Yajue Madhara ya Vipodozi vyenye Kemikali na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku

Mkuu hawaoleweki ndio maana wanajitahidi kujibadilisha na wengi wao wapo humu

Ina mahusiano gani na mada husika o unapenda kubadili mada??

Nikirudi kwenye topic husika ni umasikini pia unachangaia maana rahisi ina gharama zake ndo kama hayo makansa n.k
 
Wanaume wa sikuhizi mnajipendezesha km wanawake...

Wanaume wa siku hizi mnatumia dawa za nywele..

Na si vipodozi tuu hata wapenzi wenye sumu mnatumia..tena sumu ya kuwaua taratibu sababu mnachepuka na kwenda kavu kavu...


Na si hayo tuu hata vyakula mnatumia vyenye sumu...Vinywaji vyenye sumu.....

poison poison poison full poison


Huyo anayeandika gazeti nae utakuta anatumia sumu..km si ngozini kichwani...Anayetanganza nae vile vile

pole sana bibi umri ndio huo mmh
Naona umechanganyikiwa hadi unajijibu mwenyewe
stress noma kama binti aliyefukuzwa na mkwewe
 
Ina mahusiano gani na mada husika o unapenda kubadili mada??

Nikirudi kwenye topic husika ni umasikini pia unachangaia maana rahisi ina gharama zake ndo kama hayo makansa n.k

wanawake wanatafuta muonekanao mzuri kwa namna yeyote ile ili awavutie wanaume kama hujui endelea kushangaa
 
Mwalimu alifundisha sana tena kwa bidii, wote tulisikiliza na tukasikia. Lakini walio elewa na kufaulu ni wachache sana!

Mwenye kuelewa na aelewe! Mwisho wa safari kusiwe na kulaumiana!

Ukielewa mueleweshe na mwenzio!
 
[FONT=courier
new]Zaidi ya asilimia 52 ya wanawake hutumia vipodozi vyenye sumu
ambavyo huwasababishia matatizo mbalimbali ikiwamo kansa ya ngozi, figo
pamoja na kuharibika kwa mimba kwa mama mjamzito. Aidha katika utafiti
uliofanywa na Asasi isiyokuwa ya kiserikali Envirocare mwaka jana
inaonyesha mikoa ambayo imeathirika zaidi na matumizi ya vipondozi hivyo
ambayo ni Tanga, Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na
Kilimanjaro.

Meneja wa Mradi huo, Elfansia Shayo, alisema Envirocare imeandaa
kampeni kwaajili ya kupinga matumizi ya vibodozi hivyo itakayofanyika
leo jijini Dar es Salaam. “Envirocare kwa kushirikiana na Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imefanya utafiti ulionyesha zaidi ya
asilimia 52 ya watumiaji wa vipodozi hivyo ni wanawake na baadhi yao
wanajua madhara yake,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo, Loyce Lema, alisema kampeni hiyo
inahusu kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi ya vipodozi hivyo na
ambazo viambato hivi husababisha madhara kwa watumiaji na mazingira.
Alisema pamoja na TFDA kuweka mfumo thabiti wa udhibiti wa vipodozi
ambao unatumia njia mbalimbali ikiwamo usajili wa vipodozi, utoaji wa
vibali vya biashara, na ukaguzi wa maduka bado mfumo huo unachangamoto
kwani vipodozi vimekuwa vikiingizwa nchini kwa kutumia njia zisizo
rasmi.[/FONT]

CHANZO:
NIPASHE

tukatupie picha zetu halis ntuone tulivyo natural? mpaka naona mungu alinipendelea
 
Mbona hata nyie wengi tuu asilimia 90 mnatumia

Huyo anayeandika gazeti nae utakuta anatumia sumu..km si ngozini kichwani...Anayetanganza nae vile vile

Yawezekana kwa sababu wakati mwandishi wa Nipashe amesema ni asilimia 52 ya wanawake, mwandishi wa gazeti la Mwananchi amesema ni asilimia 52 ya Watanzania hutumia vipodozi vyenye sumu wengi wao wakiwa wanawake.

"Tunafanya kampeni ya kupambana na vipodozi vyenye sumu kwa sababu tatizo ni kubwa nchini. Hadi sasa asilimia 52 ya Watanzania hutumia kati ya Sh35,000 hadi 50,000 kwa mwezi kununua mkorogo, matokeo yake wengi wameathirika na wanashindwa kuacha," alisema Euphrasia Shayo ambaye ni meneja wa kampeni ya kupinga matumizi ya vipodozi vyenye sumu.

Akizungumzia madhara ya vipodozi hivyo, Shayo alisema kwa kiasi kikubwa mkorogo husababisha saratani ya ngozi na kupunguza nguvu za kiume kwa wanaume wanaojamiiana na wanawake walioupaka.

"Kwa mtu aliyeathirika na matumizi ya mkorogo inabidi atumie dawa kwa miaka mitatu mfululizo huku akifuata ushauri wa kitaalamu. Siyo rahisi kuacha kwani kwa siku mtu hutumia hadi dawa tisa, hivyo itabidi kuacha moja baada ya nyingine," alisema.

Chanzo: Wengi hutumia vipodozi sumu - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Hata hivyo, mwandishi wa Nipashe anaweza kujitetea kwa kumnukuhu meneja huyo akisema kuwa "Envirocare kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imefanya utafiti ulionyesha zaidi ya asilimia 52 ya watumiaji wa vipodozi hivyo ni wanawake na baadhi yao wanajua madhara yake," alisema.
 
tukatupie picha zetu halis ntuone tulivyo natural? mpaka naona mungu alinipendelea

atharivipodozi.jpg


Wanawake zaidi ya milioni 6 nchini huenda wakaugua saratani, kuzaa watoto wenye mtindo wa ubongo au kupoteza maisha kutokana na kukithiri kwa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hatari. Utafiti wa Profesa Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Georgia, Atlanta, Marekani, Kelly Lewis wa kitengo cha Sosholojia, kuhusu wanawake wanaotumia ‘mkorogo' Tanzania umebainisha hayo.

Taarifa ya utafiti huo inaonyesha kuwa asilimia 30 ya wanawake, sawa na 6 milioni ya wanawake wote nchini ambao ni milioni 23, wanatumia vipodozi vyenye kemikali hatari, vyenye madini ya zebaki, hydroquinone na maji ya betri. Dk Lewis akishirikiana na timu ya Watanzania 20, aliwahoji wanawake 420 katika Jiji la Dar es Salaam ambapo wengi walikiri kujichubua kwa sababu ya dhana kuwa weupe ni uzuri, pamoja na kuwaridhisha wenza wao wanaopenda wanawake weupe.

Utafiti huo wa Shahada ya Uzamivu ulifanyika kuanzia mwaka 2000 na kumalizika Mei 17, 2012. Profesa Lewis anasema kuwa vipodozi hivyo hasa vyenye madini ya zebaki, kwa kiasi kikubwa husababisha ugumba, saratani na maradhi ya figo."Inatisha.

Wanawake hawatumii ‘mikorogo' ya dukani pekee, lakini pia wanatengeneza mikorogo ya kijadi kwa kuchanganya asidi ya maji ya betri ya gari, dawa ya meno (cc Zinduna) na sabuni ya unga," anasema Dk Kelly. Akizungumza kwa njia ya Barua Pepe, Profesa Lewis anasema kuwa anatarajia kufanya kipindi kuhusu wanawake wanaotumia mikorogo Tanzania ili kutoa elimu. ‘Kutokana na maombi mengi, nimefungua Kituo cha Utalii kwa Umma na nitafanya safari mbili za kuja nchini Tanzania," anasema.

TFDA imebainisha vipodozi vyenye sumu kuwa ni pamoja na ni Carolight, inayotajwa kuwa na sumu kali zaidi pamoja na vile vyenye madini ya zebaki au mercury, ikiwamo sabuni ya Jaribu na Mekako. Vipodozi vingine ni vile vilivyochanganywa na viambata sumu kama Clobetasol na Betamethasone ambapo itajwa pia krimu ya Amira, Betasol na Skin Success.

Inaelezwa kuwa wanawake wanaotumia mafuta ya aina hiyo wakiwa wajawazito huwaathiri watoto walioko tumboni. Asilimia 70 ya vipodozi hivyo hutoka nje ya nchi, ambapo imebainika kuwa hakuna sheria kali za udhibiti wa dawa na vipodozi.

Chanzo: Ladies Perfume: NEWS CORNER
 
Inatisha.

Lakini si kwenye vipodozi tu. Hata kwenye sekta zingine mambo ni hayo hayo tu.

Kwa mfano bidhaa za vyakula vilivyosindikwa vinavyotoka nchi za nje zipo nyingi tu ambazo huwa zimemaliza muda wake lakini bado huuzwa madukani.

Ni watu wachache sana ambao hujihangaisha kusoma tarehe ya mwisho wa ubora.
 
Inatisha.

Lakini si kwenye vipodozi tu. Hata kwenye sekta zingine mambo ni hayo hayo tu.

Kwa mfano bidhaa za vyakula vilivyosindikwa vinavyotoka nchi za nje zipo nyingi tu ambazo huwa zimemaliza muda wake lakini bado huuzwa madukani.

Ni watu wachache sana ambao hujihangaisha kusoma tarehe ya mwisho wa ubora.

Hali inatisha....hata sie tunaokula vya mashambani tunaambiwa vinalimwa kisasa mno...makemikali kibao. Dunia hii hakuna kwa kukimbilia
 
Sad story!
Nina mtu namfahamu, anaishi mjini kwa kazi hii ya kuuza vipodozi tena vilivyopigwa marufuku kuuzwa nchini. Anauza vipodozi kwa jinsi zote, wanaume na wanawake tena kwa bei ghali Sana. Wadada wengi wanaongeza makalio, wanatumia dawa za kuongeza weupe nk.

Pia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume pamoja na kuongeza ukubwa wa uume vimekuwa katika soko kubwa kwa huyu mheshimiwa. Kuna mashine za kuongeza ukubwa wa uume, analeta kwa magendo na kuuza kwa 150k tsh na zipi kwenye soko, vijana wanazingangania. Pia vidonge vya kuongeza nguvu za kiume ni soko kubwa
 
Back
Top Bottom