Yahoo inasumbua!

Yahoo inasumbua!

Somoche

Platinum Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
7,034
Reaction score
9,648
wakuu leo najaribu kuingia kwenye e mail yangu ya yahoo lakini haifunguki ni mimi tu ama nyote?!! nisaidieni watalaamu
 
Me huwa nnatumia yahoo katika simu, ila lugha inayotumiwa siielewielewi. Lakini inafunguka kwa kugesi hiyo lugha hivyohivyo.
 
Kwa ujumla YAHOO iko very slow...sio peke yako tu!!
 
tuamie gmail au mwasemaje waungwana???????????????????????
 
Aisee Gmails ni mtandao wa ukweli chini ya Google! Ka vip hamia Gmail!!!!!
 
Hata mimi inanisumbua, kote kwenye messenger na mail, sijafanikiwa kufungua tangu juzi ijumaa!
 
Mi zinasumbua zote sio kwenye kufunguka ila kwenye ku-attach chochote zinagoma sio Yahoo wala Gmail, zote zinakataa kufanya attachment
 
Yahoo ikisumbua jaribu kutumia Classical yahoo badala ya All new yahoo.

Me huwa nnatumia yahoo katika simu, ila lugha inayotumiwa siielewielewi. Lakini inafunguka kwa kugesi hiyo lugha hivyohivyo.

Inawezakana kutokana na nchi uliyopo haitumii lugha unayojua.Au Page ya yahoo unayofungua sio page ya yahoo ya lugha unayojua. kama unataka kingereza kwenye adress bra type yahoo.com au yahoo.co.uk.

Yahoo ya Norway ina kinorway. yahoo ya Germany kijerumani, etc. Lakini unaweza kuchagua au kubadilisha interface ya nchi gani unataka kuona
 
Kama ungekuwa unatumia NOKIA basi unge Download OPERA MINI 4.2.Mjomba,hapa ungepata yahoo,kwa kasi ya ajabu.Unaweza kufanya mambo yote km upo kwenye PC.
 
mimi natumila yahoo mail beta-inafunguka-lakini haitaki ku-attach/ku-upload content yoyote ile-ni zaid ya wiki sasa najaribu lakini inatoa hii statement"file can't be sent"-sijajua tatizo ni nini
 
Mi nlikuwa yahoo,mwaka jana nlikuwa nataka file toka email yangu,iligoma asubui,tangu asubuhi mpaka jioni,ilipofunguka nlihamisha file zangu na vyote muhimu nkakimbilia gmail. Sijawahi kusumbuka na gmail hata siku moja na kila siku kazi zangu nyingi nafanya online.
 
Yahoo ikisumbua jaribu kutumia Classical yahoo badala ya All new yahoo.



Inawezakana kutokana na nchi uliyopo haitumii lugha unayojua.Au Page ya yahoo unayofungua sio page ya yahoo ya lugha unayojua. kama unataka kingereza kwenye adress bra type yahoo.com au yahoo.co.uk.
Yahoo ya Norway ina kinorway. yahoo ya Germany kijerumani, etc. Lakini unaweza kuchagua au kubadilisha interface ya nchi gani unataka kuona
Nimefanya kuikrem hiyo lugha yenyewe, baadhi ya maneno huwa yanasomeka hivi, email=poczta, sign in=zaloguj sie, sign out=wyloguj sie, search=szukaj, password=hasto. Haya ni baadhi ya maneno tu ninayopewa, naamini wataalamu wa lugha mpo mtayajua vizuri,
Nisaidie yahoo ya Tanzania kama ipo, sitaki ya Norway wala Germany.
 
ipige chini ingia gmail huku bata tupu. hakuuna k2 ya namna hiyo huku>
 
Yahoo imeanza kusumbua sana miezi ya karibuni tangu walipoanza kutambulisha system yao mpya ya 'Yahoo mail beta'
Kwenye software development 'beta' ni final stage kabla software haijawa released kwa matumizi, kwa hiyo mara nyingi 'beta' versions huwa zina faults.

Ushauri wangu usitumie 'Yahoo mail Beta', tumia 'Yahoo mail Classic' au all new yahoo, not 'beta'
Kama bado inasumbua, hamia Gmail, unaweza ukafungua email mpya ya Gmail na ukaredirect mail zako za yahoo ziwe zinaingia kwenye email yako mpya ya gmail kuondoa usumbufu wa kumtaarifu kila mtu kuwa umebadili email address

Yahoo ilinisumbua sana wiki 3 zilizopita, nilikuwa siwezi kulogin kwenye mail account, ila naweza kulogin kwenye messenger. Nilitafuta msaada kwenye 'yahoo service chat' ambayo waliniweka kwenye queue zaidi ya masaa matatu, nilipofanikiwa kulogin, nkamodify settings mail zote nkazidirect kwenye Gmail, sijawah pata usumbufu kwenye Gmail.
 
Back
Top Bottom