Yabainika: Mjane wa Tanga aliyemlilia Rais Magufuli si tapeli. Nyaraka nyeti zaibuliwa

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
304
236
IMG_2906.JPG


MJANE kutoka Tanga, Swabaha Mohamed Shosi aliyewashtaki baadhi ya watendaji wa Serikali kwa Rais John Magufuli hapo jana akidai kuzungushwa kupewa haki yake ya mirathi si tapeli kama inavyosambazwa mitandaoni, FikraPevu imejiridhisha.

FikraPevu ililazimika kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba ili kupata ukweli wa tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwa mama huyo mitandaoni na aliithibitishia kuwa Jeshi lake halijawahi kupokea malalamiko yoyote dhidi ya mjane huyo kuhusika na utapeli.

Zimekuwepo jitihada za makusudi mitandaoni zikitoa taarifa zinazoonyesha kuwa kuna watu wanamfahamu kwa undani mjane huyo na kudai ni tapeli aliyekubuhu, bila kuwataja waliowahi kutapeliwa, walitapeliwa nini na lini walifanyiwa utapeli huo.

TUNACHOKIFAHAMU:

FikraPevu imepata kuziona nyaraka mbalimbali zinazohusiana na sakata la mjane huyu ikiwemo barua toka kwa Wakala wa Usajili na Ufilisi (RITA) ya tarehe 13 Februari 2014 kwenda kwa Mkuu wa Upelelezi kuwa nyaraka za ndoa ya mama huyo ni halali.

Screenshot from 2017-02-03 17-53-49.png


Aidha, nyaraka nyingine ni mawasiliano kati ya mjane huyo na Wizara ya Sheria na Katiba ikiwemo taarifa iliyoripotiwa Tanga kuhusu mjane kutishiwa....

Habari na nyaraka zaidi(zikiwemo za mahakamani na Wizarani) soma => Yabainika: Mjane wa Tanga aliyemlilia Rais Magufuli si tapeli. Nyaraka nyeti zaibuliwa
 
Binafsi nimeona zile text zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

Kiukweli inasikitisha kuona wengi wetu hupokea taarifa na kuzituma katika makundi mengine bila kujali athari zinazopatikana. Tunawasaidia waovu kunyang'anya haki za wanyonge.

Kama huna hakika na taarifa uliyosikia juu ya jambo fulani usiitume kwenye makundi mengine kwa kuwa ukweli utakapobainika nawe utakuwa ni mshiriki wa uovu uliofanyika.
 
Iwe huyu mama ni mjane feki au la, lakini huu mkasa wa jana ni kifunguamacho na kifungua masikio kuhusu utafutaji, utoaji, na hata uminywaji HAKI nchini bongoland.

Lakini pia umetoa vidokezo kwa watu wa usalama wa Rais. Ilikuwaje huyu mama akafika katika mkutano huo.

Hiyo tisa, kumi aliingiaje na kuweza kutembea na bango hadi hapo alipodhibitiwa? Je, walinzi walitumia professionalism katika kumdhibiti au walikuwa nao wamepanic?

Bongoland na watu wake tu kivutio kingine cha utalii.
 
Nadhani hapa ufanyike uchunguzi huru wa kina kubaini ukweli ili haki itendeke kwa kila upande, maana kwa sasa kila mtu anaongea la kwake
 
Fikra Pevu ushahidi wa upande mmoja hauwezi kukubalika. Kuna watu hulia sana ila mwisho wa siku huwa ni matapeli.

Ingekuwa fair kama mngeweka nakala ya hukumu halisi. Na pia kutuwekea na ile inayodaiwa kuwa feki.

Nakala kipisi ya hukumu iliyowekwa hapo sidhani kama ilimpa ushindi wowote kwenye kesi ya msingi bali haki yake ya zuio kuwa lisifanyike jambo bila swala la msingi kupatiwa ufumbuzi lilikubaliwa ( si mwana sheria but ndio tafsiri ninayoina hapo)
 
tunaomba utafute na ushaidi wa upande wa pili wa anaowalalamikia ili kuweka mzani wa hii habari yako.otherwise confrimation of marriage certificate haiwezi kutuondolea dhana kuwa yeye ni tapeli unless utoe prove ya upande wa pili yaani hao anaowalalamikia ukishindwa tueleze ili tubaki kwenye hoja maana tayari unafanya jitihada za kutuondoa kwenye hoja
 
Kwa vile swala hili limefika mahala pake nafikiri tuvute sheria na haki itapatikana kwa pande zote mbili.
Mimi nadhani Fikrapevu wamejidharilisha, wameongea na kamanda wa Polisi, wameshindwa nini kuongea na mama wa marehemu na wajane wengine wa marehemu? Hivi hao wengine sio wajane? Rais wetu mpendwa jana ametumia busara na hekima, ameagiza uchunguzi ufanywe ili kila mtu apate haki yake. Tusubiri.
 
Mimi nadhani Fikrapevu wamejidharilisha, wameongea na kamanda wa Polisi, wameshindwa nini kuongea na mama wa marehemu na wajane wengine wa marehemu? Hivi hao wengine sio wajane? Rais wetu mpendwa jana ametumia busara na hekima, ameagiza uchunguzi ufanywe ili kila mtu apate haki yake. Yaani cheti cha RITA ndio nyaraka nyeti? Tusubiri.
 
muda ndio utaamua ukweli kama huyu mama ni tapeli itajulikana bahati nzuri rais hakutoa maamuzi ya pupa bali aliwaagiza wanaohusika wafatilie madai ya huyu mama ili haki ipatikane
 
Hilo Gume Gume la Kimombasa ni Hatare sana!

Jana alitaka kutingisha Mihimili ya Nchi hadharani!

Mzuka wa JPM Jana haukuwa juu sana Kama ule wa kuzindua Daraja la Kigamboni otherwise tungekuwa tunasubiria uteuzi wa Vigogo kwny Idara nyeti sana za nchi Muda huu
 
Mwenye mamlaka na mali za marehemu kisheria si mtu anaitwa mke, au mme,au mtoto, au mzazi wa marehemu, bali ni yule aliyeteuliwa na mahakama kuwa msimamizi wa mirathi. Inaweza kuwa kati ya hao niliwataja au mtu baki kabisa au afisa wa serikali toka RITA. Mtu kuwa mmoja ya warithi haikupi haki ya moja kwa moja kudeal na mali za marehemu. Sasa huyo mama atwambie kama yeye ni msimamizi wa mirathi au ni mmoja wa wanufaika/beneficiaries wa mali za marehemu

Na je aliposema nadhulumiwa mali za mme wangu, ni mrithi pekee, yaani hakuna wengine!?

Na kama kuna mirathi imefunguliwa na msimamizi wa mirathi kuteuliwa, je hicho alicholilia mbele ya rais ni sehemu ya mgao wake au anataka yeye pekee arithi vyote na wengine wakose!!?

Kwa kifupi na kwa uzoefu wangu, kesi za mirathi karibu zote ni balaa, na huchukua muda mrefu mahakamani
 
Back
Top Bottom