Yaliyojiri Dodoma: Shughuli ya Kitaifa ya kumuaga Hayati John Magufuli

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Tayari msafara umeshajipanga kuondoka Ikulu Chamwino kuelekea bungeni kuagwa kisha utapelekwa uwanja wa Jamhuri

=========

DODOMA: WABUNGE WATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA DKT. MAGUFULI

1.jpg


2.jpg
Spika wa Bunge Job Ndugai akiwaongoza Wabunge na Viongozi wengine mbalimbali kwenye shughuli za kuuaga mwili wa Hayati Magufuli

Wabunge wa Bunge la Tanzania wametoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano aliyefariki dunia Machi 17, 2021

Wabunge wameuaga mwili wa Dkt. Magufuli katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma na baada ya zoezi hilo kukamilika, mwili huo utapelekwa Uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya shughuli ya kitaifa ya kutoa heshima za mwisho ambao itahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kimataifa

NAIBU SPIKA: WENGI WAMEONA MEMA YA DKT. MAGUFULI. WATU WENGINE KUTOONA WEMA NI KAWAIDA

Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania umewasili Viwanja vya Bunge Dodoma kisha atapelekwa Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli ya kumuaga Kitaifa

Akizungumza katika Viwanja vya Bunge, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameeleza walio wengi wameona mema aliyofanya Dkt. Magufuli, akisema watu wengine kutoona wema ni jambo la kawaida

RATIBA YA KUMUAGA DKT. MAGUFULI DODOMA YABADILISHWA

Kutokana na wingi wa watu waliojitokeza Uwanja wa Jamhuri kumuaga Hayati Dkt. John Magufuli, ratiba imebadilishwa ambapo imeelezwa mwili utaagwa na watu wachache uwanjani

Imeelezwa mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa wananchi kuaga kwenye mitaa ili watu wote waweze kutoa heshima zao za mwisho

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge amesema baada ya watu wachache kuaga, mwili wa Dkt. Magufuli utatolewa Uwanjani na kupitishwa round about ya Jamhuri na kisha katika Barabara ya Iringa na kisha ya Polisi

Ametaja Barabara nyingine ambazo mwili utapita kuwa ni Jamatini, Bunge, Morena, Emaus kuzungushia Barabara ya Waziri Mkuu hadi African Dreams na kutokea Barabara ya Arusha hadi Uwanja wa Ndege.

WAZIRI MKUU: NAMNA NZURI YA KUMUENZI DKT. MAGUFULI NI KUUISHI UTUMISHI WAKE

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema namna nzuri ya kumuenzi Hayati Dkt. John Magufuli ni kwa Watu kuuishi utumishi wake uliojaa ujasiri, maono na mapenzi makubwa kwa Nchi

Akizungumza katika Uwanja wa Jamhuri amesema, "Wengi tulitamani aendelee kuwa nasi kimwili, hata hivyo kifo ni suala lisiloepukika"

Ameungana na kauli iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Watanzania kuendelea kushirikiana na kuzidisha umoja na mshikamano.

-

Umoja wa Afrika: Magufuli alikuwa mkombozi wa Afrika katika Utawala na Uchumi.​

Rais wa DR Congo ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa nchi za Afrika ameyasema haya alipokuwa akitoa salamu za rambirambi leo Dodoma.

Ameongeza pia Hayati Magufuli aliifanya Afrika iheshimike tena na pia ametimiza ndoto za waasisi wa nchi barani Afrika.

RAIS KENYATTA: DKT. MAGUFULI AMEONESHA WAAFRIKA TUNA UWEZO WA KUSIMAMIA UCHUMI WETU

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema katika miaka michache, Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania ameonesha kuwa Waafrika wana uwezo wa kujitoa katika utegemezi wa watu na vitu vya nje

Amesema, "Kwa muda mfupi tumeona kazi ya barabara, ujenzi wa Uwanja wa Ndege na mambo mengine mengi ambayo yatakuwa na manufaa kwa Watanzania na wana Afrika Mashariki"

Rais Kenyatta amemuelezea Hayati Dkt. Magufuli kama Rafiki wa karibu ambaye walikuwa wanaongea mara kwa mara. Amesema kifo chake ni pigo kwasababu alikuwa mtu wa heshima

Ameongeza, "Nawahakikishia tutaendelea kufanya kazi pamoja, tutaendelea kushirikiana na kuhakikisha tunaleta pamoja Jumuiya ya Afrika Mashariki"

RAIS RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI AMSHUKURU DKT. MAGUFULI KWA MAMBO MATATU

Katika hotuba yake Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Rais Cyril Ramaphosa amesema Hayati Dkt. Magufuli alisimama kama shujaa dhidi ya Rushwa na ubadhirifu, akimuelezea kama Kiongozi aliyepinga vitendo hivyo akiamini Viongozi wanapaswa kutumikia wananchi wao

Amemshukuru Dkt. Magufuli kwa kuelekeza nguvu katika maendeleo ya Kiuchumi wa Taifa la Tanzania, Ukanda na Bara la Afrika kwa ujumla

Vilevile, Rais Ramaphosa amemshukuru Hayati Dkt. Magufuli kwa kuwa Mwana wa Afrika aliyeona umuhimu wa tamaduni kukumbukwa na kufundishwa, akisema alikuwa Kiongozi aliyetaka watu kujivunia Lugha za Kiafrika

Amesema Tanzania ilipata bahati kuwa na Kiongozi kama Hayati Dkt. John Magufuli

RAIS SAMIA: MATOKEO NDIO JIBU PEKEE ALILOPENDA KUSIKIA DKT. MAGUFULI. SIO VISINGIZIO NA LAWAMA

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Hayati Rais Magufuli alipenda kusikia matokeo kutoka kwao na wala sio visingizio na lawama

Amesema, "Alitukumbusha kuwa amejitolea maisha yake kuwa sadaka kwa Watanzania hivyo hakuwa na budi kufanya kazi usiku na mchana kuwaletea Maendeleo. Sote tulihofia sana iwapo alipata muda wa kutosha wa kupumzika"

Amesema katika Uongozi wa Dkt. Magufuli, wamejifunza mengi akisisitiza "Tupo vizuri, tumeiva sawasawa"

MWILI WA DKT. MAGUFULI WAZUNGUSHWA MARA TANO UWANJA WA JAMHURI

Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli umezungushwa mara katika Uwanja wa Jamhuri ili kutoa fursa kwa wananchi kutoa heshima zao za mwisho

Hilo limefanyika baada ya Viongozi, Wakuu wa Nchi mbalimbali pamoja na Familia ya Dkt. John Magufuli kutoa heshima zao za mwisho katika Uwanja huo ambapo shughuli ya Kitaifa imefanyika

Baada ya kuzungushwa katika uwanja huo, mwili wa Dkt. Magufuli utazungushwa kupita maeneo kadhaa ili wakazi wa Dodoma waweze kumuaga Kiongozi huyo

 
Tv zionyeshe matukio mbele na nyuma ya msafara upigaji wao hauko proffessional wanaonyesha mbele tu wanasahau kuonyesha nyuma ya msafara pia kuna bodaboda na watu wanaukimbiza kusindikiza mwili umati wa watu nk.

Kuna news pia kubwa nyuma ya msafara.

TV camera men be proffessional
 
Tv zionyeshe matukio mbele na nyuma ya msafara upigaji wao hauko proffessional wanaonyesha mbele tu wanasahau kuonyesha nyuma ya msafara pia kuna bodaboda na watu wanaukimbiza kusindikiza mwili umati wa watu nk...
Wanamuogopa meko
 
Watangazaji muwe mnanyamaza na kuacha watazamaji tuangalie na kuwasikiliza waombolezaji naona tu tunawasikiliza ninyi tu muwe mnanyamaza kutuachia wenyewe tuwasikiñize sio ohhj eako wanslia halafu kilio chenyewe hata hatukisikii. Watangazaji msiwasemee hasa msafara ukifika maeneo ya watu wengi.

Let only the camera talk
 
Kitu interesting kwenye msafara ni kuwa msafara wa hizo pikipiki za polisi zililizozingira msafara na kuuongoza ni za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Polisi wa Zanzibar ndio wanaongoza msafara wa kuagwa Dodoma.
 
Raisi Ramaphosa wa Afrika ya kusini ndio anawasili Uwanja wa ndege Dodoma
 
Tayari msafara umeshajipanga kuondoka Ikulu Chamwino kuelekea bungeni kuagwa kisha utapelekwa uwanja wa Jamhuri
Nasubiri wenye wivu WATENGENEZE formula nyingine ya the expected dceased at jamhuri stadium...kama waliyoiteneneza ya uhuru stadium.
Jpm turned people to be 'mathematicians' as well...
The hatred is amazing..
Nenda pumzika jemedari wetu.....
 
Tayari msafara umeshajipanga kuondoka Ikulu Chamwino kuelekea bungeni kuagwa kisha utapelekwa uwanja wa Jamhuri
Omba mods warekebishe heading hasa kwenye jina la marehemu. Ni Magufuli na sio 'magufuri'.

'Yanayojiri Dodoma kuaga Hayati Dk Magufuri'​

 
Kitu interesting kwenye msafara ni kuwa msafara wa hizo pikipiki za polisi zililizozingira msafara na kuuonhoza ni za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .Polisi wa Zanzibar ndio wanaongoza msafara wa kuagwa Dodoma
Fafanua Kidogo Kwanini Zitoke Mbali
Bongo Hakuna
 
Tv zionyeshe matukio mbele na nyuma ya msafara upigaji wao hauko proffessional wanaonyesha mbele tu wanasahau kuonyesha nyuma ya msafara pia kuna bodaboda na watu wanaukimbiza kusindikiza mwili umati wa watu nk.

Kuna news pia kubwa nyuma ya msafara .


TV camera men be proffessional
Ni kama vile hawakuruhusiwa kutumia drones. Wangeruhusu media moja kutumia drones wengine wachukue picha toka kwao.
 
Fafanua Kidogo Kwanini Zitoke Mbali
Bongo Hakuna
Leo anaagwa kimuungano ndio masna msafara unaongozwa na polisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuonyesha sura ya kimuungano kwenye kumuaga leo kitaifa
 
Back
Top Bottom