MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 847
Ubaya wa vyama vya siasa Africa ni kwamba natural defense mechanism kwa chama kilicho shindwa uchaguzi ni kusema kura ziliibiwa. Ndiyo maana 2011 Ivory Coast tuliona maajabu pale chama kinacho shikilia dola kika shindwa na kudai wapinzani waliiba kura:crazy:. Ukweli ni kwamba vyama vya siasa Africa, hata Tanzania havipendi kufanya vitu scientifically kama vile polls na survey ili kujipima na sijui kwa nini. Vinaendeshwa zaidi na hisia ndiyo maana hata pale wanapo shindwa kihalali wanaona wameibiwa.