Yaliyojiri Bungeni: Jumamosi, 29 Novemba 2014 (Hatma ya Sakata la Tegeta Escrow Account)

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Habari wakuu,

Baada ya jana bunge kuahirishwa usiku, Leo saa tatu limerejea tena na aliekalia kiti ni mama Anna Makinda na ameshaahirisha bunge mpaka saa tano asubuhi kupisha vikao vya vyama(caucus) kuketi.
==============

MAJADILIANO YANAENDELEA

Lukuvi: Kama ulivyotoa taarifa ya kuahirisha bunge asubuhi nia yako ilikuwa tupate maazimio yatakayo tuunganisha wabunge ili tuwe na maazimio yenye maridhiano yanayokubalika ndani na nje. Wabunge tumetumia fursa ya kukaa kwenye vyama, CCM tumekaa kwa na tumefanya baadhi ya marekebisho ili tutoke na maazimio, tunaomba tuendelee na majadiliano na naomba utuongezee saa moja.

Mnyika: Waziri amesema mashauriano (consultation) zinazoendelea ni za CCM hatuwezi kutoka kama bunge moja kama mashauriano ya CCM yanaenda kuchakachua mapendekezo ya kamati hivyo yasiwe mapendekezo ya wabunge, naomba muongozo hii habari ya kuweka maazimio ya chama kwa kutumia wingi wao kwenye bunge.

Lukuvi: Naomba tushaurine kwa pamoja nje ya bunge na niko sawa na Mnyika. Naomba uturuhusu tupate saa moja tushauriane kama bunge nje ili tupate muafaka.

Spika: Kimataifa ndivyo tunavyofanya, Naagiza viongozi wa upinzani na wenzao wakae pamoja maana hatutafika na anapendekeza mpaka saa kumi.

Zitto: Saa kumi mbali sana, serikali imeomba saa moja hivyo napendekeza masaa mawili tu, saa kumi ni mbali sana. Baada ya masaa mawili turudi hapa tuendelee na kazi za bunge.

Mbatia: Nakubaliana na hoja ya waziri, watu wakishauriana vizuri itaondoa mivutano na kuondoa mambo ya uchama na tukija hapa muda utakuwa mfupi wa kumalizia. Napendekeza saa nane ili iwe masaa matatu kwani saa kumi itatoa mda mchache.

Sendeka: Nakubaliana na mapendekezo lazima watayoyaleta tukubali hapana maana wanaweza kushindwana. Tuwashauri waende na naunga mkono hoja ya saa kumi lakini mimi ningependelea saa tisa.

Wenje: Napendekeza mashauriano, kamati iundwe wakakubaliane na turudi saa kumi ili vikao vya vyama(causus) vipewe muhtasari(briefed) walichoafikiana

Makinda: Nataka turudi saa kumi, wale viongozi wetu wakakae pamoja.

Silinde: Naungana na suala la saa kumi, lakini kwa sababu kumekuwa na tuhuma nyingi, napendekeza wote waliotumiwa kwenye ripoti wasihudhurie kwenye mashauriano.

Makinda: Na mimi pia nilikua nafikiria hivyo pia Zitto achukue watu wake wachache wahudhurie na naahirisha bunge mpaka saa kumi.

Bunge limeahirishwa mpaka saa kumi
===============================

KIKAO CHA BUNGE KIMEAHIRISHWA MPAKA SAA MOJA USIKU
==============================

Kikao cha bunge kimerejea tena na wabunge ndio wanaingia bungeni huku wakimsubiri spika wa bunge aingie bungeni tayari kwa kuanza kikao. Vikao vya bunge kwa leo vimeahirishwa mara mbili. Spika wa bunge aliagiza pande zote mbili waweze kuridhiana.

Spika wa bunge na katibu wa bunge ndio wanaingia bungeni tayari kwa kuanza kikao cha bunge. Zitto amesoma maazimio mapya baada ya kuondolewa ya zamani.

MAAZIMIO

Azimio: TAKUKURU na Polisi wamchukulie hatua bwana Sethi, na kumfungulia mashitaka akithibitika

Azimio: Serikali ichukue mitambo ya IPTL na iikabidhishe kwa TANESCO

Azimio: Serikali ipitie upya mikataba ya Umeme na itoe taarifa kabla ya kumalizika kwa mkutano ujao wa bunge la Bajeti

Azimio: Kwa kuwa majaji walihusika, Rais aunde Tume ya kijaji ya uchunguzi na kuwasimamisha jaji Mujulusi na Prof Luhangisa

Azimio:
Mamlaka husika ziitangaze Benki ya Stanbic na benk yoyote nyingine itakayogundulika kuwa zinahusika na utakatishaji

Azimio: Mamlaka ya uteuzi iwawajibishe na inashauriwa kutengua uteuzi wa Prof Tibaijuka, Prof Muhongo, Jaji Werema, Maswi

Azimio: Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge

Mbowe: Ametoa nasaha zake na kumuomba waziri mkuu awe mkali kuepusha mitafaruku ziku zijazo.

Fulikujombe naye anaongea, amesema wameacha uchama na kuwa wamoja katika kuwatetea watanzania na kuahidi kwa watanzania kuwa watazidi kufanya kazi vizuri na kwa uaminifu zaidi kwa niaba ya kamati pia anazungumzia kukesha kwao kulina ripoti mafisadi wasije kuipata na hatua stahiki itachukuliwa kwa kila mmoja

Wassira: Nilikua miongoni mwa wajumbe sita kuwakilisha katika kikao cha maridhiano, jana hali ilikua mbaya sana na tulitoka katika mazingira yasiyoeleweka lakini kwenye binadamu hapaharibiki jambo kumbe tukitumia busara jambo gumu linakuwa rahisi. Tumebadilishana mawazo kwa uaminifu zaidi, kwa niaba ya CCM tunashukuru kwa mjadala na CCM imeshiriki katika kufikia maazimio. Jambo lolote lenye kuleta msukosuko katika nchi haliwezi kuwa sera ya CCM hivyo tunaomba wananchi wayaunge mkono hayo tuliyokubaliana. Kama Zitto alivyosema tumegusa kila muhimili lakini tumeyagusa kwa nia njema, naunga mkono hoja.

Wabunge wameafiki japo Ole Sendeka alikua anataka muongozo kabla ya kura ya ndiyo.

Sendeka: Hakuna eneo linaloeleza kwamba taarifa hizi zitaletwa kwenye bunge hili tukufu, ni lazima taarifa irudi tena hapa kwenye bunge. Azimio la namna hii ni vizuri liwekewe taratibu.

Makinda: Swala hili limetikisa nchi, kamati zipo hivyo tuaminiane na nawashukuru kwa kazi nzuri mliyofanya na katibu anatoa hoja ya kuahirisha bunge.

Pinda: Leo tunahitimisha mkutano wa 16 na 17, ulijumuisha kazi kubwa zifuatazo(anazitaja) na anasema atazingatia maoni na ushauri kutoka kwa wajumbe, anaelezea maswali yaliyoulizwa pia anaongelea mgogoro wa wakulima na wafugaji wilaya ya Kiteto pia anaongelea biashara haramu ya pembe za ndovu kati ya Tanzania na China, kuchaguliwa Anna Makinda kwenye bunge la SADC. Anaomba kwa niaba ya serikali, atahakikisha maazimio yote yaliyopitishwa yatasimamiwa kama yalivyoazimiwa na watawasilisha bungeni matokeo ya kazi waliyoifanya. Yapo mandekezo mahsusi 14 kutekelezwa na serikali, tutahakikisha yanafanyiwa kazi kikamilifu. Yaliyopita si ndwele hivyo tukange yajayo. Serikali itaendelea kusimamia mali za taifa na kulindwa, wale wote watakaopatika kwa ushahidi wa kutosha wataadhibiwa na sheria za nchi yetu. Naitwa bango kitita kwa sababu huwa nahakikisha kila kitu kinatekelezwa ndani ya muda. Kwa nia njema, nilisemee, Je fedha za escrow ni za umma? CAG aliacha mwanya na serikali itallifanyia jambo hili kwa kina na serikali italifanyia uchunguzi kwa kina na kuja na majibu. Naomba niseme, jambo muhimu pia ni kuteremsha bei ya umeme kwa watumiaji wetu, tutahakikisha serikali inalipwa kwa fedha ambazo ni za umma, nilichijifunza leo kumbe mambo mengi yanawezekana kwa kupitia kamati ya maridhiano tena ndani ya muda mfupi.

Nakushukuru Spika na wabunge, serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika 14 desemba 2014 na maandalizi ya msingi yamekamilika.

HITIMISHO: Niwashuru waliofanikisha mkutano huu, niwashukuru PAC na kamati ya maridhiano(anashukuru makundi mbalimbali na safari njema wanaporudi pia sikukuu ya Chrismas na anatoa hoja kuahirisha bunge mpaka 27 January 2015 saa tatu asubuhi.

Spika anatoa nasaha zake kwa wabunge, Wimbo wa Taifa umeimbwa.Spika Makinda amewatahadharisha Wabunge wasirubuniwe na wanao-Lobby; wasidhani wana kinga, watawekwa ndani na kupoteza nafasi zao. . Anawahoji wabunge na anaahirisha bunge mpaka Januari 17 mwaka 2015

==================

KAFULILA: Ninaona fahari nilichokiamini na kukisimamia kimefanyika na hatua kuchukuliwa, kuna vitisho na kudhalilishwa ila vyote ni sehemu ya changamoto.
=================

ASANTENI NYOTE KWA KUWA PAMOJA KIPINDI CHOTE NA PONGEZI ZA DHATI KWA JAMIIFORUMS NA KWA WOTE WENGINEO WALIOFANIKISHA.
 
Litatokea nini! Kama wewe wameshakujuza au umo hapao mjengoni , basi tufahamishe.
 
Mimi naomba Maccm yakileta rafu kama ya Jana UKAWA watumie mbinu kama ya hana..

Maana wanachi wote tupo na UKAWA
 
Mwaka juzi, New York(State) si nchi..iliazimisha Miaka takribani 150 ya kutokatika kwa umeme Jimboni hapo, huku kwetu bado umeme unakatwa makusudi katika mambo ya muhimu(kupata taarifa muhimu na mustakabali wa Nchi) tena Nchi nzima halafu watu tumekaa kwa raha zetu.

Haya, ngoja tusubiri iwapo TANESCO wakituonea huruma!
 
Back
Top Bottom