Yajue machache kuhusu nchi ya Brunei

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
1) Hadi kufikia 2011 zilikuwa ni nchi mbili TU ambazo hazikuwa na madeni, nazo ni LIBYA na BRUNEI

2) Brunei ndio nchi ambayo asilimia kubwa ya raia wake wanamiliki magari, wastani wa 1 kwa mtu 1.5

3) Sheria zake nyingi zinasimamia upande wa sheria za kiislamu, asilimia 72 ya raia wake ni waislaamu

4) Mwaka 2014 Brunei ilipitisha sheria ya wapenzi wa jinsia moja kufungwa miaka 10 jela na mwaka 2019 ikapitisha kuwa adhabu nyingine inaweza kuwa kupigwa mawe hadi kufa

5) Nchi hii inaongozwa kisultani ambapo sultani ndie mwenye kauli ya mwisho sultan wa brunei ndio waziri mkuu, ndio Waziri wa Fedha na ndie Waziri wa Ulinzi

6) Raia wa Brunei anayeshinda kwenye mashindano ya Quran ya kimataifa hupewa BND 2000 ambazo ni sawa na Tsh milion 3 kila mwezi katika maisha yake yote

7) Sultan wa Brunei Hassan Bolkiah ana miliki magari elfu 5 kati ya hayo magari 20 ni lamborghini.

8) Raia wa Brunei wanapata elimu bure na huduma ya afya bure na raia wake hawalipi kodi yoyote

9) Nchini Brunei si ruhusu kushikana mikono watu wa jinsia mbili tofauti

10) Ni makosa kuuza na kunywa pombe katika maeneo ya wazi

11) Chura aina ya Belalong tree wanapatikana katika nchi ya brunei pekee

12) Asilimia 97 ya raia wa Brunei wamepiga kitabu

13) Uchumi wa Brunei umeegemea utajiri wa mafuta, gesi na makaa ya mawe

14) Lugha kubwa ni kimalaya japo Kiingereza na kichina kinatumika pia

15) Dini kubwa katika nchi ya brunei ni uislam lakini pia kuna wakristo na wabudha

16) Unapoingia nyumba yoyote ukiwa Brunei lazima uvue viatu nje

17) Brunei ndio nchi yenye watu wanene katika meneo ya kusini mashariki mwa bara la Asia asilimia 51 ya watoto wana unene uliopitiliza

18) Mchezaji tajiri zaidi duniani ni kapteni wa Brunei Faiq Bolkiah ana utajiri wa Dollar Bilioni 20, yaani uchukue utajiri wa messi jumlisha utajiri wa Mo jumlisha utajiri wa Ronaldo jumlisha utajiri wa Dangote Chukua utajiri wa Jay Z bado hawamfikii huyo Faiq Bolkiah. Kwa sasa Faiq anachezea timu ya Leicester ya reserve. Faiq Bolkiah anatoka katika familia ya mfalme wa Brunei.
 
Huyo mchezaji tajiri umepata wapi takwimu zake Mkuu

Huyo bwana mdogo kazaliwa USA na amekulia kule lini amekuwa tajiri?

Japo ni kweli ana uraia wa Nchi mbili
 
Mafuta na gesi yetu kama vingeweza kutufikisha kwenye uchumi huo wabongo wangeishia kula bia na kufanya matamasha ya nyama choma saa 12hrs mpaka 12hrs 24/7

Kweli MUNGU anaangalia kwanza ndio akupe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom