Kuna maisha baada ya na maisha kabla ya

Kuna maisha baada ya na maisha kabla ya

Robert20

Member
Joined
May 29, 2026
Posts
25
Reaction score
69
Maisha yanafikirisha sana
Mim ni form 4 point 29 enz hizo 2011 .Kichwani nipo empty kiasi chake
Yote ni mipango ya Mungu .ckuwa na wazazi mambo ni mengi Tena hayaelezeki, Wabongo. wanasema mambo ni meng mda mchache,

Kuna huu msemo 'AIBU UTAONA WEWE'- msemo wenye maana kubwa na fikrishi sana

Why nasema ukiishi maisha unayoyajua kuna raha yake nalenga uhalisia wa maisha
1. ukiishi familia ya kimasikini jirani zako wakawa Wana uwezo mkubwa
2. ukiishi maisha ya kitajiri badae ktkt ya safari babako uchumi ukashuka up to zero
3. ukiajiliwa na ukafukuzwa kabla haujajiandaa kwa lolote
4. ukioa mwanamke / ukaolewa Kisha mnaachana kwa sababu ya fedha
5. ukiwa KIONGOZI wa juuu alafu ,uteuzi wako ukatenguliwa
6. ukiwa KIONGOZI wa juu kweny tasisi alafu ukasistaaf ,unarudi kweny jamii
8. unaonea watu kwa sababu ya madaraka au nafasi ulionayo
9. unamtoa kafara ndugu kwa sababu ya pesa
10. unalala njaaa kwa sababu Hauna pesa na ni kweli Hauna
11. Unapewa maelekezo ufanye na unafanya lakini ukweli unaujua
12. Unamtongoza mwanamke unalala nae baadae unamuacha bila sababu za mcingi
13. unafungua biashara Bado Kuna watu wanakuroga Ili UsieNdelee .
Na mambo mengne mengi

Hapa Kuna namna nitasema, Ukweli hakuna binadamu asieumia but tusikate tamaa na tumtangulize Mungu. Naamini Kila mtu ana kundi lake
 
13 _nilifungua biashara asubuh nakutana na madawa yamemwagwa kwenye mlango.
 
Back
Top Bottom