Yafuatayo ni madhara ya muda mrefu ya kula chumvi nyingi kwenye chakula

Khamis_Munga

New Member
Nov 11, 2022
1
0
Kifo ni hatua ya mwisho ya madhara ya chumvi lakini kuna madhara mengi sana yasababishwao na chumvi kabla ya kifo.

Tafiti zilizofanywa na jarida la new england journal of medicine nchini uingereza limegundua kwamba zaidi ya watu milioni moja na laki sita wanauawa na na ulaji wa chumvi kila mwaka,

Maisha ya kisasa na vyakula vilivyopo vinawafanya watu kula chumvi nyingi sana kuliko zamani, hii husababisha madhara makubwa ambayo hayatibiki kirahisi.

Kiafya mtu anatakiwa ale chakula chenye chumvi inayosikika kwa mbali sana na asiongeze chumvi chakula kinapokua mezani, hii ni sawa na gramu 1.5 mpaka 2.3 kwa siku, hii ni sawa na kijiko kimoja cha chakula kwa siku nzima.

Yafuatayo ni madhara ya muda mrefu wa kula chumvi nyingi kwenye chakula...

Presha ya damu; chumvi ina tabia ya kuzuia maji kutoka nje ya mwili kupitia mkojo, lakini pia kuna ushahidi kwamba kupunguza ulaji wa chumvi kwa wagonjwa wa presha hupunguza presha kwa wagonjwa wa presha.

Kansa ya tumbo; utafiti umeonyesha kwamba nchi ambazo kuna ulaji mkubwa sana wa chumvi kama japani kuna wagonjwa wengi sana wa kansa ya tumbo la chakula ukilinganisha na nchi ambazo hazina ulaji mkubwa wa chumvi kama uingereza.

Ugonjwa wa moyo; chumvi husababisha kuvimba kwa moyo na kuufanya kua mkubwa kitaalamu kama left ventricular hypertrophy, hii husababisha moyo kushindwa kusukuma damu kama unavyotakiwa kufanya kazi.

Magonjwa ya figo; kupanda kwa presha ya damu husukuma damu nyingi sana kwenye mishipa ya damu, hii huharibu figo na kuifanya kushindwa kutoa maji mwilini lakini pia viungo muhimu kama macho na mishipa ya damu huharibika.

Kupungua kwa uwezo wa mishipa ya fahamu; katika watu wenye umri mkubwa chumvi inazidi kupunguza uwezo wao wa kufanya shughuli mbalimbali na kujikuta wakitetemeka na kushindwa kubeba hata kikombe kimoja cha chai.
 
Back
Top Bottom