Zab 16:3
"Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao."
👉Watakatifu wanaozungumzwa katika andiko hilo ni watu waliookoka na wapo hai duniani
Waefeso 2:8-9
"Maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu."
👉Hapo imeandikwa "mmeokolewa" sio "mtaokolewa," kuonyesha kwamba mtu anaokoka akiwa hai duniani.
Yohana 5:24
"Amin, amin, nawaambia, yeye asikiaye neno langu, na kumwamini yeye aliyenipeleka, anao uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani."
👉Amepita kutoka mautini kuingia uzimani maana yake tayari ameokoka - ameokoka hukumu ya moto wa milele.
👉Kuna watu wanaojifanya wameokoka lakini hawaishi kulingana na mapenzi ya Mungu. Waliookoka kweli utawatambua kwa matunda mema.
Mathayo 7:16-17
"Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mbovu huzaa matunda mabaya."
👉Kama mtu anadai ameokoka lakini anafanya ufuska bila toba, basi ni wazi huyo hajabadilishwa na Yesu Kristo.
Mathayo 7:21
"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni."
👉Andiko hilo linaonyesha wazi watakaoingia mbinguni ni wale wanaofanya mapenzi ya Mungu. Na mapenzi ya Mungu yanafanywa hapahapa duniani tungali hai.
KAMA UNAJIONA HUJAOKOKA, OMBA(FUATISHA) SALA HII YA TOBA UTAOKOKA SASA HIVI:
“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”
👉Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea na wokovu. Jiunge pia na Kanisa linalohubiri wokovu na kuamini kwamba tunaokoka hapahapa duniani; watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kuendelea na wokovu.