Napenda kueleza kuwa mimi ni mfuatiliaji sana wa siasa za Kenya. Namshangaa Odinga kulalamika kuwa amedhulumiwa kwenye uchaguzi, anabishana na ukweli. Ukweli ni kwamba siku alipogombana na Ruto ndipo siku alipopoteza urais. Ruto ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa kule bonde la ufa ambalo linakaribia wapiga kura asilimia 30. Huwezi kupoteza rift valley ukawa rais kenya. Odinga alishindwa kumvumilia Ruto ambaye ni a very controversial politician.
Hali hii ya kushindwa kuwavumilia wanasiasa 'controversial" ndani ya chadema itakigharimu sana chama kama ilivyoigharimu ODM. Nimesomo mahali eti chadema bado wanakazania kumfukuza Shibuda. Nina ushahidi pamoja na kwamba hardliners watanipuuza kuwa Shibuda ana ushawishi sana usukumani ambayo inawapiga kura wengi. Hii inatokana na ujasiri wake wa kuwatetea wakulima wa pamba na wafugaji kwa muda mrefu. Lakini Shibuda anazifahamu sana fitna za kisiasa hasa za usukumani. Waulize CCM wanamfahamu, maana hata pamoja na kumfanyia visa vingi, alishinda Maswa kwa kishindo na kupata pia madiwani wengi. Ni ukweli pia kuwa baada ya Chadema kukosana na Shibuda ushawishi wa Chadema kwa Wasukuma umepungua, nina ushahidi, fuatilia hata uchaguzi wa madiwani uliopita.
MI NAONA CDM WAMEMPA UVUMILIVU WA KUTOSHA SANA BUT TUKUMBUKE HATA KUMPA CHANCE YA KUGOMBEA UBUNGE MBOWE ALICHEZA DUME KARATA NA KUMUACHA AIMBE MASHAIRI YA TAARABU SIO MBAYA TUSUBILI 2015 WASUKUMA SIO MASWA TU. KUNA MWANZA,SHY AND TBR