Yah. kuondolewa thread zinazokiuka sheria, maadili, miongozo na taaluma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yah. kuondolewa thread zinazokiuka sheria, maadili, miongozo na taaluma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 27, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG][​IMG]

  Yah. kuondolewa thread zinazokiuka sheria, maadili, miongozo na taaluma

  Nikiwa mdau mmojawapo wa hapa JF, kumekuwepo na malalamiko mengi kuhusu kuondolewa kwa baadhi ya mada zinazoletwa. Pengine ni kutokana na wengi wetu tunapoleta mada kutokuwa makini kwa kuangalia vigezo ambavyo ni muhimu kwa mtandao ambao ni public.

  Nchi kama Marekani habari iliyoandikwa kuhusu Usalama wa Taifa kwa kudonoa majina ya wahusika, namba zao za simu, walikozaliwa na mengineyo lingekuwa kosa kubwa ambalo bila ajizi ni kufungiwa gazeti hilo for good na mhusika kupambana na mkono wa sheria kitu ambacho ni kuishia kifungoni. Ref: "Intelligence Identities Protection Act" ya US.

  Hii mitandao inaongozwa na sheria za wanao-provide, ukivunja sheria zao tutakuja lalamika kukosa uhondo na hazina kubwa ambayo tunaifaidi kwa sasa hapa.

  Uhuru nao ukizidi unashtukia umekiuka mambo mengi na kusababisha matatizo, tuwe na kiasi na tutafaidi tunachotaka.

  Asante sana kwa mmiliki wa Mtandao huu na shukrani kwa uhuru aliotupa ambao kwa mapana na marefu hakuna mtandao mwingine Tanzania ambao unaweza kufikia uhuru huo hata kwa 50%. Vema tuutumie vema uhuru huu kwa manufaa yetu na nchi yetu.

  Candid Scope
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hiyo Marekani unayoingelea ni Marekani ipi? Yaani CIA ituhumiwe kuteka, kutesa kwa lengo la kuua na wahusika wajulikane au watajwe na victim lakini habari kama hiyo ifagiliwe tu chini ya kitanda...hiyo Marekani siyo hii United States of Amerika, kadanganye wengine!
   
 3. N

  Njele JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anika mambo ya CIA uone cha moto, bongo ni tambalare kabisa, maana kuwafunua hivyo utafumuliwa fumu fumu. Mambo mengine hapa bongo uhuru umepitiliza mno kwa vyombo vya habari, kukiuka maadili na taaluma ya uandishi ni kitu cha kawaida, lakini tuwe makini siku nyingi utashtukia umegusa idara nyeti katika ulimwengu mwingine utajikuta umekalia jivu lenye moto (ndukhsa).
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...