Yah: Mapitio ya kitabu chako mh.Mk.uu wa K aya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yah: Mapitio ya kitabu chako mh.Mk.uu wa K aya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Whisper, May 1, 2012.

 1. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwako Mheshimiwa Mkuu wa Kaya,

  wakati unatafakari jinsi ya kufanya Book review hasa zile chapter zilizolalamikiwa na wasomaji wako, niruhusu na mimi nitoe wangu mchango. Tafadhali niruhusu kama kijana wako, nahisi nami nina haki kama ulivyompa haki ya kumsikiliza mdogo wangu wangu wakati ulewa mwanzo wa kupanga (sura) chapters za kitabu chako hiki cha part II.

  Wanunuzi wengi wa kitabu chako, wamepigia mistari myekundu katika sura kadhaa wakidai kuwa umeshindwa kuleta muunganiko wa hadithi yako nzima yenye kusisimua. Nami naungana nao kwa kuwa maoni yao yana mashiko.

  Eti mwanzo wa sura hiyo ya tatu, maneno "Damu isiyo na hatia ya Mbagala" imejirudia tena mwishoni mwa sura hiyo safari hii ikiitwa "Damu isiyo na hatia ya Gongo la Mboto". Kwa mwandishi aliye makini asingeruhusu maneno haya kujirudia. Eti wanapendekeza mchapaji wa sura hii aondolewe asije akaongeza neno lingine punde baada ya wewe kufanya book review. Eti mauzo usipofanya hivyo mauzo yataendelea kudorora. ukitaka kitabu hiki kisomwa na rika zote usisahau kufanya mare

  Ingawa sura ya kwanza ulifanya vizuri kubadili rangi ya machapisho toka nyekundu kwenda nyeusi, napo ulijitahidi sana. wasomaji wanalalamika ulibana saaana ile rangi kiasi kwamba imepauka, haisomeki hata kwa kuvaa mawani nzito. Maneno yanaonekana kama matamu lakini hayasomeki. Tunaogopa kukwambia urekebishe na hapo kwani tumegundua hapo ndo mwisho wa uchaguzi wako, na kwamba tukikulazimisha utachapa kwa rangi nyeupe wakati karatasi ni nyeupe. (labda utuwekee na vinundu vinundu kama maandishi ya wale ndugu zetu walemavu wa macho. Kwa hapa ninaomba hekima yako ikuongoze.

  Ninauhakika bila shaka yoyote sura ya pili imechanwa na wanunuzi walio wengi wa kitabu chako. Hawakuona sababu ya kuwa na sura hiyo kwani inakera, inatia hasira na kichefucheefu. Ninaamini hata wewe wakati unaweka sura hiyo hukutarajia kama ingeharibu kitabu chako. Mwanzoni tu mwa sura hii mhusika aliposema haoni sababu ya kubadili manual ya uendeshaji wa gari make ya Bongo kwa kuwa watu wamekuwa wakiitumia kwa mannual hii hii. Tulishangaa sana kwani pamoja na modifications nyingi sana hata gia ya reverse hatujui iko wapi, honi hatujui inapigiwa wapi na hata hand brake hatuioni. Tulifikiri wanawake ni akini sana kwenye system kumbe huyu amewasaliti wote. Ninaona sababu ya Biblia takatifu kutowahesabu wanawake katika hesabu zake. Pengine aliwahi kuwepo mmoja wa design hii. Mh. mkuu wa kaya, usisahau kubadilisha Surs hii ya pili kwani na yenyewe iko mwanzoni tu mwa kitabu chako. Ingependeza sana kama na huyu dereva mkuu kumuondoa kabisa, ingawa ni mwanaume lakini tunaona kama vile ana chongo. Ni hatari sana kama utatoa leseni tena kwa dereva kama huyu kwa kuwa atatuingiza shimoni. Hebu kumbuka kosakosa kadhaa za ajali tulizopata mpaka tunaokolewa na majirani zetu, ingawa hatuwapendi.

  Pale katikati ya kitabu kuna ile sura ya saba inayohusu ustawi wa maeneo yetu. kwangu mimi ninaona kama unataka utuue kwa magonjwa ya mlipuko. Ni ukweli usiopingika kuwa wakinamama ni wazuri sana kwenye welfare za familia zao. Ila huyu katika kitabu chako sijui alizaliwa na nani. Eti anaonjwa chakula kwa kulamba mwiko na kuurudishia chunguni. nani anauhakika na kinywa chanke, halafu haonyeshi hata heshima ya kupiga maoti wakati wa kupokea kitu toka kwa mwanaume. Sisi wanabongo hatujawahi kulea binti wa namna hii. tafadhali rekebisha sura hii ili iwe na mvuto.

  Sasa na mimi nachanganyikiwa, naona eti ni heri uandike upya kitabu chako. Ukichanganya maoni yangu na yale mliyoazimia juzi na wahariri wa kitabu chako, Je utaweza? mimi nimewabishia wengi nimewaambia kuwa hapo ndo mwisho wa uwezo wako, lakini wananibishia. ngoja tukupe muda.

  Wasiwasi wangu ni kuwa eti wana jamvi hawapendi kusoma maneno mengi. Basi ni ombi langu ya kuwa uchanganye mabadiliko haya na yale ambayo wahariri wa mwanzo walikushauri.

  Basi roho wa bwana azidi kuwa nawe unapopitia wakati huu mgumu wa kumchinja Isaka. Ukiwa na imani ya kweli Mungu wetu atakutwalia mwanakondoo. Amen
   
 2. m

  mwikumwiku Senior Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  majungu matupu
   
Loading...