Yaani katika yote, hili? Nkamia Acha Utani Bana!

Yaani katika yote, hili? Nkamia Acha Utani Bana!

Haya ya Nkamia ni matokeo ya kuusoma upepo wa Magogoni. Hii kampeni ya kubaki madarakani haijawahi kuanza mapema kama kipindi hiki. Na sababu kuu ni kwamba watu wamegundua jamaa hapendi kupingwa au kukosolewa na ndio maana akasitisha mikutano ya hadhara ya siasa ya kitaifa. Pia anajaribu kumjibu kila anayemkosoa, tena kwa kejeli. Ameonyesha chuki ya wazi kwa wapinzani.

Kwa maoni yangu naona wakati muafaka umefika wa sisi kukiri kwamba huyu mtu hatukumfahamu vizuri tabia yake wakati anagombea. Wote tulimjua kama mchapakazi ambaye hayumbishwi, kumbe kuna la ziada-hapendi kupingwa wala kukosolewa.
 
Naomba kujua Mkaa wa mia anataka Raisi ndo aongezewe muda au na wabunge na madiwani?
 
Kwa wale tunaoifahamu nchi yetu vizuri, kusema mabadiliko ya Katiba hayahitaji rukhsa ya Raisi ni kuwa mvivu wa ku-observe mambo na kusema ukweli. Kwa mfumo uliopo niambie nani atafanya au atatoa ridhaa hiyo kama siyo Raisi? MMM umekuwaje? Siamini kwamba hilo hulioni.
 
Ishapita hiyo...hoja hii hailetwi kwa bahati mbaya.
 
Kati ya watu wa ajabu nilioanza kuoredhesha ktk nafsi yangu huyu ameshika namba moja!Atambue kati ya vitu vinavyotumia gharama kumbwa ktk utawala ni demokrasia.
 
Haya ya Nkamia ni matokeo ya kuusoma upepo wa Magogoni. Hii kampeni ya kubaki madarakani haijawahi kuanza mapema kama kipindi hiki. Na sababu kuu ni kwamba watu wamegundua jamaa hapendi kupingwa au kukosolewa na ndio maana akasitisha mikutano ya hadhara ya siasa ya kitaifa. Pia anajaribu kumjibu kila anayemkosoa, tena kwa kejeli. Ameonyesha chuki ya wazi kwa wapinzani.

Kwa maoni yangu naona wakati muafaka umefika wa sisi kukiri kwamba huyu mtu hatukumfahamu vizuri tabia yake wakati anagombea. Wote tulimjua kama mchapakazi ambaye hayumbishwi, kumbe kuna la ziada-hapendi kupingwa wala kukosolewa.
Wengine tulijua ni kimeo tokea zamani.Kama ulifuatilia nyendo zake hata kwenye uwaziri alishafanya madudu na ukurupukaji wa kutosha,ndo haya mengine yanamuwinda sasaiv kama ile ishu ya deni canada na meli ya wachina
 
Wanaeza hata kuvunja sheria hawa kwa kutumia vibaya uwingi wao kupitisha.

Hii siyo Rwanda.
 
Tangu lini mwanaccm akakubali katiba ya Warioba inayowapa wananchi nguvu? Nkamia katumwa kupima upepo uko bungeni na inawezekana muswada uko jikoni, yule Kabudi sio wakumuamini sana.
 
Kwa mawazo yangu na utafiti mdogo nilioufanya nimeona kwamba ukipitishwa muswada wa Raisi kuongoza miaka saba.Matumizi ya simu kwenye issue nzima ya mitandao ya kijamii itafungiwa na kuruhusiwa kutumiwa wakati wa usiku.HUU NI UTAFITI WA AWALI niliouona.Mrejesho nitaurudisha baada ya utafiti kukamilika.Naomba kuwasilisha
 
Hapana IO sihawahi kuwa shabiki wa serikali mbili..mi ni shabiki wa serikali moja au utengano.
 
874d9b8a403d5e0562ad116efe4ad9fc.jpg
 
Mwanzoni tulidhani ni jambo la utani au uropokaji tu, lakini sasa tumegundua kuwa alichokisema Juma Nkamia siku chache zilizopita bungeni kilikuwa ni kitu halisi na mpango kamili.

Bila kumumunya maneno Tanzania tunaingia kwenye jaribio zito la kutaka kubadilisha katiba ya nchi ili muda wa rais kukaa madarakani ubadilishwe kutoka miaka mitano mpaka miaka saba kwa muhula mmoja.

Habari za ndani kabisa katika medani ya siasa zinasema kuwa, Juma Nkamia ni mjumbe tu katika hili ila wenye huo mpango wapo na muda ukifika watakuja hadharani, na wamedhamiria kweli kweli. Hawatanii.
Wapo wanaoamini kuwa, Nkamia kausoma mchezo na kuamua kuucheza mapema ili apewe ile tuzo(cheo) au kutumwa kupima upepo au katumwa kutupoteza maboya ili ile siri ya mpango halisi tuchelewe kuigundua mapema au huenda katumwa kutuandaa kusaikologia....

Mwanzoni walianza na kampeni hizi
-Magufuli baki.
-Magufuli atawale hata mpaka 2030.
-Hakuna haja ya kufanya uchaguzi 2020.
-Tubadirishe katiba ya CCM ili rais aliyepo madarakani asipingwe na mwanaCCM yoyote akitaka kuendelea na awamu ya pili.

Watanzania tuanze kujipanga kisaikologia katika kukubali au kulipinga, kwa sababu mpango wa hilo jaribio uko tayari na kinachofuata ni utekelezaji wake.

Jambo kubwa kwa sasa ni kutaka kujua kwa wazi kabisa, Juma Nkamia katumwa na nani?
Tuwajue mapema waliopo nyuma yake ili tujue nguvu ya msukumo wa jambo hilo.

Kwa kuanzia tu, sote tunafahamu kuwa Juma Nkamia ni mbunge wa jimbo la Chemba kutoka CCM, tunategemea kusikia kauli kutoka kwenye chama chake sasa kama wako pamoja naye au wanampinga?
Pia serikali ya CCM iliyopo madarakani ikiongozwa na Mheshimiwa Magufuli kama wanaunga mkono au wanapinga hilo jaribio la Nkamia?
Ukimya wao utazaa maswali mazito sana.

LISEMWALO LIPO, KAMA HALIPO HUENDA LINAKUJA.
 
Naye atafungwa..
Jino kwa Jino.
Akacheze dance na akina lipumba. vipi.
Na washwa washwa.
Ukweli mchungu!!!
 
Kama kungekuwa na sayansi nyingine yenye maisha ningehamia niachane na utawala wa Bashite na baba yake.
 
Back
Top Bottom