Yaliyojiri Bungeni: Jumamosi, 29 Novemba 2014 (Hatma ya Sakata la Tegeta Escrow Account)

Mtani ubarikiwe, hakuna maombi ya watu wengi ya kijinga, hakika Mungu wetu anasikia maombi yetu. Nami na familia, ukoo wangu na hata hawara zangu, dua zetu ni kuingoa CCM.

Yaaani Mungu atupe uhai tushuhudie kwa macho itakuwa furaha isiyo kifani kumuondoa huyu mchwa nondo ccm.
 
Nimesoma mahala kwamba Waziri mkuu atatangaza kujiudhuru kwa Prof Muhongo,Prof Tibaijuka na AG.Halafu Maswi anaachishwa kazi.Aliye na habari mpya atuletee jamvini.

Hebu rudi tena kasome kama kuna mpya wameandika...
 
kwa dar tune Capital redio daily wanarusha bunge,kwa jana hata Clouds ilikuwa hewani
capital 101.3

Hii ni historia sijawahi ona tukio linalorushwa na TV na Radio nyingi hapa nchini kama ESCROW!!!.Hakika asasi za kiraia zinatakiwa kuwapa nishani Tumbili na PAC na Gazeti la THE CITIZEN
 
Kama alivyoomba mh spika anahitaji formulation ya maazimio yatakayoepusha mgogoro.sasa basi kwa kuwa wawakilishi wetu wamekwama au kukwamishwa basi si vibaya kuwasaidia na kuwanasua katika mkwamo huu.

Azimio la kwanza lisomeke hivi:

Kulingana na taarifa ya vyombo vya kiserikali,Kamati ya PAC na maoni ya wabunge mbalimbali bunge linaazimia kuwa sakata la escrow ni sakata la kifisadi na lilokiuka sheria,mienendo na maadili kkatika utendaji kazi wa serikali.hivyo bunge halina budi kuchukua kali kwa manufaa ya usalama wa nchi.

azimio hilo hapo juu ndio liwe msingi wa maazimio yatakayofuata ambayo ninyi wadau ningependa muyaongeze.
 
Pa ofisi kuna standby generator leo sitoki kwa ofisi mpaka nisikie mpaka mwisho!!
Digital world,Radio,laptop,tablet,tecno na desktop lazima nipate habari mwanzo mwisho!! 40 minutes to go!!!!

15min to go!!
 
Kwa nini mwanasheria asijiuzuru ili kuwaokoa hao wote maana kesha tamka kuwa awajibishwe yeye kwa sababu ndio alimwagiza!!

Kuwajibishwa mwanasheria mkuu wa serikali haina maana kuwa hao wengine wasiadhimbiwe. Walikuwa na wajibu wa kufanya upembuzi wa maamuzi wanayoyatoa. Wanawajibika kusimamia misingi ya kimaadili mwanasheria angewashikia gobole? Think big kosa la mwingine halikwepeshi kosa langu.
 
Ee Mola,walaani wanaotetea ufisadi na mafisadi ndani na nje ya bunge letu. Ee Mungu, wabariki watetezi wa haki zetu watz
 
1. Ipigwe kura ya kutokuwa na imani na KIKWETE kwa ajili ya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi na raslimali za uma.

2. Ipigwe kura ya kutokuwa na imani na PINDA kwa kushindkwa kusimamia ofisi yake na kusababisha hasara kubwa kwa taifa, lakini pia kutokutimiza wajibu wake kama pm.
 
mahaba mengine bwana, tusikilize kipindi cha watoto????, sasa kwa taarifa yako, hapa arusha siku zote tunaskilaza bunge kupitia arusha one radio, radio five au sunrise radio and mambo jambo radio ambazo siku zote huwa urusha matangazo, radio one imeanza jana tuuuuuuu
Nadhani utakuwa unakaa Arusha maeneo ya Kikatiti ambapo labda mawimbi ya radio one yameanza jana
 
Lipo Jipya Mkuu Na Labda Tu Kwa Faida Yako Na Kwa Wengine Hivi Tunavyobwabwaja Humu Wana CCM Wanamshawishi Werema, Maswi, Muhongo na Masele Kutangaza Kuachia Ngazi. Mangula Anahaha Sasa Na Kinana Hajalala Leo Ukizingatia Mr. TEZI DUME Anatua Leo Saa 9 na Dakika 20 Alasiri. ILA Tatizo Kubwa Ni Kwamba Hao Wahusika Na Wao Pia WEMEPIGA Mkwara Kuwa WAKITOLEWA Kafara Basi Na Wao Watayaibua Ya Mr. TEZI DUME na Wanae Minaj Na Salama Condom. Na Tegemeeni MTAFARUKU MKUBWA Leo Bungeni Na KUNA UWEZEKANO Hata ZIKAPIGWA LEO Bungeni! Hali Ni TETE.

Ila watu mnajua kupachika majina jamani, ameshakuwa mr Tezi dume tena.
 
mwanza nzima haina umeme.... tanesco na nyie kama tbc tu, hamna jipya!!!! kaeni na maumeme yenu uzuri nilishacharge simu lol!!!!
 
Habari wakuu,

Baada ya jana bunge kuahirishwa usiku, Leo saa tatu limerejea tena na aliekalia kiti ni mama Anna Makinda na ameshaahirisha bunge mpaka saa tano asubuhi kupisha vikao vya vyama(caucus) kuketi.

Mimi nachoona kinachoendelea sasa hivi ni siasa tu na sio ukweli. Ni muhimu wananchi tujue kuwa suala la ufisadi/ubadhirifu au fraud huwa inaandamana na concealment(uficho). Hii ndio sifa kuu ya Fraud yoyote ile duniani. Sasa hapa kilichotokea kinawezekana ni fraud, tena Grand Corruption, Economic and Organized Crime etc.........!

Pili tuelewe kuwa ushahidi wa fraud yoyote sio lazima uwe Beyond reasonable dought bali kinachotakiwa ni Balance of probability. Fraud ni criminal au jinai ya aina yake. Uchunguzi wa fraud unahitaji taaluma ya vitu vitatu kwa pamoja, yaani LEGAL, ACCOUNTING AND INVESTIGATION.

Sasa tujiulize, je waliofanya huu uchunguzi au wanaofanya huu uchunguzi wana taaluma hizo au wametumia taaluma hizo? Kama zipo na zimetumika basi suala liende mahakamani watu wachuane kwa ushahidi ili mwisho tujue ukweli badala ya kupiga siasa kwenye mambo yanayohitaji taaluma tofauti!

Kwenye siasa huwa hakuna mshindi hadi sanduku la kura au dhuluma iamue. kwa hivo kusubiri bunge litupe majibu ya hili suala tutasubiri sana...........!
 
Back
Top Bottom