Yajue masuala mbalimbali kuhusu Biashara ya kuuza Juisi ya matunda ya aina mbalimbali

Chuck j

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
2,358
815
1590726265781.png

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
Nataka kufanya biashara ya juice,hii ya kutengeneza,matunda ya embe na nanasi,nawapa wadada wanaenda kuuza maeneo kama masokoni na kwenye mkusanyiko wa watu wengi,msaada wa kuboresha na kuifanya kwa anaejua.
---
Salam sana wakuu.

Nilipo nimeona fursa ya kuanzisha biashara ya natural juice na popcorn..nataka kujua vitu vitu vifuatavyo
-Bei ya popcorn machine
-Bei ya blender kubwa
--Bei ya juice machine ile ya kuuzia
-Bei ya blender kubwaa ya kutengeneze hizo juice
-Vifungashio vya ki..sasa napata wapi
Na chochote cha kunisaidia
---
Nina mpango wa kuanzisha fresh juice kwa kutumia baiskeli ya miguu mitatu kwa kuzungukia wateja!

Nina mpango wa kuiuza juisi hii siku za weekend,hasa nikilenga kuuzuia mashabiki wa ligi ya uingereza na zinginezo ktk kumbi zinazoonesha mpira! Nina mpango wa kubandika stickers za timu za ligi mbalimbali ktk glasi za wateja! Mathalani shabiki wa arsenal akipenda anaweza serviwa juice yenye sticker ya Giroud!

Na pia kujaribu kubandika picha za wachezaji ktk baiskeli yangu,misimamo ya ligi,top scorers,kupiga nyimbo za timu,na other infos! Pia kutoa free juices kwa mashabiki watakaojibu maswali ya mpira,hasa ligi ya simba na yanga!
Naomba ushauri jinsi ya kuboresha wazo hili?
---
Wadau,

Nina mtaji wa kuweza kufanya biashara ya juisi. Lakini tatizo bado sijapata mahali pazuri pa kufanyia biashara wala sijapata mfanyakazi wa kufanya naye hiyo biashara. Niko Dar es Salaam.

Mwenye uzoefu au anayejua chochote tuwasiliane hasa PM
1590726440003.png


BAADHI YA MAONI NA UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA WADAU WA JF
Hii biashara ukikomaa inalipa ile mbaya. Ninaposema kulipa ile mbaya kulingana na nature yake. Nakushauri kama upo Dar nenda pale Kariakoo, vitu vyote hivyo vipo.
Maana hapa hata ukishauriwa ni kwamba aina zote ulizotaja hapo juu zina Size kulingana na ujazo wake.

Kwa kujazia hapo,nakushauri
-Tafuta mashine ya Juice ila ya Port mbili hadi tatu,ili iwe rahisi kuuza juice za aina zaidi ya moja.
-Najua hapo utahitaji Freezers

-Ongezea kwa kuuza Fresh fruites, usiuze zile za kiswahili sana za papai telee,matangao ya kutupia halafu unakoroga, huo ni uji sio Fruite. Uza ile ya vipande kwa mfumo wa packing na mfumo wa kula hapo hapo. Hii inalipa sana mkuu, Dar matunda mengi sana ila ndio mkoa wa watu wanoongoza kwa uvivu wa kujimenyea matunda wao wenyewe.

-Nakushauri katika biashara hii usiweke Juice za viwandani, kwanza ni kujaza Banda bila sababu, pili faida yake inaweza kuathiri mapato ya upande wa pili.

Tambua kwamba kitu chochote unachoweka kwenye freezer au fridge lazima kupata baridi kitumie moto,na fridge au freezer hufanyakazi kulingana na idadi ya vitu vilivyomo ndani yake ili compressor iweze kuvuta umeme.Sasa biashara za faida ya shilingi 50 na zinahitaji umeme katika mfumo unaotaka kuanza wewe zitakugharimu bila kujua.

-Hakiisha fremu yako ya biashara isiwe kijiwe, watu wengie wenye kupenda kutumia kwenye mabanda hayo,huwa wanapenda kuona banda ni rafiki wa mteja na sio banda kama kijiwe cha kumnyima uhuru mteja.

-La zaidi,ukipata Mashine ya Ice cream na ukawa umepeta mafunzo ya utengenezaji wake basi hapo miguu juu.
Ila hesabu ya mashine hii ni ndefu sana,3.5 - 5m size ya kawaida outlets mbili

Nikumbuka lingine nitakuja
---
Hii Bisahara inalipa sana ukiwa sio bahili kwa wafanyakazi wako.Wengi inawashinda kwa kutowajali wahusika. Unatakiwa kwanza uwe msafi na pia jaribu kuwa unaibadilisha ladha ili isiwe common.

Na kama unaweza basi tengeneza za aina tofauti.Mfano Dar matunda ni mengi sana.
Niliwahi kuifanya hii mtaani ilikuwa inatoka licha ya changamoto za kutorejeshwa chupa.

Unaweza kuwa unatengeneza Juice ya ina moja,mfano ya Ukwaju,Avocado,Stafeli(hii unaweza kuuza mpaka ukachanganyikiwa),na pia unaweza kufanya ya kuchanganya.
Juice ya Stafeli ni nzuri sana kama vile ya avodaco,ni bora uuze ghali upate faida kidogo ila ubora uwe mzuri.

Watu wengi wanafanya Juices za kuchanganya,Embe,Peshen,Nanasi,Tangawizi kidgo, nk,kwakuwa ni rahisi na pia mchananyiko wake unatoa faida kubwa.Lakini tambua kwamba baadhi ya Juice za kujitegemea pia nazo zina faida pia.Hapo watu wanakimbia labda wingi,mfano Stafeli au avocado inabidi liwe lakutosha na huifanya iwe juice nzito kiasi.

Muhimu ni kwamba walipe wafanyakazi wako vizuri itakulipa na mungu atakuongezea. Kuna mama nilimuona Ilala anauza lakini anawadhulum wafanyakazi wake balaa, Mungu hawezi kukubariki kwa kutaka faida kubwa. Utakuta unafanya baada ya muda unafunga biashara au utatafuta Mganga.

Pia ukipata pesa nunua hata Pikipiki zile ndogo uweke Tenga nyuma ili uwe unachukua mzigo mwenye Pale Buguruni mida ya Jioni matunda yanamwaga karibu ya Bure. Kuliko kumpa Carry ambapo lazima atakubana. Mtaji ukikua nunua Carry unakuwa unapiga mzigo mwenyewe. Hata Mbuyu ulianza kama Spinach
---
tips
1.wawekee matunda mengi kias tofaut na wauzaj wengine hata kama wapo mbali na eneo lako lengo ni kutengeneza custumer base ili iwe kubwa then utaanza kupunguza kiac cha kipimo taratibu mpaka wanazoea.
note;; mwanzo wa biashara usiangalie sana faida vutia kwanza wateja sasa jifanye mkuda ufurahie shoooo
2. usafi kiwango cha rami (wewe, vyombo, banda lako,front side)
3. lugha nzuri
4. jua vizur matunda gani rais kuoza ili ujue jins gan ya kuyauza kwa uharaka..mfn-unaweza kuyatumia hata kumuongezea mteja kiaina.
6. addition weka hata kibango(list of fruit) front side kama upo road kubwa.
7.yote tisa kenda
kama huna plan nzur ili uone mafanikio ya biashara yako ni sawa SAWA NA KUPIGA MARKTIME TU BRO
Yaan umeuza laki afu kaja mwajuma ndala ndefu umempa 40.,au starehe kama zote.
---
kuna dada mmoja alianza na kuuza lita 5 mpaka kumi. alianza kwa kutumia madumu pamoja na glass za kawaida.

Za majumbani sio commercial kama ni biashara jaribu kutafuta kamtaji na uwe na vitu vifuatavyo

1. Blender yenye nguvu heavy duty. ukipata Kenwood Original (ok)
Hizi za kichina hazidumu na zinapata moto haraka na kuzima zima.
2. Juicer ambayo ni heavy duty ama kama unatumia za majumbani basi tumia Kenwood JE730 hii bei yake ipo chini ya hizo za commercial; bei ya keenwwod Je730 ni kati ya tsh 450,000/= na 490,000/=
View attachment 1014988
Hii ni ya nyumbani ila inauwezo mkubwa hata kwa biashara ndogo inafaa.
===
CHANGAMOTO YA BIASHARA KUUZA JUISI NA NAMNA YA KUIKABILI
Kuharibika
Kutokana Na kuwa juisi unayotengeneza haina kemikali yeyote iliyoongezwa ili kuitunza hivyo huweza kuharibika pindi ikikaa kwa mda wa zaidi ya saa 24.

Kumbuka Juisi atakayopeleka mteja aliyesambaziwa ataiweka kwenye jokofu lake Na kawaida ya wafanyabiashara hawezi kuwasha jokofu mda wote hivyo uhakika wa Juisi kukaa kwa mda mrefu unakuwa mdogo.

Nini kifanyike?
1. Usitengeneze Juisi nyingi wakati unaanza
tengeneza Juisi kidogo huku ukizidi kupanua masoko yako. Hii itakusaidia kuzijua changamoto zinazokupata zikiwa kidogo Na kuzitatua bila ya kupata hasara kubwa sana.\

2. Weka Juisi kidogo kwa mfanyabiashara
wakati mnaanza biashara usizidi pakiti tano kwa sehemu inayochangamka Na pakiti tatu kwa duka linadolola.

3. Fungasha Juisi za bei ya chini
kuanzia miatatu Na miambili ikiwezekana Na za Mia Mia usifungashe za miatano maana makampuni makubwa yanatengeneza Juisi za bei hiyo hivyo hutaweza ushindani utakuwa mkubwa.

4. Kila siku hakikisha Unafanya ukaguzi kwa wafanyabiashara uliowasambazia Juisi zako
ili kuangalia kama kuna Juisi zilizokaa zaidi Na zinaweza kuwa zimehatibika uzibadirishe. Kubali kuingia hasara hii maana itakufanya uimarishe soko lako Na kulilinda.

Kama hutabadirisha mfanyabiashara mwingine anaweza kuwapatia Juisi kama zilivyo Na kujikuta wateja wanahama kutumia juice zako. Sio hasara kwa mfanyabiashara kuona Juisi hazina wateja tena akaacha kuziuza tena Na wewe kupunguza soko. Biashara ikipanuka kazi hii unaweza kumpa mtu mwingine ili kupunguza majukumu Na kumudu usimamizi

5. Usipende faida kubwa
Hii huangusha sana wafanyabiashara wengi sana, ukiwaza kupata faida kubwa sana sio mbali biashara yako itakufa.
Waza kupata wateja wengi sana Na kama unavyojua Tanzania yetu watu wengi hupenda vitu vya bei ya chini ndo maana utaona watu wengi wananunua maji ya Mia yaliyofungwa Na kuacha ya miatano

6. Mazingira safi
Tengeneza Juisi yako katika mazingira ya wazi ukiimarisha usafi Na umakini mkubwa. Nunua sare nyeupe pea kama sita Na vikofia Na grovuzi za kuvaa wakati wa kutengeneza Juisi, Osha vifaa vyako vikae vikiwa safi hadi Juisi ionekane ilivyokaa kwenye kifaa mazingira yasafishwe Na kuwa mbali Na vitu hatarishi kama:
- choo
-Mshimo la taka
Usijifiche watu wakaanza kukutilia mashaka
Zalisha Juisi yako mapema sana kuanzia saa kumi hadi saa kumi Na mbili uwe umemaliza Na kupaki katika kipindi cha awali ili kuwezesha wasambazaji kupeleka Juisi kwenye masoko kwa wakati, yaani kufikia saa tatu masoko yote yamesambaziwa juisi.

7. Malipo mazuri kwa wasambazaji na wafanyabiashara
Wape faida kubwa wasambazaji Na wafanyabiashara ili kupata molali ya kuendelea kuuza Juisi yako Na uzidi kuliteka soko.

8. Simamia mwenyewe
Nakwambia hivi simamia biashara yako kwa asilimia Mia. Simaanishi ufanye kazi zote peke yako usije ukanielewa tofauti nasema simamia biashara yako mwenyewe usimpe kazi mtu mwingine halafu wewe ukajiweka kama bosi mkusanya pesa utalia mda sio mrefu.

Hakikisha kila unachokiwaza kinatekelezwa Na uliyemuagiza usicheke Na mtu kazini hapa pesa Mzee umewekeza, usijiondoe
 
Nataka kufanya biashara ya juice,hii ya kutengeneza,matunda ya embe na nanasi,nawapa wadada wanaenda kuuza maeneo kama masokoni na kwenye mkusanyiko wa watu wengi,msaada wa kuboresha na kuifanya kwa anaejua.

Si mbaya, ila may be uwe makini na package yaani uweke katika chupa/sijui container safi, za kuvutia nk, Suala la usafi pia nk, mie ni hayo tu..ila wauza juice ni kama vile wengi so yako inabidi iwe tofauti kidogo in terms ya hiyo packaging, na mambo kadha wa kadha, bila kusahau matangazo na hudumu bora kwa wateja...ngoja waje winging
 
Ndugu wanajamii forum, Kwanza natoa pongezi kwa jukwaa hili la wajasiliamali. Mimi ni mdada mwajiliwa tayari ila ninapenda sana kujiajili ama kuwa na kibiashara changu pembeni kinachoniingizia hela kwa matumizi mengine madomadogo ya familia.

Ninawaza kuanza kutengeneza juice original ya embe, parachichi, ndizi na mengineyo na kuweka kwenye kijiwe changu, je inalipa kwa wale wazoefu? au ushauri jamani. Nimejaribu kuingia mtandaoni nikaona machine za kusagia juice ila sina uzoefu nazo mwenye uzoefu na bei na wapi zinapatikana anijuze jamani. Asanteni sana.
 
Machine nilizoziona kwenye mtandao za kutengenezea juice ni hizi attached here. Kwa wale wazoefu, nisaideni ubora wake, matumizi, bei
na wapi nawezazipata. Natanguliza shukrani ndugu



juice2.png
juice3.png
 
Juice ina faida nzuri sana, kama utapata sehemu nzuri ya biashara na usafi wa hali ya juu,chemsha maji ya juice au nunua yale madumu makubwa ya Uhai.

kama upo Dar unaweza pata used maeneo ya Ilala karibia na club ya wazee kuna maduka ya vyombo used au magomeni mapipa.

Kama unataka mpya kuna duka lipo maeneo ya Gold star maeneo ya gerezani (utaona wameweka sanamu ya chef nje) wanauza vifaa vya hoteli na bakery zipo hapo mi nilinunua yangu hapo.
 
Juice ina faida nzuri sana, kama utapata sehemu nzuri ya biashara na usafi wa hali ya juu,chemsha maji ya juice au nunua yale madumu makubwa ya Uhai.
kama upo Dar unaweza pata used maeneo ya Ilala karibia na club ya wazee kuna maduka ya vyombo used au magomeni mapipa. Kama unataka mpya kuna duka lipo maeneo ya Gold star maeneo ya gerezani (utaona wameweka sanamu ya chef nje) wanauza vifaa vya hoteli na bakery zipo hapo mi nilinunua yangu hapo.
zavi unaweza kunifahamisha bei ya hizo mashine za juisi? Je Blender haiwezi kufaa?
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wanajamii forum, Kwanza natoa pongezi kwa jukwaa hili la wajasiliamali. Mimi ni mdada mwajiliwa tayari ila ninapenda sana kujiajili ama kuwa na kibiashara changu pembeni kinachoniingizia hela kwa matumizi mengine madomadogo ya familia. Ninawaza kuanza kutengeneza juice original ya embe, parachichi, ndizi na mengineyo na kuweka kwenye kijiwe changu, je inalipa kwa wale wazoefu? au ushauri jamani. Nimejaribu kuingia mtandaoni nikaona machine za kusagia juice ila sina uzoefu nazo mwenye uzoefu na bei na wapi zinapatikana anijuze jamani. Asanteni sana.

kuhusu soko hilo si la kuuliza, hata wanaotembeza mtaani watu wanakunywa bila kujua usalama wa maji yaliyotumika na processing nzima. kikubwa hapo mkuu ni location, uwe na sehem ambayo ni strategic...yenye mzunguko mzuri wa watu na mazingira safi.

Pia kuwa mbunifu sana, usiuze juisi pekee, uza pia na fruit salad, yoghurt, matunda fresh nk...kama mimi mpenzi wa papai nikiingia kwako nachagua papai unaliandaa natafuna kisha naenda zangu! ubunifu tu mkuu, fanya kitu tofauti kidogo na wengi.
 
Machine nilizoziona kwenye mtandao za kutengenezea juice ni hizi attached here. Kwa wale wazoefu, nisaideni ubora wake, matumizi, bei na wapi nawezazipata. Natanguliza shukrani ndugu

hiyo ni dispenser utahitaji blender nzuri na vyombo vinginbe kama glass na visevio vingine!
 
Juice ina faida nzuri sana, kama utapata sehemu nzuri ya biashara na usafi wa hali ya juu,chemsha maji ya juice au nunua yale madumu makubwa ya Uhai.
kama upo Dar unaweza pata used maeneo ya Ilala karibia na club ya wazee kuna maduka ya vyombo used au magomeni mapipa. Kama unataka mpya kuna duka lipo maeneo ya Gold star maeneo ya gerezani (utaona wameweka sanamu ya chef nje) wanauza vifaa vya hoteli na bakery zipo hapo mi nilinunua yangu hapo.

Asante sana ndugu yangu kwa mchanganuo huo, mie sipo Dar, nipo Shinyanga mjini. Ndo nataka nifanye hichi kitu. Usafi ni jambo muhimu sana katika uandaaji wa juice, ila ningefurahi kupata hizo machine. Nashukuru sana
 
kuhusu soko hilo si la kuuliza, hata wanaotembeza mtaani watu wanakunywa bila kujua usalama wa maji yaliyotumika na processing nzima. kikubwa hapo mkuu ni location, uwe na sehem ambayo ni strategic...yenye mzunguko mzuri wa watu na mazingira safi. pia kuwa mbunifu sana, usiuze juisi pekee, uza pia na fruit salad, yoghurt, matunda fresh nk...kama mimi mpenzi wa papai nikiingia kwako nachagua papai unaliandaa natafuna kisha naenda zangu! ubunifu tu mkuu, fanya kitu tofauti kidogo na wengi.

Asante sana mkuu, nimependa ushauri wako. Tupo pamoja, ngoja nipambane
 
Machine nilizoziona kwenye mtandao za kutengenezea juice ni hizi attached here. Kwa wale wazoefu, nisaideni ubora wake, matumizi, bei na wapi nawezazipata. Natanguliza shukrani ndugu

Hizo hazitengenezi juice, ni ka dispenser tu.

Ukishatengeneza juice ndo unaweka humo kwa ajili ya kumvutia mteja, pia kuhifadhia.
 
zavi unaweza kunifahamisha bei ya hizo mashine za juisi? Je Blender haiwezi kufaa?

Blender lazima uwe nayo kwaajili ya kusagia matunda, na hiyo uliyoionyesha kwenye picture ni dispenser kwaajili ya kuifadhia juice . na bei zake kuanzia laki 6 mpk 1....m inategemea na container zipo ngapi. lakini ukitembea unaweza pata chini ya hapo .
 
Last edited by a moderator:
Blender lazima uwe nayo kwaajili ya kusagia matunda, na hiyo uliyoionyesha kwenye picture ni dispenser kwaajili ya kuifadhia juice . na bei zake kuanzia laki 6 mpk 1....m inategemea na container zipo ngapi. lakini ukitembea unaweza pata chini ya hapo .

Acha kumtisha bhana, Wise Sister, unaweza kuzipata hizi na ile yenye ubora kabisa inayoweza kusaga/kukamua machungwa, matango, apple, mapeasi n.k ni kama shilingi 200,000 na ile ya kukamua machungwa, nanasi n.k ni shilingi 50,000.

Hii ya elfu 50 haihitaji umeme na unaweza kuitumia mahali popote. Hizo zote unatengeneza juice bila kuchanganya na maji. Mimi ninazo nyumbani kwa matumizi binafsi lakini pia zinafaa kwa biashara.

Ili kuepuka kuharibika kwa juice pale umeme unapokatika mara kwa mara, ni vyema ukahifadhi matunda kwenye friji kwani mteja akija unaweza kumkamulia juice ndani ya dakika 2 akapata kiasi anachohitaji.

Karibu.
 
Last edited by a moderator:
Blender lazima uwe nayo kwaajili ya kusagia matunda, na hiyo uliyoionyesha kwenye picture ni dispenser kwaajili ya kuifadhia juice . na bei zake kuanzia laki 6 mpk 1....m inategemea na container zipo ngapi. lakini ukitembea unaweza pata chini ya hapo .
Asante sana ndugu yangu kwa ushauri na mawazo mazuri, ngoja nipambane
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom