Yaani katika yote, hili? Nkamia Acha Utani Bana!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,251
Reaction score
44,586
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa wanaonisoma kwa muda mrefu watakumbuka kuwa sikuwahi kuwa shabiki wa mchakato wa Katiba Mpya ulioanzishwa na Rais Kikwete. Sikuukubali kwanza kwa sababu ulikuwa unapingana moja kwa moja na Ibara ya 100 ya Katiba hii ya sasa pamoja na mapungufu yake yote. Na hata mchakato ule ulipofikia kuundwa kwa Bunge la Katiba na baadaye kuja na Katiba Pendekezwa nadhani nilikuwa miongoni mwa watu wachache ambao siyo tu tulikataa msingi wa ile Katiba lakini tuliyakataa hata mapendekezo ya Warioba na Katiba pendekezwa.

Niliita ile Katiba na mchakato mzima kuwa ni "bambikizi". Kwamba, Watanzania walikuwa wamekubali kubambikiziwa mchakato haramu na Katiba haramu.

Nilisema wakati ule - na bado ni msimamo wangu wa sasa - hatuwezi kupata Katiba Mpya bila kuanza na mabadiliko ya kawaida ya Katiba ya sasa chini ya Ibara ya 100. Kwa sababu Katiba ya sasa haina mlango au njia nyingine yeyote ya kutuelekeza kwenye Katiba Mpya bila kufanya mabadiliko Katiba hii ya sasa; mabadiliko ambayo yatapitishwa na Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Hili siyo somo langu kwa leo hata hivyo.

Kwa leo nataka kugusia kwa pembezoni kukerwa kwangu na jaribio dhaifu la kutafuta umaarufu kwa kujaribu kutaka kubadilisha Katiba ya sasa ili iongeze muda wa Urais kutoka miaka mitano ya sasa hadi miaka saba. Binafsi sina tatizo hata na hilo pendekezo; kwani linawezekana na katika nchi ya kidemokrasia lilikubalika katika mchakato halali linaweza kuwa sehemu ya utawala wetu.

Tatizo langu ni kuwa, muda wa Urais haujawahi kuwa tatizo katika utawala wetu. Kwamba, hatujawahi kuwa na tatizo la msingi la kwanini miaka mitano haimtoshi mtu au miaka kumi (kama akichaguliwa mara mbili) kwanini haitoshi. Kama mtu akijaribu kwa miaka mitano na watu wakaona anafaa wakaamua kumuongezea mingine mitano basi mtu huyo atakuwa ameweza kufanya mambo kwa miaka kumi; hiyo ni zaidi ya miaka saba inaypendekezwa na Nkamia. Na kama mtu akishindwa katika miaka kumi hata umpe mingine mingine anaweza asifanikiwe sana na badala yake atakuwa anahangaika zaidi kukaa madarakani kuliko kufanya kazi.

Watanzania tumekuwa na matatizo mengi ya Kikatiba ambayo yangeweza kuondolewa kwa mabadiliko ya Katiba. Masuala ya mahusiano kati ya mihimili ya dola, utendaji wa mawaziri, masuala ya nguvu za Waziri Mkuu, uhusiano wa rais na Waziri Mkuu, n.k ni baadhi tu ya mambo ambayo yamekuwa yakizua maswali na hoja nyingine.

Nkamia kama kweli anataka kuonekana shujaa wa Katiba, ni bora angekaa chini na wabunge wapande zote mbili na kujiuliza ni mabadiliko gani yanaweza kupendekezwa sasa hivi katika Katiba ya sasa. Nkamia badala ya kutaka tufanye mabadiliko ya Katiba katika jambo lisilotusumbua angekaa chini na kuangalia ni jambo gani linatusumbua na angeliletea mapendekezo. Kwa mfano, angesema tufanye mabadiliko ili mawaziri na wateule wote wa Rais wa ngazi za kitaifa wapitishwe na Bungeni nina uhakika angepata kuungwa mkono.

Kwa pendekezo lake hili nina uhakika linakufa linapofikishwa hospitali tu (Dead On Arrival).

Lakini inawezekana ametoa pendekezo hili kama utani, na kejeli tu ya kuwadharau Watanzania na zaidi kupuuzia haja na matamanio hasa ya Watanzania. Sasa kama huu ulikuwa ni utani basi hatucheki; lakini kama alikuwa anamaanisha hasa napendekeza ajifikirie kama ana uwezo mzuri kichwani wa kufikiri kama mtunga sheria na mtu ambaye anayajua kweli matatizo ya Kikatiba ya nchi yetu. Kama hajui ni vizuri angekaa chini na watu wabobezi wampe darasa la bure la ni vitu gani hasa Watanzania wanatamani kuviona vikishughulikiwa katika Katiba.

Pamoja na hayo, kama yuko makini napendekeza akae chini na wabunge wa chama chake na wabunge wa chama kingine ili waje na mapendekezo makubwa ya mabadiliko ya Katiba yetu ambayo yatagusa maeneo mbalimbali. Na akifanya ihvyo chini ya Ibara ya 100 nina uhakika siyo tu ataungwa mkono na Watanzania wengi. Na kwa vile mabadiliko ya Katiba hayahitaji kibali cha Rais basi nina uhakika yanawezekana kabisa. Tatizo pekee ni kuwa yanahitaji wingi wa wabunge katika vyombo vyote viwili vya kutunga sheria na kwa vile vyombo hivi vyote vimetawaliwa na Chama cha Mapinduzi basi kazi yake inaweza kuwa rahisi au ngumu kutegemeana na aina ya mapendekezo yenyewe.

Nje ya hapo, utani mwingine mbaya.

MMM
 
Nkamia anawapa mtaji wapinzani 2020. Hilo la kujiongezea muda halitakuwa jema sana. Azuiwe! Kama ana nia ya Magufuli baki basi asubiri walau 2022.
 
definition nyepesi kabisa kuliko zote ya demokrasia ni 'wengi wape', labda atakayepinga ili atakuwa dikteta uchwara
 
Nkamia anawapa mtaji wapinzani 2020. Hilo la kujiongezea muda halitakuwa jema sana. Azuiwe! Kama ana nia ya Magufuli baki basi asubiri walau 2022.
 
Ni hivi hilo pendekezo sio la Juma Nkamia bali ni la yule aliye juu zaidi. Walianza utani wa Magu baki wakapima upepo, sasa wameamua kulifanya kwa vitendo. Na ninakuhakikishia hilo litapita kwa sababu wabunge wa ccm wanaunga mkono chochote kinacholetwa na mbunge wa ccm. Na kwakuwa sasa hivi wananchi wamewaachia wabunge wafanye lolote bila kuwashirikisha basi hilo la miaka 7 litapita na ikibidi atakuwa kama Kagame au Museveni. Kama huamini ngoja maneno yangu utaona ni nini nakwambia.
 
Nkamia ametaka kuongezwe muda wa bunge jamani sio muda wa urais labda kama barua niliyoiona sio yake au aliwasilisha barua mbili tofauti.
 
Inawezekana kuna nguvu kubwa isiyoonekana nyuma ya Nkamia.Ni swala la muda tu tutajua.Ukiona mwitikio wa wabunge walio wengi ni mzuri,ujue hii tena ni amri kutoka kwenye ule muhimili uliojichimbia zaidi.
Sekretarieti ya sasa ya chama haiwexi kumpa jukumu kama hilo mtu ' aina' ya Juma!!!
 
Japo Nkamia analaumiwa, but he has a point.
Uzoefu wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete, imeonyesha rais wa Tanzania hukaa miaka 10. Hivyo uchaguzi wa rais 2020 ni igizo tuu la uchaguzi ambao ni wastage of time, money, and resources

P
Kumbe hata wewe ni kilaza ? Tambua hapo unaongelea miaka14 sio saba tena acha ukilaza paschal! Kuwa serious basi.
 
Nkamia anawapa mtaji wapinzani 2020. Hilo la kujiongezea muda halitakuwa jema sana. Azuiwe! Kama ana nia ya Magufuli baki basi asubiri walau 2022.
Upinzani usikubali kuujadili huo mjadala.
Waamue kata kamba na kuja huku mtaani ili tuwape baraka
 
Nkamia ametaka kuongezwe muda wa bunge jamani sio muda wa urais labda kama barua niliyoiona sio yake au aliwasilisha barua mbili tofauti.
Amesema (akihojiwa na chombo kimoja cha habari kwa njia ya simu) nanukuu "Rais ni sehemu ya Bunge"
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa wanaonisoma kwa muda mrefu watakumbuka kuwa sikuwahi kuwa shabiki wa mchakato wa Katiba Mpya ulioanzishwa na Rais Kikwete. Sikuukubali kwanza kwa sababu ulikuwa unapingana moja kwa moja na Ibara ya 100 ya Katiba hii ya sasa pamoja na mapungufu yake yote. Na hata mchakato ule ulipofikia kuundwa kwa Bunge la Katiba na baadaye kuja na Katiba Pendekezwa nadhani nilikuwa miongoni mwa watu wachache ambao siyo tu tulikataa msingi wa ile Katiba lakini tuliyakataa hata mapendekezo ya Warioba na Katiba pendekezwa.

Niliita ile Katiba na mchakato mzima kuwa ni "bambikizi". Kwamba, Watanzania walikuwa wamekubali kubambikiziwa mchakato haramu na Katiba haramu.

Nilisema wakati ule - na bado ni msimamo wangu wa sasa - hatuwezi kupata Katiba Mpya bila kuanza na mabadiliko ya kawaida ya Katiba ya sasa chini ya Ibara ya 100. Kwa sababu Katiba ya sasa haina mlango au njia nyingine yeyote ya kutuelekeza kwenye Katiba Mpya bila kufanya mabadiliko Katiba hii ya sasa; mabadiliko ambayo yatapitishwa na Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Hili siyo somo langu kwa leo hata hivyo.

Kwa leo nataka kugusia kwa pembezoni kukerwa kwangu na jaribio dhaifu la kutafuta umaarufu kwa kujaribu kutaka kubadilisha Katiba ya sasa ili iongeze muda wa Urais kutoka miaka mitano ya sasa hadi miaka saba. Binafsi sina tatizo hata na hilo pendekezo; kwani linawezekana na katika nchi ya kidemokrasia lilikubalika katika mchakato halali linaweza kuwa sehemu ya utawala wetu.

Tatizo langu ni kuwa, muda wa Urais haujawahi kuwa tatizo katika utawala wetu. Kwamba, hatujawahi kuwa na tatizo la msingi la kwanini miaka mitano haimtoshi mtu au miaka kumi (kama akichaguliwa mara mbili) kwanini haitoshi. Kama mtu akijaribu kwa miaka mitano na watu wakaona anafaa wakaamua kumuongezea mingine mitano basi mtu huyo atakuwa ameweza kufanya mambo kwa miaka kumi; hiyo ni zaidi ya miaka saba inaypendekezwa na Nkamia. Na kama mtu akishindwa katika miaka kumi hata umpe mingine mingine anaweza asifanikiwe sana na badala yake atakuwa anahangaika zaidi kukaa madarakani kuliko kufanya kazi.

Watanzania tumekuwa na matatizo mengi ya Kikatiba ambayo yangeweza kuondolewa kwa mabadiliko ya Katiba. Masuala ya mahusiano kati ya mihimili ya dola, utendaji wa mawaziri, masuala ya nguvu za Waziri Mkuu, uhusiano wa rais na Waziri Mkuu, n.k ni baadhi tu ya mambo ambayo yamekuwa yakizua maswali na hoja nyingine.

Nkamia kama kweli anataka kuonekana shujaa wa Katiba, ni bora angekaa chini na wabunge wapande zote mbili na kujiuliza ni mabadiliko gani yanaweza kupendekezwa sasa hivi katika Katiba ya sasa. Nkamia badala ya kutaka tufanye mabadiliko ya Katiba katika jambo lisilotusumbua angekaa chini na kuangalia ni jambo gani linatusumbua na angeliletea mapendekezo. Kwa mfano, angesema tufanye mabadiliko ili mawaziri na wateule wote wa Rais wa ngazi za kitaifa wapitishwe na Bungeni nina uhakika angepata kuungwa mkono.

Kwa pendekezo lake hili nina uhakika linakufa linapofikishwa hospitali tu (Dead On Arrival).

Lakini inawezekana ametoa pendekezo hili kama utani, na kejeli tu ya kuwadharau Watanzania na zaidi kupuuzia haja na matamanio hasa ya Watanzania. Sasa kama huu ulikuwa ni utani basi hatucheki; lakini kama alikuwa anamaanisha hasa napendekeza ajifikirie kama ana uwezo mzuri kichwani wa kufikiri kama mtunga sheria na mtu ambaye anayajua kweli matatizo ya Kikatiba ya nchi yetu. Kama hajui ni vizuri angekaa chini na watu wabobezi wampe darasa la bure la ni vitu gani hasa Watanzania wanatamani kuviona vikishughulikiwa katika Katiba.

Pamoja na hayo, kama yuko makini napendekeza akae chini na wabunge wa chama chake na wabunge wa chama kingine ili waje na mapendekezo makubwa ya mabadiliko ya Katiba yetu ambayo yatagusa maeneo mbalimbali. Na akifanya ihvyo chini ya Ibara ya 100 nina uhakika siyo tu ataungwa mkono na Watanzania wengi. Na kwa vile mabadiliko ya Katiba hayahitaji kibali cha Rais basi nina uhakika yanawezekana kabisa. Tatizo pekee ni kuwa yanahitaji wingi wa wabunge katika vyombo vyote viwili vya kutunga sheria na kwa vile vyombo hivi vyote vimetawaliwa na Chama cha Mapinduzi basi kazi yake inaweza kuwa rahisi au ngumu kutegemeana na aina ya mapendekezo yenyewe.

Nje ya hapo, utani mwingine mbaya.

MMM
Ati haukuwa mshabikiwa katiba mpya!!!??

Kumbuka kuwa ulikuwa mshabiki mkuu wa serikali mbili. Ulipinga kwa nguvu zote serikali tatu
 
Back
Top Bottom