dogo kubwa
JF-Expert Member
- May 21, 2016
- 798
- 695
Mkuu wakati unapembua maoni ya wadau toa taarifa polisi na kwa mwenyekiti wa mtaa
Good advice!!Fata ushauri wa kwenda polisi, ukizubaa kuna siku atakuvamia ndani kwako ajifanye anataka kupiga kelele umembaka, hapo ili muyamalize utaombwa kiasi flani cha hela ili yaishe, ila kama ulishawahi polisi issue itaisha haraka.
Aisee asante mkuu ingawa yanachekesha lakini inasikitisha.Siku ukikagonga ako katoto ujue umetekwa mazima na hiyo familia utaihudumia mpk hela yako ya mwisho. Umenikumbuka nilikuwa na kademu kamemaliza form 4 Kinondoni kwa Manyanya miaka ya nyuma. Walahi sitakuja kurudia kucheza michezo ya kikubwa na watoto wa uswazi kaliniteka kale katoto sijawahi ona. Nimekuja kupata akili nasomesha mpk wadogo zake bahati kuna siku nilikafuma na njemba ndio akili ikakaa sawa

Ikawaje mkuu endeleaInaweza ikawa kweli maana hata mie ishanikuta sema msichana alikua mkubwa yupo chuo kimoja hapa dsm.
Yani tulikua na mahusiano, tulipoachana yule dada hakua tayari so alikua kama anaumwa akakonda sana akapelekwa na hospital. Sasa ikabidi wazaZi wake waulize kwa rafiki zake mwenzenu ana nini wakamwambia ukweli.. Kuwa kaachwa basi nikapigiwa sana simu kuwa nimsamehe coz anaweza kufa mpaka wazazi wake kunitisha eti watafunga safari kuja home..
So jamaa anaweza kuwa na story ya kweli.
Hahaha ok mkuu ilibidi badae nimsamehe tu sababu alinicheat lakini kutokana na kuumwa ikabidi nimsamehe.Ikawaje mkuu endelea
Matokeo ya kidato cha nne bado eeeh?Sina mda mrefu toka nipate ajira iliyonifanya niame toka kwa wazazi na kupata chumba magomeni mtaa kapuni si mwenyeji hapa mtaani ratiba zangu saa 12 asubui nachomoka kwenda jobu na narudi majira ya jioni, siku za jmosi na jpili siendi job.
Kilichotokea jmosi moja niko home napiga usafi wanguo yani nafua nilipomaliza nikaenda kununua maji jirani na ninapoishi kwenye tank nikapatiwa uduma na kabint kamoja hivi kazuri kiasi nilivyomuona nilihisi ananijua maana alinichangamkia akaniuzia maji huku akinioji maswali kadhaa then nikaondoka zangu.
Mchana nipo nje ya nyumba niliyopanga nasoma gazeti moja la michezo akaja mtoto kama wa miaka mitano hivi akanipa karatasi akasema ametumwa na Dada V jina lake linaanzia na hiyo herufi nikapokea nikasoma ndani niyule msichana alieniuzia maji akajitambulisha kwenye barua zaidi anaomba namba yangu ya cm na anasema anataka niwe wake ila kwa siri maana anasoma kidato cha 3 shule akanitajia.
Dakika kadhaa yule Dogo akarudi anasema amefata majibu nikamwambia asiwe na haraka hivyo sikutoa.
Baada ya siku 3 Demu kanitegea mingo stendi akanibembeleza nikubali ombi lake nikamwambia asiwe na haraka kwani mambo mazuri hayataki haraka.
Baada kama ya wiki nikapata habari yule Demu anaumwa kutoka kwa yule dogo.
Usiku mama mmoja amekuja anajitambulisha ni mama wa yule binti anataja kujua uhusiano na mwanae nilianza lini nilikataa mwisho nikamueleza ishu ilivyokua mama aliondoka kama hakuniamini vzr siku ya pili narudi kutoka job mama kanitimbia geto anadai amekuja tukubaliane juu ya kumsaidia binti yake maana amepata kama ugonjwa maana shule asomi nyumbani kama anaumwa mda wote ananiwaza mimi kwahiyo mama ameniomba nami niigize kama nampenda binti yake ili apate kusoma.
Waungwana hebu nishaulini natamani kuhama mtaa lakini kodi yangu niliolipa bado kubwa nifanyeje maana naona kama huyu mama anataka kuniingiza kwenye mtego.