Yadaiwa Makonda alimwaga Rushwa Kigamboni, mratibu wake alikuwa Jack Pemba

Hata hivyo ndio mbunge mtarajiwa ,anasubiri kuapishwa tu,Ndugulile atatafutiwa kazi nyingine
What is So Special with or in Makonda??? Wapiga Kura za maoni hawakuona hiyo Speciality yake wampigie? Ndugulile ana tatizo gani Hadi asipewe nafasi ya Ubunge? Human Doctor mzaliwa na Mkaazi wa Kigamboni anyimwe Kwa nini? Acheni upambe Mbuzi kama Bashite anawalipa kumpigia Debe mitandaoni mmebugi. Wapiga Kura wameamua ule sio Uteuzi.
 
What is So Special with or in Makonda??? Wapiga Kura za maoni hawakuona hiyo Speciality yake wampigie? Ndugulile ana tatizo gani Hadi asipewe nafasi ya Ubunge? Human Doctor mzaliwa na Mkaazi wa Kigamboni anyimwe Kwa nini? Acheni upambe Mbuzi kama Bashite anawalipa kumpigia Debe mitandaoni mmebugi. Wapiga Kura wameamua ule sio Uteuzi.
Wewe komaa.lakini nilichokuambia ndio kitakua
 
Anguko lake ni anguko la babayake pia.
Akili zako sio nzuri; hivi umeona huko mtaani badala ya CCM kutoa sadaka ya
sare zake safari hii hakuna charity, watu wanananua vitambaa, wanapata wateja wakununua na kushona; inakuambia jinsi Magu alivyobadili CCM.

Waambie CDM wajaribu kama wataweza.

Magufuli hana mpinzani; endeleeni kuwalisha pumba akina Lissu kama wanaweza fua dafu mbele ya jemedari.
 
Huyu Noel Severe wa Arumeru Magharibi huku Arusha anatajwa kutumwa na wakuu na kamwaga mifwedha haswa kashika kata zote hata waliodhani watashinda wameshangaa kibao kilivyogeuka.. unalishwa Rushwa plus Yamini babaake huachi kupiga Kura ya ndiyo.
Wew ulikuwa upande wa ojungu ole satabau nn ?au ngereza mnk mtu kapata kuramoja afu bado analalamika eti yule jama cmjui ila wache wapeperushe benderaa ya ccm mnk kuna watu hawakuwa serious na uchaguzi
 
Sema utakua mjinga kama uliamini alipata zile kura 122 bila kumwaga pesa. Makonda ni mtu pekee aliepata uBilionea katika serikali ya awamu ya 5.
 
A
Mkakati wa timu ya Makonda kuhakikisha zinapatikana kura nyingi za maoni kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu Jimbo la Kigamboni uligubikwa kwa rushwa, imebainika.

Rushwa hiyo iliyotembezwa waziwazi kwa wajumbe wa mkutano huo uliomalizika leo, imedhihiri baada ya wapambe wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuanza kuwatukana na kuwatisha baadhi ya wajumbe hao.

Waliokula pesa na kuhisiwa kutompigia kura waitwa wahuni

Mara baada ya matokeo ya wagombea hao wa CCM kutangazwa, wapambe wa Makonda, wengi wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano walisikika wakitukana na kuwaita wajumbe waliodai wamekula pesa zao kuwa ni “wahuni.”

Mmoja wa wapambe hao, Jack Pemba aliyeonekana mara kwa mara maeneo ya Kigamboni tangu wiki iliyopita akiwa na Makonda, alisema “Kigamboni watu wajinga sana, wanaacha mpiganaji?” hapa akionekana kumaanisha Makonda.

Jack Pemba anatajwa katika safari zake za Kigamboni kuwa alikuwa akifuatana na timu ya wapambe wenzake kusaka wajumbe na kuwapa rushwa.

Katika uchaguzi huo, Makonda aliambulia kura 122 huku mbunge aliyemaliza muda wake, Dkt. Faustine Ndugulile akiibuka kidedea kwa kura 190.

Jack Pemba ambaye amekuwa akijinadi kuwa “rafiki na ndugu tajiri” wa Makonda, aliwasili nchini Jumanne ya wiki iliyopita.

Pemba aliwaeleza marafiki zake kwamba amekuja “kumaliza kazi Kigamboni” kwani ana mzigo wa kutosha (pesa).

Pamoja na Kigamboni maeneo mengi kulikofanyika uchaguzi huo yamedaiwa kugubikwa na vitendo vya rushwa, huku wabunge waliomaliza muda wao wakitajwa kutumia fedha nyingi kuwahonga wajumbe.

Mmoja wa wagombea kutoka Lindi amesikika akilalamika kuwa mafao ya wabunge waliomaliza muda wao yametumika kuminya haki katika mchakato huo.

CHANZO: Makonda alitembeza rushwa Kigamboni. Wapambe wake wawawakia waliokula pesa zao
Akamatwe na kufikishwa kunako husika, CCM rushwa imekuwa nembo ya chama.
 
Back
Top Bottom