds fm kaa mkao wa paka chongo mda wowote unaliwa.
maana kuanzia bosi wao mpaka wafanyakazi ni makanjanja wakutupwa.
sema mlio enda wote mafara ilibidi mfanye fujo na kuwaingizia hasara ya mwaka ili nao watie akili.ilibidi lile jukwaa na music systerm yote ndani ya dk 2 tu mnagawana kila 1 anaondoka na chake yaani kweli nyie mabwege tatizo vijana wa dar wengi ni mchele mchele.ndio maana vijana wa tmk huwa wanawakomesha sana kwa kuwapora .
 
Mbona wasanii walibaki wengi sana sijui walikua wanaimba dk ngapi ngapi lol!ishapita tena!
 
Back
Top Bottom