Ya Waziri Mwakyembe;hadi sasa bado siamini

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,175
25,446
Kila nikifanya tafakuri sipati jibu. Tangu jana nimejitahidi kufikiri na kufikiria bila ya kupata nini hasa kilisababisha. Kitendo cha Waziri wa Uchukuzi, Dr.Harrison Mwakyembe kuikana UDA kuwa haiko Wizarani mwake bado sikielewi. Ni usahaulifu au alilenga jambo fulani?

Dr.Mwakyembe ni kati ya Mawaziri wasomi wabobezi ambao Serikali ya Rais Kikwete inao. Ni Msomi wa Sheria ambaye anaaminiwa na kutarajiwa kujua madaraka yake;mipaka ya madaraka yake;walio chini yake na walio nje ya uwanja wake wa kujidai wa Wizara ya Uchukuzi. Uchukuzi ni usafirishaji.Sasa iweje Shirika la Usafirishaji la Mkoa wa Dar es Salaam lisiwe chini ya Wizara ya Uchukuzi?

Nasema tena kuwa hadi leo bado siamini maneno ya Dr.Mwakyembe. Siyaamini kwakuwa yanatisha sana. Inawezekana wapo Mawaziri ambao hawajui wanaowaongoza. Sasa wanaongozaje? Sakata la UDA 'lilishazimwa' kimahakama.Hakukuwa na sababu za kukana haraka vile. Nitoe wito kwa viongozi wetu-wa ngazi zote kutambua wanaowaongoza/wanavyoviongoza ili uongozi wao uwe na maana,tija na faida.
 
mwakyembe ile sumu aliyowekewa naona inamchanganya mpaka anakuwa msahaulifu sikuizi,ukijumuisha na kuikana dessertation yake iliyompa phD kwenye bunge la katiba.inanitia mashaka uwezo wake wa maamuzi na utambuzi wa daktari huyu nguli wa sheria.
 
Ndugu zangu siyo kweli mnachoamini hapo. Dkt. Mwakwembe anamaanisha hivyo anavyomaanisha. Kama amekataa kuhusu UDA, yawezekana siyo chombo ambacho kimo ndani ya wizara yake. Mbona Vyombo vingine vimeainishwa katika taarifa na bajeti ya wizara yake na kwa nini isiwe hiyo. Unajua watu tusichanganye mambo, fuatilieni kwanza kabla ya kumshangaa mtu. Wizara ina watendaji wengi wakiwemo wakurugenzi wa idara na wataalamu, je sasa iweje wote wakatae
 
Mwakyembe huenda anamaanisha kuwa, kuna nguvu kubwa sana nyuma ya UDA ambayo iko zaidi ya uwezo wa Uwaziri wake, akiigusa tu UDA, anaweza kupoteza unga!!!!!!!!
 
Ndugu zangu siyo kweli mnachoamini hapo. Dkt. Mwakwembe anamaanisha hivyo anavyomaanisha. Kama amekataa kuhusu UDA, yawezekana siyo chombo ambacho kimo ndani ya wizara yake. Mbona Vyombo vingine vimeainishwa katika taarifa na bajeti ya wizara yake na kwa nini isiwe hiyo. Unajua watu tusichanganye mambo, fuatilieni kwanza kabla ya kumshangaa mtu. Wizara ina watendaji wengi wakiwemo wakurugenzi wa idara na wataalamu, je sasa iweje wote wakatae

Kwahiyo UDA iko Wizara gani?
 
Umeishasema UDA ni usafiri dar es salaam na wamiliki walikuwa halmashauri ya jiji pamoja na hazina sasa utasemaje UDA ipo wizara ya uchukuzi,Mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni Mwakyembe hajakosea kwa alichokisema ya kuwa haipo kwenye wizara yake
 
UDA noma sana, kwa hali iliyopo wamiliki wa UDA inaonekana wanaogopewa na kila mtu tena wanajiamini kupita kiasi wakati kwa hali ya kawaida sana inaonekana ulifanyika ufisadi wa kutosha.. ila mwisho wa Saimon Group kuongoza hili shirika ni Oct 2015
 
Umeishasema UDA ni usafiri dar es salaam na wamiliki walikuwa halmashauri ya jiji pamoja na hazina sasa utasemaje UDA ipo wizara ya uchukuzi,Mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni Mwakyembe hajakosea kwa alichokisema ya kuwa haipo kwenye wizara yake
 
Kila nikifanya tafakuri sipati jibu. Tangu jana nimejitahidi kufikiri na kufikiria bila ya kupata nini hasa kilisababisha. Kitendo cha Waziri wa Uchukuzi, Dr.Harrison Mwakyembe kuikana UDA kuwa haiko Wizarani mwake bado sikielewi. Ni usahaulifu au alilenga jambo fulani?

Dr.Mwakyembe ni kati ya Mawaziri wasomi wabobezi ambao Serikali ya Rais Kikwete inao. Ni Msomi wa Sheria ambaye anaaminiwa na kutarajiwa kujua madaraka yake;mipaka ya madaraka yake;walio chini yake na walio nje ya uwanja wake wa kujidai wa Wizara ya Uchukuzi. Uchukuzi ni usafirishaji.Sasa iweje Shirika la Usafirishaji la Mkoa wa Dar es Salaam lisiwe chini ya Wizara ya Uchukuzi?

Nasema tena kuwa hadi leo bado siamini maneno ya Dr.Mwakyembe. Siyaamini kwakuwa yanatisha sana. Inawezekana wapo Mawaziri ambao hawajui wanaowaongoza. Sasa wanaongozaje? Sakata la UDA 'lilishazimwa' kimahakama.Hakukuwa na sababu za kukana haraka vile. Nitoe wito kwa viongozi wetu-wa ngazi zote kutambua wanaowaongoza/wanavyoviongoza ili uongozi wao uwe na maana,tija na faida.

Unamshangaa leo? Juzi juzi tu alikana PhD Thesis yake! Kazi aliyoifanya kwa miaka isiyopungua mitatu kaikana!
 
mwakyembe ile sumu aliyowekewa naona inamchanganya mpaka anakuwa msahaulifu sikuizi,ukijumuisha na kuikana dessertation yake iliyompa phD kwenye bunge la katiba.inanitia mashaka uwezo wake wa maamuzi na utambuzi wa daktari huyu nguli wa sheria.
Kwa wanazuoni, kama mtu akikana andiko lake la PhD taratibu zikoje ili mtu huyo aweze kuendelea kutambilikana miongoni mwenu. Je ni kweli kuwa mtu huyo itambidi aandae andiko lingine ili atunukiwe PhD halali?
 
kabla ya kuandika jipya anajivua kwanza UDAKTARI wake , amekwishafanya hivyo ?
 
Mwakyembe ni mganga njaa tu,mnafiki wa kutupwa,rejea ishu ya RICHMOND mpaka leo kizungumkuti.
 
kabla ya kuandika jipya anajivua kwanza UDAKTARI wake , amekwishafanya hivyo ?
Nafikiri chuo alichosoma ndo wanajukumu la kumvua hiyo degree waliyomtunuku, Ref: Mgabe vs Vyuo vya uingereza. Kwa hiyo nategemea UDSM imvue huo udaktari na kumwamru aandike thesis nyingine kama atahitaji kuwa daktari tena.
 
Mkuu,Dr.Mwakyembe amesomea Shahada yake ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Hamburg,Ujerumani. Na si UDSM.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom