Yah; Pongezi kwa kutangaza bendera yetu kama “chapa ya cocaine” duniani

Yah; Pongezi kwa kutangaza bendera yetu kama “chapa ya cocaine” duniani

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
780
Reaction score
1,831
Meli inayopeperusha bendera ya Tanzania kukamatwa El Salvador 06.02.2025 ikiwa na shehena ya tani 6.6 ya dawa za kulevya. Mlikuwa mnasubiri upepo upite, au mlikuwa mnapiga hesabu za jinsi cocaine tani 6.6 zilivyoweza kutosha katika meli inayopeperusha utambulisho wetu bila ninyi kufahamu

Je, mnasajili meli kama line za simu mitaani? Inakuwaje meli yenye bendera ya Tanzania inanaswa na mzigo wa TZS 460 bilioni huko El Salvador, nchi ambayo hata kwenye ramani wengi wa watendaji wenu hawaijui, bila mfumo wenu wa ufuatiliaji (Tracking System) kutoa ishara yoyote?

Hizo siku 10 tangu meli kukamatwa, mlikuwa mnafanya nini? Mlikuwa mnatafuta msamiati mpya wa kutupanga kwamba “mkataba wa usajili ulishaisha”? Maana hiyo ndiyo lugha yenu ya kila siku meli zetu zikinaswa na uharamia baharini. Hii siyo mara yenu ya kwanza.

Tunajua Zanzibar ina inaendesha open registry, lakini bendera inayopeperuka ni ya Jamhuri ya Muungano. Leo hii heshima ya Mtanzania yeyote anayesafiri nje inashuka kwa sababu ya uzembe wenu wa kusajili meli za “magenge ya uhalifu” ili tu mpate dola za usajili.

Hatutaki kusikia “uchunguzi unaendelea.” Tunataka kuona watu wanawajibishwa. Huwezi kusajili meli inayobeba “canter tatu za cocaine” ikiwa na jina la nchi yako halafu useme “hatukujua.” Kama hamjui meli zenu zilipo, mnafanya nini ofisini? Mnakuna kende tu?

Acheni kutuona sawa na watoto wenu. Maelezo yenu ni kama rushwa. Hatupokei. Kama hamuwezi kulinda heshima ya bendera yetu nzuri baharini, futilieni mbali hiyo mifumo yenu ya usajili wa meli za nje (Open Registry) maana inatuletea laana na aibu kuliko faida.

Halafu tuelezeni, mzigo huo wa dawa za kulevya (cocaine) zilikuwa zinatoka wapi kwenda wapi? Huo mzigo wa thamani ya TZS 460 bilioni ni mali ya mdosi gani? Usajili (Zanzibar Maritime Authority - ZMA) unaomesha meli imesajiliwa kwa jina la nani. MTAJE

MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Mwananchi (Asiyechukua Rushwa ya Maelezo).
 
Back
Top Bottom