Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Kila nikifanya tafakuri sipati jibu. Tangu jana nimejitahidi kufikiri na kufikiria bila ya kupata nini hasa kilisababisha. Kitendo cha Waziri wa Uchukuzi, Dr.Harrison Mwakyembe kuikana UDA kuwa haiko Wizarani mwake bado sikielewi. Ni usahaulifu au alilenga jambo fulani?
Dr.Mwakyembe ni kati ya Mawaziri wasomi wabobezi ambao Serikali ya Rais Kikwete inao. Ni Msomi wa Sheria ambaye anaaminiwa na kutarajiwa kujua madaraka yake;mipaka ya madaraka yake;walio chini yake na walio nje ya uwanja wake wa kujidai wa Wizara ya Uchukuzi. Uchukuzi ni usafirishaji.Sasa iweje Shirika la Usafirishaji la Mkoa wa Dar es Salaam lisiwe chini ya Wizara ya Uchukuzi?
Nasema tena kuwa hadi leo bado siamini maneno ya Dr.Mwakyembe. Siyaamini kwakuwa yanatisha sana. Inawezekana wapo Mawaziri ambao hawajui wanaowaongoza. Sasa wanaongozaje? Sakata la UDA 'lilishazimwa' kimahakama.Hakukuwa na sababu za kukana haraka vile. Nitoe wito kwa viongozi wetu-wa ngazi zote kutambua wanaowaongoza/wanavyoviongoza ili uongozi wao uwe na maana,tija na faida.